Kutafuta maridhiano kuhusu maswala ya muunguno na kuboresha muungano ni jambo litakalowatafuna CCM milele, hadi hapo watakapokubali kufuata siasa za kisataarabu. Siasa zenye kushirikisha wananchi katika maamuzi muhimu kama haya. Kinyume chake kila Raisi atakaye chaguliwa kuongoza nchi ataonekana wazi ameshakula kiapo cha kufanya mauaji huko Zanzibar. Maana ni apende au asiepende. Na viongozi wa Zanzibar wanatakiwa kukomaa kisiasa zaidi inashangaza wanalambishwa asali midomoni wanaendelea kulamba wanashindwa kabisa kutoa hoja ya wanachokitaka, Wazanzibari wanaye raisi, watanganyika hatuna, wanayo katiba yao, watanganyika hatuna, wanalo bunge lao watangganyika hatuna, wanayo nchi yao watanganyika hatuna. Kilichopo ni serikali ya muungano, Bunge la muungano, Katiba ya muungano, nchi ya muungano nk. Tuliodhoofika zaidi katika hili ni watanganyika.