Zanzibar kumekucha - Abdallah Issa

Zanzibar kumekucha - Abdallah Issa

Huu jamani sio uungwana. Hata sisi ambao sio wanachama wa CUF tunalaani kauli hii ya Karume.
Mgomvi wako keshasalimu amri, wewe bado unataka kumpiga tu????
Aahhh CCM jamani. Acheni mambo hayo na jengeni nchi!
Anyway, sitostaajabu kesho kusikia kuwa Juma Duni ndio Makamu wa Waziri Kiongozi Zenj!
Hebu tutoleeni hio hotuba yote tupate kuichambua. Para moja tu haielezi kitu na pengine labda hizi comments zetu tunakosea!
 
Karume ni rais wa Zanzibar.. hivi anaposema pasipo kushirikishwa Wananchi wake (Wazanzibar) kuna kosa gani?
 
Hebu weka direct quote, audio au video.

Mpaka sasa haijulikani maneno halisi aliyosema Karume ni yapi.
 
Karume ni rais wa Zanzibar.. hivi anaposema pasipo kushirikishwa Wananchi wake (Wazanzibar) kuna kosa gani?

Hakuna kosa, lakini hio Nd. Mkandara ni kusema in a political jargon kuwa hataki hicho wanachokitaka CUF.
Anyway, simlaumu Karume sana. Wakulaumiwa ni CUF. CUF waited too long to go back to their proper senses and see the truth!!!
Huko Zenj Karume alikuwa hana lake tena. Waliomtegemea kuwa angekuwa KIDUME kama baba yake wote walipwerewa zamani. Yeye na Muungwana ni sufuria moja. CUF sasa wamepoteza step na Karume atatamba.
Of course, sote tumefurahi kuwa huu ugomvi umekwisha salama, kwani CUF hawawezi tena kula matapishi yao, but don't under-estimate CCM.This party was founded by Mwalimu Nyerere and we all know how clever he was!!!
 
Hebu weka direct quote, audio au video.

Mpaka sasa haijulikani maneno halisi aliyosema Karume ni yapi.

Nadhani hii habari ina toka hapa....

Karume awakana CUF kweupe
Mwinyi Sadallah
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume, amesema hakuna maamuzi yanayohusu maslahi ya nchi yatakayoamuliwa bila ya kushirikishwa wananchi wake.
Rais Karume aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kibandamaiti kufuatia mazungumzo yake ya kumaliza mpasuko wa kisiasa wa Zanziabr kati yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
Alisema katika muafaka mpya uliopatikana, hakuna mshindi kwa vile mazungumzo hayo yamezingatia maslahi ya nchi na kuendeleza sera ya CCM ya kudumisha amani na mshikamano kwa wananchi wake.
“Tunaamini amani ya kudumu imefika Zanzibar mafanakio haya ni ya vyama vyote na Wazanzibari wote hamna mshindi katika hilo, ushindi huwa katika uchaguzi sio katika suala la amani,” alisema.
Alisema katika mazungumzo hayo, hakuna jambo jingine walilokubaliana zaidi ya kuzungumzia misingi ya kudumisha amani na utulivu kwa wananchi wa Zanzibar.
“Hakuna jingine katika mazungumzo hayo isipokuwa suala la amani na utulivu lilikuwa na nafasi kubwa na hilo siyo dogo wanaobeza waache,” alisema Rais Karume.
Hata hivyo, alisema kama kutakuwa na jambo lolote linalohusu Zanzibar, wananchi ndiyo watakuwa waamuzi wa suala hilo kwa vile viongozi kazi yao ni kuzungumza na siyo kufikia uamuzi.
Rais Karume alisema anaamini wananchi wa Zanzibar hawawezi kukataa jambo lolote lenye maslahi kwa nchi lakini alisema mtu unaweza kukataa pale mwingine atakapoamua kukulazimisha, kula biriani wakati wa asubuhi badala ya chai na vitafunio vyake.
“Kama jirani yako atakujia asubuhi na mapema na kukukaribisha chakula cha biriani na akakulazimisha, basi utakataa kwa kuona kuwa kina madhara ndani yake kwa vile biriani huliwa mchana,” alisema.
Hata hivyo, hakufafanua zaidi lakini alisema hakumwita Katibu Mkuu wa CUF Ikulu bali alimtolea salamu akiomba kutaka kuonana naye na kumpa nafasi hiyo.
Alisema baada ya kukutana na Maalim Seif Ikulu, alimpa nafasi ya kumsikiliza na kumueleza Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeamua kumaliza tofauti za kisiasa na badala yake washirikiane kujenga nchi.
“Tumekaa Baraza Kuu la Uongozi tumeona nchi imetulia na maendeleo tumeyaona hivyo tukiendelea kushirikiana maendeleo yataongezeka zaid,” alimkariri Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif katika mazungumzo yake.
Rais Karume alisema baada ya kuwasilisha ujumbe huo, Maalim Seif aliomba amuombee dua kwa vile anakwenda kutoa uamuzi mzito mbele ya wanachama wake na kutoa ahadi ya kutekeleza ombi hilo. “Pale pale nikamwambia nashukuru kuniambia maneno yako na siku zote nimekuwa nikikuombea dua njema,” alisema Rais Karume huku akishangiliwa na wanachama wa CCM.
Hata hivyo, alisema katika mazungumzo yake yaliyofanyika Novemba 5, mwaka huu, Ikulu, hakumpa chai ya maziwa kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu, baada ya kufikia uamuzi wa kumtambua kuwa Rais halali wa Zanzibar.
“Hakuna chai wala uji bali alikunywa maji glasi moja na mie moja,” alisema Rais Karume na kuongeza kuwa wanachama wote wa CUF wamuunge mkono Hamad kufuatia uamuzi wake wa kuamua kusahau tofauti na kujenga umoja wa kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari.
Alisema uamuzi wa Hamad umeleta faida kubwa kwa Zanzibar kutokana na hatua hiyo kuungwa mkono na mataifa mbalimbali zikiwemo nchi wahisani kwa vile upinzani sio ugomvi bali ni kusukuma mbele maendeleo.
“Upinzani sio ugomvi, upinzani sio vita bali ni kutofautiana mawazo kwa lengo la kuharakisha maendeleoa kwa wananchi,” alisema.
Alisema kimsingi CUF wamekuwa wakimtambua muda mrefu kwa vile wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekuwa wakishirikiana na mawaziri katika vikao vya baraza lake tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz, alisema Rais Karume amejitahidi kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo katika kipindi cha uongozi wake.
Alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, bandari ya Malindi, Uwanja wa Ndege pamoja na mradi wa umeme vijijini hatua ambayo itasaidia katika utekelezaji wa mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
Aidha, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Yussuf Mohammed, aliwataka wanachama wa CCM waiombee dua CCM iendelee kushinda maisha.
Mkutano huo ulikuwa umepambwa na mabango yanayosomeka ‘Tunakupongeza Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar kwa hekima, busara zako na uwezo mkubwa wa kusukuma umoja na mshikamano wa nchi yetu’.
Aidha, mabango mengine yalisomeka ‘Chagua Chama cha Mapinduzi kwa maendeleo yako, Mchague mgombea wa CCM mwenye sifa achana na wababaishaji, Sera ya CCM ndiyo ukombozi wa umasikini'.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamuhuna na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo mawaziri na viongozi wa chama.

NIPASHE
 
MwnaFalsafa1,
Mkuu kuna kitu gani hapa ambacho hakikueleweka toka mwanzoni?.. mbona alozungumza Karume ndivyo nilivyoelewa mimi toka mwanzo na nikafikia kumlaumu Maalim Seif.. Karume alimwalika Sief asubuhi akampa mix safi sana ya chai, chapati, samaki wa kukaanga, maamri na juice ya embe, mkuu katoka pale na shibe yake leo mlitegemea Seif angebeba nini toka ktk mwaliko ule?.

Mshindi hapa NI CCM na hata siku moja siwezi under-estimate CCM kwa sababu naelewa wazi kwamba CCM is a system iliyo kamilika tofauti na vyama vyote..Karume kuwmalika Sief alishapata baraka zote za baraza la Mapinduzi wakati Maalim Seif aliangalia tumbo lake...Sana sana pengine kaahidiwa kuwa Waziri kiongozi ktk Uchaguzi Ujao, jambo ambalo haliwezekani na halitawezekana.
 
Nilijua hili dili kanyaboa kwa CUF, my personal assesment ni kwamba...CUF 2010 ndio mwisho wenu kote kote...kutakuwa na ugomvi mkubwa kati ya wanachama na viongozi..expect the huge split in future..
 
Lakini lipumba alisema makubaliano kati ya seif na karume ni pata potea
 
Waombeeni
makubaliano yao yapeleke tija kwa wazanzibar, watu bwana mnatia mikosi wakati hata gari halijainuka bwana.

waombeeni mazuri sio ku expect negative, watanzania bwana
 
Waombeeni
makubaliano yao yapeleke tija kwa wazanzibar, watu bwana mnatia mikosi wakati hata gari halijainuka bwana.

waombeeni mazuri sio ku expect negative, watanzania bwana
Ndugu, swala siyo maombi hapa swala ni makubaliano ya kulazimisha..CUF wangebaki na hardcore rules kwasababu haki haiombwi ..tatizo wanataka short-cut..no way CCM watawapiga tena changa la macho..na watasambaratika vibaya baada 2010 ..take my word...
 
Ndugu, swala siyo maombi hapa swala ni makubaliano ya kulazimisha..CUF wangebaki na hardcore rules kwasababu haki haiombwi ..tatizo wanataka short-cut..no way CCM watawapiga tena changa la macho..na watasambaratika vibaya baada 2010 ..take my word...

Mkuu
Mimi nafikiri alichokifanya Maalim ni cha kuigwa na alitakiwa kufanya hivyo mda mrefu. Nikiwa namaana lengo hasa la uongozi ni watu wakukubali kuwaongoza ktk hali tulivu na yenye maelewano baina ya wananchi. Bado nafikiri ni bora ccm ama cuf wasambaratike kuliko ccm ama cuf kuwa na nguvu wakati wananchi tumesambaratika.

Alichokifanya Maalimu labda ni kitu haba kinachokosekana viongozi wengi wa afrika yani kulazimisha kuwaongoza wananchi hata kama hawako tayari kuongozwa nao.

Nafikiri kwa wakati huu swala zinahitajika ili hata kama Karume kama anania nyingine Mungu apate kumukumbusha na hatimaye kurudi ktk makubaliano yao ya kuipeleka Zanzibar mbele.

Kuunza kutia mikosi na shutuma mapema namna hii nafikiri sio mwafaka.
 
Kila gazeti limeandika linavyo juu kwa elimu zao za Buguruni na amana ilala.alicho zungumza Mh karume ni kama kiongozi wa Znz na siyo kama mwana CCM!!!
 
MkamaP,
Mkuu hapa sikukuelewa kidogo ujnaposema 'Bado nafikiri ni bora ccm ama cuf wasambaratike kuliko ccm ama cuf kuwa na nguvu wakati wananchi tumesambaratika.

Makubaliano ya Maalim na Karume yamewaunganisha wao CUF na CCM na kuwaacha waanachi wakisambaratika..Ni hali ilyiotokea Zimbabwe na Kenya ambayo kisiasa kweli inafaa sana lakini wananchi wenyewe ndio wamejenga uhasama zaidi na hata kuleta chuki kwa viongozi wao wenyewe. Amini maneno yangu Raila wa juzi hapindwi na Wahjaluo tena na huyo Morgan ndio kabisaaa, nilimhisi toka zamani kwamba yeye na Maalim Sief hawana tofauti.
 
MkamaP,
Mkuu hapa sikukuelewa kidogo ujnaposema 'Bado nafikiri ni bora ccm ama cuf wasambaratike kuliko ccm ama cuf kuwa na nguvu wakati wananchi tumesambaratika.

Makubaliano ya Maalim na Karume yamewaunganisha wao CUF na CCM na kuwaacha waanachi wakisambaratika..Ni hali ilyiotokea Zimbabwe na Kenya ambayo kisiasa kweli inafaa sana lakini wananchi wenyewe ndio wamejenga uhasama zaidi na hata kuleta chuki kwa viongozi wao wenyewe. Amini maneno yangu Raila wa juzi hapindwi na Wahjaluo tena na huyo Morgan ndio kabisaaa, nilimhisi toka zamani kwamba yeye na Maalim Sief hawana tofauti.

Tatizo la Raila
ni mviziaji navyofikiri kama walivyo viongozi wa chadema, yani yeye alipopata uwaziri mkuu anataka kuwapeleka jela akina William Rutto, maana anajuwa akimwacha rutto basi Ruto ana sapoti ya wakalenjing ambao ya wenzekana wakawa wengi kuliko jamii nyingine kenya.

Na anachokifanya Raila ni kuwanyofoa wafuasi wote wa Ruto na ruto mwenyewe kitu kinachofanywa na vhadema yetu. Na saizi Raila hapendwi tena.

Tukirudi ktk kwetu ugunja na pemba ,mkuu wangu Maalimu kweli ni maalimu haswa ana busara, effect ya yeye kuwa ngangari ni kubwa mno kuliko akiwa ngunguri. Maana ya kwamba si kweli wapemba na wa unguja hawapendani kijamii ila inapokuja kisiasa ndo wanachukiana.

Hii ni sawa mnapokuwa ktk uwanja wa mpira wewe na mdogo wako na mbaya zaidi mkiwa ktk timu pinzani mle mtapigana viatu balaa na tena kurushiana ngumi wewe na mdogo wako mle uwanjani ni swala la kawaida,lakini mkirudi nyumbani utafikiri vile hakuna kilichotokea. hii kwanini uwanjani mnarushiana nguni na mabuti.? kwa sababu ile ina maslahi tofauti na vionjo tofauti. Kumbe muaandaaji wa mechi akiepusha kuandaa mechi za namna hii tafrani haitatokea .

Kinacho watengenisha wapemba na wa unguja si sababu za kijamii ni vionjo vya kisiasa ambavyo mara nyingi husababishwa zaidi na wakuu wa vyama.

nikupe mfano mimi mkatolic na wewe muislamu na tukikutana tukabishana mambo ya dini mtu mwingine anaweza fikiri sie ni maadui, kumbe wapi vile ni vionjo vingine vya kidini ,lakini tukitoka hapo utashangaa kabisa.

Watanzania kwa ujumla hatuna ubaguzi wowote sisi kwa sisi, hakuna utengano wa ki mahali(pemba ama ugunja), hatuna wa kidini na wala wa kikabila. Ila vionjo vinapokuwa stimulated na wapambe kuvitia chumvi basi inaonekana eti kuna uwadui wakati ni vitu vya kawaida.

Wewe pale Nansio hamjawahi kupigana fimbo na timu pinzani ama timu ya kijiji cha pili kama vile ukalani.?

Nakumbuka mechi hizi nusra watu tulikuwa tunatoa roho kwa fimbo.
Pia huwezi niambia mashabiki wa yanga na simba ni maadui ktk maisha yao ya kawaida ila ktk vionjo vya mchezo huwa maadui.

Hivyo Maalimu kutaka kuviondoa hivi vionjo ni kwamba cuf ama ccm zinaweza sambaratika lakini wananchi kutokana na vionjo hivyo kutokuwa stimulated basi amani tupu hakuna tena kukimbilia mombasa.
 
Ni uwongo kuwa Karume kawakana CUF,mnachokijadili si kilichotokea mkutanoni bali Mwinyi Sadalla na Mhariri wake kuuza gazeti lao kwa heading ya kifitna fitna kama hiyo. Nimekuja Zanzibar siku mbili kabla ya mkutano huo na nimeufuatilia live kupitia redio Zanzibar na TVZ, sijaona wala sijasikia Karume kusema kuwa amewakana CUF na kama suala la maslahi ya Zanzibar, rais Karume alikuwa sahihi kuwaambia wafuasi wake kuwa ni wazanzibar wanaopaswa kuamua mustakbali wao, poleni kwa wale waliokuwa hajamuwelewa rais Karume alikusudia nini, provided kuwa wananchi wote wameunga mkono hatua hiyo, na risala iliyosomwa kwa niaba ya wana CCM wa mikoa mitatu ya Unguja, ilionyesha wazi kuwiana na kauli ile ya Maalim Seif Shariff Hamad na yeye rais Karume aka acknowldge hatua ya Katibu Mkuu wa CUF kama ni ya kijasiri, Mwinyi Sadalla na Mhariri wake wameuza gazeti lao na sisi tumewaelewa viongozi wetu kwa kuwa tumewasikia kwa masikio yetu na hatujahadithiwa na wala kusoma porojo za waandishi wa habari wanaochunga mkate wao...mbona hawakusema kuwa rais Karume amewaambia wafuasi wake kuwa "...alichosema Maalim Seif katika viwanja hivihivi ni sahihi..."
 
Junius,
Hata mimi sikuona Karume akiwakana CUF isipokuwa alichosema ndicho kilikuwa ktk makubaliano yake na Maalim Seif. Wengi hapa hawakubaliani na maelezo aliyotoa sasa nakuomba wewe useme kitu tofauti na bandiko lilowekwa hapo juu.

MkamaP,
Mkuu wangu hujui Historia ya nchi ile na huwajui Wapemba na Waunguja kwa undani wao. Ni sawa na Wasomali huungana wanapokuwa na adui toka nje, lakini wao kwa wao uadui wao ni wa asili na hakuna mtu toka nje anayeweza kuwapatanisha..Karume ni mtu wa nje hawezi kubeba mzigo wa Waunguja isipokuwa anafanya kwa maslahi ya CCM..and That is the fact.
 
Mkandara,
Nafikiri nimeshaeleza hapo juu kuwa walichoripoti Nipashe ni biashara na maudhui ya hotuba ya rais Karume ambayo mi binafsi nimeisikiliza yalikuwa sawia na yale tuliyosikia kutoka CUF wenyewe na vyombo vya habari hapa nyumbani vimeweka kama ilivyokuwa, ukiachia hamasa za kisiasa za hapa na pale,kama pale rais Karume alipodai kuwa eti ni Maalim Seif ndiye aliyeomba mazungumzo hayo,wakati watu wa jikoni tunajuwa nini kiliendelea kabla, wanasiasa wamebaki na sehemu yao kama hiyo ya kuwafurahisha wafuasi wao wajione kuwa hawakupoteza na hilo hata sisi tumefanya kaitka mkutano wa awali. Hii ni sehemu ya stori ya mwandishi mmoja kutoka zanzibar, da salma.....

Juzi akihutubia mamia ya wazanzibari Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume aliwataka wananchi na wapenda amani kuunga mkono mazungumzo kati yake na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ambayo yanalenga kumaliza tofauti zao za kisiasa na kujenga umoja na mshikamano nchini.
Rais Karume aliwakumbusha wananchi kwamba kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta nafasi ya kumaliza matatizo lakini sasa wakati umefika hivyo kuwataka wananchi wote bila ya kujali tofauti zao za kisiasa kushirikiana na kujenga Zanzibar mpya ambayo itawashirkisha wananchi wote
 
Junius,
Nakukubali mkuu wangu lakini unaweza nambia mazungumzo hayo yameleta Amani gani kwa wananchi? Yaani unataka kunambia siku zote wananchi mlikuwa hamkubali Urais wa Karume kwa sabau zipi haswa! je, hizo sababu zenu zimetikmizwa au Maalim Seif kawakilisha kipi ambacho kimerudisha Amani baina yenu.

Mkuu mimi marafiki zangu wa karibu ni Wanzabar na wafahamu kwa tabia na hulka zao kwamba hawana Uhasama wowote ambao umetakiwa makutano haya. Tena wao wanaungana kwa ukaribu zaidi kuliko Bara kama jamii moja..Uhasama ulokuwepo ni wa Kisiasa na sii wananchi wake kwani hadi sasa hivi matatizo ya Asili hayapo ktk agenda za Mzanzibar yeyote. hakuna Uhasama wowote sipokuwa ule wa Kisiasa..sasa nambie hayo mazungumzo yanaleta Amani ipi ikiwa wananchi wenyewe wana Amani muda wote isipokuwa pale tu Siasa zinapoingia kati.
 
Back
Top Bottom