Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
LOL wao nasikia wanaanzisha ya kwao Bongo
Ukirudi na wewe utapewa connection ya vijisenti na kelele zako zote zitaisha.
LOL wao nasikia wanaanzisha ya kwao Bongo
daraja la nini wakati hatuna maji ya kunywa?
Ukirudi na wewe utapewa connection ya vijisenti na kelele zako zote zitaisha.
forward and backward economic linkages - trade (karafuu, mwani, utalii, uvuvi n.k)
"Now it [Zanzibar] lags far behind Indonesia and Madagascar for the spice, used in cigarettes such as those known as kretek in Indonesia, perfume, cooking and herbal medicine" - Zanzibar clove farmers still await free market | Reuters
Na bandari ya Zanzibar itakuwa na kazi gani wakati huo?
kwani daraja linaondoa ulazima wa bandari?
Wakati mwingine inabidi kujiuliza kama tunajiamini tunaweza au tunasubiri wengine waamue tunaweza.. NSSF na wadau wengine kama mko serious kwa hili you have my support....
Tumeanza na daraja la Kigamboni kuunganisha pande mbili za jiji la Dar es Salaam. Soon tutahamia ujenzi wa daraja la Bara na VisiwaniWakati mwingine inabidi kujiuliza kama tunajiamini tunaweza au tunasubiri wengine waamue tunaweza.. NSSF na wadau wengine kama mko serious kwa hili you have my support....
Siku ukigombea nitakupa kula zangu na familia yangu na ndugu zangu ....nimekua nikifikilia hiki kitu ...nikaamua kusesearch uzi wa kuhusu idea ya kujenga daraja n nikauona ....big up mkuuBila ya shaka utakuwa umesikia leo taarifa ya lile daraja refu zaidi kupita bahari limefunguliwa huko China leo. Daraja hilo liitwalo Daraja la Qingdao Jiazhou lina urefu wa kilometa 42 (sawa na umbali wa mbio za marathoni) kama mile 26 hivi. Daraja hilil la China la kisasa kama picha zinavyoonesha limejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.5 (karibu na shilingi za Kitanzania Trilioni 2 na ushee). Daraja hili lilianza kujengwa mwaka 2006 na limekamilika mwaka 2011 kama ilivyotarajiwa.
(Picha zote na AP na Reuters)
Tunajifunza Nini?
a. Bahari si kikazo cha kuunganisha sehehu mbili za nchi moja.
b. Gharama ya kujenga daraja kama hili kuunganisha Tanzania moja ziko ndani ya uwezo wetu na ninaweza kuargue kuwa tunaweza kufanya kwa fedha zetu wenyewe japo utaalamu na wataalamu tunaweza kuwashirikisha rafiki zetu wa China - tukiwapa BAES!
c. Gharama ya dola bilioni 1.5 ni sawa na fedha zilipotea katika ufisadi kwa mwaka mmoja uliopita tu. Tukichanganya fedha zilizopotea kwa miaka kumi iliyopita tungeweza kabisa kuunganisha Zanzibar mara tatu - kutokea Tanga kwenda Pemba, kutoka Dar (au Bagamoyo-the closest points to the mainland from Unguja?) na Pemba na Unguja! - by the Way kwa miaka kumi iliyopita ufisadi umegharimu zaidi ya bilioni 10 (dola!!)
d. Kwenye kile kinachoitwa Mpango wa Maendeleo ambao uko tayari kutumia shilingi trilioni 42 hakuna mpango wa kuthubutu kama huu.
e. Tunapoelekea miaka 50 ya Uhuru hakuna kitu kitakachoonesha Muungano wetu kuwa umehimiri vishindo na matatizo kama kuzinduliwa kwa daraja la Muungano (Union Bridge) japo sehemu yake mwaka 2014 huku likikamilika 2015.
f. Naamini ujenzi wa daraja/madaraja ya kuunganisha Zanzibar na Bara utasaidia sana katika kuleta maendeleo visiwani na kuusogeza ule udugu wa damu kati yetu karibu zaidi kwani kwa mara ya kwanza bahari itaondolewa kama alama ya kutengana kwetu, watu wa Zanzibar na bara wataweza kwenda nchini mwao wakati wowote na mahali popote bila kutishiwa sana na masuala ya usalama kama ilivyo sasa.
g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.
Maswali ya Kutafakari:
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
Je, Rais Kikwete anaweza kuja na mpango kama huu madhubuti wakati daraja la kuunganisha Kigamboni na Kivukoni tu pale limeshindikana hadi hivi sasa licha ya kuwa katika mipango kwa muda mrefu?
Je, yawezekana wazo hili haliwezi kuletwa, kutetewa wala kusimamiwa na viongozi wetu wa sasa - kwani hawana uwezo wa kulisimamia kama Nyerere alivyosimamia kujengwa kwa reli ya Uhuru (of course lazima nirushe dongo kidogo tu!)?
Je, yawezekana Chama cha Mapinduzi kimepoteza kabisa uwezo wake wa kuthubutu mambo makubwa na sasa kimeamua kufanya mambo madogo kama "mabarabara ya juu kwa juu"?
Je, tusubiri uongozi mpya ambao utakuwa tayari kuliunganisha taifa letu.
Jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo kwa kuangalia China ni kuwa inawezekana kuunganisha kwa daraja umbali wa kilomita 42 (au hata zaidi) kwani Zanzibar iko kati ya Maili 16-31 sawa na kilomita 25-50 hivi (kutegemeana na eneo unalosimama kutoka bara). Hii ina maana tukiangalia mahali ambapo ni shortest distance. Hivyo swali la kama inawezekana kiteknolojia au vinginevyo limeshabiwa. Kwa upande wetu ni swali la kisiasa zaidi - je tuna viongozi ambao wanaweza kubuni, kusukuma na kusimamia mpango huu?
UPDATE - OKTOBA 23, 2018
Wachina wamezindua daraja jingine leo hii ambalo lina umbali wa maili 34 (zaidi ya kilomita 60). Je, wamewezaje? Daraja hili jipya linaenda kuviunga visiwa vya Hong Kong na Macau na China Bara... Unguja na Pemba ziungwe na Bara kwa namna hii?
View attachment 908357
Tayari inasemekana mchakato tayariwewe jamaa huwezekaniki aisee
wameshindwa kusupply umeme wa uhakika kwenye % isiozidi 20 ndani ya population ya watu mil.40 .sembuse hii kitu?