Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 30, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Bila ya shaka utakuwa umesikia leo taarifa ya lile daraja refu zaidi kupita bahari limefunguliwa huko China leo. Daraja hilo liitwalo Daraja la Qingdao Jiazhou lina urefu wa kilometa 42 (sawa na umbali wa mbio za marathoni) kama mile 26 hivi. Daraja hilil la China la kisasa kama picha zinavyoonesha limejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.5 (karibu na shilingi za Kitanzania Trilioni 2 na ushee). Daraja hili lilianza kujengwa mwaka 2006 na limekamilika mwaka 2011 kama ilivyotarajiwa.

  [​IMG]

  [​IMG]

  (Picha zote na AP na Reuters)

  Tunajifunza Nini?

  a. Bahari si kikazo cha kuunganisha sehehu mbili za nchi moja.
  b. Gharama ya kujenga daraja kama hili kuunganisha Tanzania moja ziko ndani ya uwezo wetu na ninaweza kuargue kuwa tunaweza kufanya kwa fedha zetu wenyewe japo utaalamu na wataalamu tunaweza kuwashirikisha rafiki zetu wa China - tukiwapa BAES!
  c. Gharama ya dola bilioni 1.5 ni sawa na fedha zilipotea katika ufisadi kwa mwaka mmoja uliopita tu. Tukichanganya fedha zilizopotea kwa miaka kumi iliyopita tungeweza kabisa kuunganisha Zanzibar mara tatu - kutokea Tanga kwenda Pemba, kutoka Dar (au Bagamoyo-the closest points to the mainland from Unguja?) na Pemba na Unguja! - by the Way kwa miaka kumi iliyopita ufisadi umegharimu zaidi ya bilioni 10 (dola!!)
  d. Kwenye kile kinachoitwa Mpango wa Maendeleo ambao uko tayari kutumia shilingi trilioni 42 hakuna mpango wa kuthubutu kama huu.
  e. Tunapoelekea miaka 50 ya Uhuru hakuna kitu kitakachoonesha Muungano wetu kuwa umehimiri vishindo na matatizo kama kuzinduliwa kwa daraja la Muungano (Union Bridge) japo sehemu yake mwaka 2014 huku likikamilika 2015.
  f. Naamini ujenzi wa daraja/madaraja ya kuunganisha Zanzibar na Bara utasaidia sana katika kuleta maendeleo visiwani na kuusogeza ule udugu wa damu kati yetu karibu zaidi kwani kwa mara ya kwanza bahari itaondolewa kama alama ya kutengana kwetu, watu wa Zanzibar na bara wataweza kwenda nchini mwao wakati wowote na mahali popote bila kutishiwa sana na masuala ya usalama kama ilivyo sasa.
  g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.


  Maswali ya Kutafakari:
  Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
  Je, Rais Kikwete anaweza kuja na mpango kama huu madhubuti wakati daraja la kuunganisha Kigamboni na Kivukoni tu pale limeshindikana hadi hivi sasa licha ya kuwa katika mipango kwa muda mrefu?
  Je, yawezekana wazo hili haliwezi kuletwa, kutetewa wala kusimamiwa na viongozi wetu wa sasa - kwani hawana uwezo wa kulisimamia kama Nyerere alivyosimamia kujengwa kwa reli ya Uhuru (of course lazima nirushe dongo kidogo tu!)?
  Je, yawezekana Chama cha Mapinduzi kimepoteza kabisa uwezo wake wa kuthubutu mambo makubwa na sasa kimeamua kufanya mambo madogo kama "mabarabara ya juu kwa juu"?
  Je, tusubiri uongozi mpya ambao utakuwa tayari kuliunganisha taifa letu.

  Jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo kwa kuangalia China ni kuwa inawezekana kuunganisha kwa daraja umbali wa kilomita 42 (au hata zaidi) kwani Zanzibar iko kati ya Maili 16-31 sawa na kilomita 25-50 hivi (kutegemeana na eneo unalosimama kutoka bara). Hii ina maana tukiangalia mahali ambapo ni shortest distance. Hivyo swali la kama inawezekana kiteknolojia au vinginevyo limeshabiwa. Kwa upande wetu ni swali la kisiasa zaidi - je tuna viongozi ambao wanaweza kubuni, kusukuma na kusimamia mpango huu?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,931
  Trophy Points: 280
  wewe jamaa huwezekaniki aisee
  wameshindwa kusupply umeme wa uhakika kwenye % isiozidi 20 ndani ya population ya watu mil.40 .sembuse hii kitu?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kabla ya hilo daraja hapo juu kuna watu waliangalia bahari wakafikiria; halafu akawashirikisha wenzake, wakaona mantiki, wakaenda mbele, wakafikiria wakaona ni feasible, wakaenda mbele na kufanya upembuzi yakinifu wakaona na gharama, wakaweka sera, wakaweka bajeti, wakaanza mchakato miaka mitano baadaye daraja hilo hapo. Remember ni chini ya chama kimoja!!!
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Stimulus package ya Tanzania ilikuwa around Tsh 1.7 trillions. Ukijumlisha na hivi vijicent vinavyopotea EPA, Kagoda, Meremeta, Rada, Vasco da Gamma travels, vitafunwa na ndugu na jamaa wote wanaohusika, Tanzania inaweza kabisa kugharamia Daraja kama hili. In fact umbali wa DAR-Zanzibar ni 40km. (2km less than huu umbali wa daraja china). But being a nation cursed with non-visionary leadership tutaendelea kusoma China leo, Cambodia kesho, Malayasia keshokutwa. Maybe we should try the other household- CDM that is!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Daraja la kutoka Magogoni hadi Kigamboni ambapo hata umbali wake haufiki kilomita moja, limetushinda.Viongozi wetu hawana uzalendo, dira wala dhamila ya kuleta maendeleonchini.
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wazo lako ni zuri Mwanakijiji. Daraja linaweza likaitwa Daraja la Umoja na nadhani lingeweza kuwa njia moja wapo ya umoja wa kweli. Tatizo ubabaishaji wa Bongo na quality ya ujenzi wetu naogopa litadondokea watu.
   
 7. Moses Kyando

  Moses Kyando Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good job Chinese
   
 8. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Tuna miaka 50 tokea kupata Uhuru pale Kigamboni tumeshindwa kujenga kadaraja tunafikiria kuunganisha Bara na Znz? Mhh hilo haliwezekani hata tukiwa na pesa zitawekewa miradi ziliwe.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Muungano wenyewe sasa hivi unatumia ARV kuongeza urefu wa maisha. teh teh teh

  Hilo wazo japo ni zuri hata bila muungano kuna upande utapinga kwa nguvu zote.
   
 10. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Naruhusu tuongee na Bill Gate ingawa kaja kinyemela atujengee daraja la Magogoni- Kigamboni bila masharti.
   
 11. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri pesa za kulijenga zitapatikana tukianza kuchimba mafuta 'yetu'
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Daraja kati ya Tanzania na Msumbiji ni kwa sababu hizi mbili ziko kwenye Muungano?
   
 13. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wazo hili angekuwanalo Mkapa naamini angethubutu,pamoja na udhaifu wake mwingine lakini kwa hilo angeweza
   
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuh... aisee, hii kiboko!!! lol :second:
   
 15. Romance

  Romance JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 587
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  naona ndio uzuri wa kujijengea reputation ya u GT angeweka hu uzi hapa mwingine angeonekana anaongea pumba na mashambulizi kibao.
   
 16. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka hii ilikuwa ni sera kuu ya Dr. (Mzee) Chemponda wakati ule ananadi chama chake ..
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tusifikiri kidogo, tusijifunge kwenye kufikiri vidogo; CCM imetufanya tufikiri kidogo, viongozi wetu hawafikiri tena makubwa! wanataka ya wastani! Well mataifa ya kisasa hayajengwi na watu wenye kufikiri kidogo au kwa wastani! Muungano ukivunjika mnaweka vituo vya mpaka na forodha katikati ya bahari kwenye hizo barabara! au hili linahitaji ugenius kulifikiria nalo? Au Muungano ukivunjika maana yake Zanzibar inazama baharini!?
   
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Kaka jina la daraja ni Jiaozhou Bay Bridge . hiyo Qingdao ni mji mabapo hilo daraja lipo.

  he world longest cross-sea bridge, Jiaozhou Bay Bridge, and the subsea tunnel is scheduled to be put into operation in Qingdao, East China's Shandong Province, on Friday, and more than 30 local residents experienced a journey cross the bridge and tunnel on Tuesday.

  Transcending 41.58 kilometers over the sea with a width of 35 meters, the Jiaozhou Bay Bridge is the longest of its kind in the world, with a life expectancy of 100 years.
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi mnafikiria huko China hakuna ufisadi? Au China viongozi wote ni wazuri na wazalendo?
   
Loading...