Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Kwa uongozi tulioao huu wa Sindbad baharia tusitegemee vitu kama hivi...na huwa wanaenda China sijui huwa ni kushangaa bila kuchukua hatua......Kifupi hawawezi si kuwa na Strategy ya kujenga kitu kama hii bali hata sidhani kama wameshwahi "kujaribu" Kufikiria kitu kama hii...Wao ni posho na kuelekeza fedha katika miradi ambayo watasimamia wao wenyewe....Hiyo kitu imejengwa na kampuni ya wachina tena ya SHANDONG hapo hapo....Hawa jamaa kila mji una kampuni ya ujenzi katika mji husika mali ya Serikali...Kuanzia barabara, Majumba na hiyo kampuni ni kwa ajili ya HIGHWAY tu!!! SWALI NI SERIKALI YETU (yao) INAMILIKI NINI????????? Usinijibu TRA....p'se....
 
Ndugu yangu hizi ni kelele za mfa maji, taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa kuna mkakati wa nguvu (tena una ufadhili wa nchi moja ya Kiskandinavia) wa kuvunja muungano kwa ajili ya mafuta na inasemekana tukigawana maji ya bahari ndugu zetu watapata eneo kubwa la kina kirefu!
 
Hivi mnafikiria huko China hakuna ufisadi? Au China viongozi wote ni wazuri na wazalendo?

...ufisadi upo sana tu China, ila huko pale mafisadi wanapokamatwa hawaishii kuvuliwa magamba pekee, bali wanang'olewa meno na kuminywa mpaka sumu na tezi zake vyote vinatoweka!!!
 
Bila ya shaka utakuwa umesikia leo taarifa ya lile daraja refu zaidi kupita bahari limefunguliwa huko China leo. Daraja hilo liitwalo Daraja la Qingdao Jiazhou lina urefu wa kilometa 42 (sawa na umbali wa mbio za marathoni) kama mile 26 hivi. Daraja hilil la China la kisasa kama picha zinavyoonesha limejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.5 (karibu na shilingi za Kitanzania Trilioni 2 na ushee). Daraja hili lilianza kujengwa mwaka 2006 na limekamilika mwaka 2011 kama ilivyotarajiwa.

e51fd62d93389c0ef10e6a706700fb3f.jpg


2011-06-30T113121Z_01_PEK07_RTRIDSP_3_CHINA.jpg





(Picha zote na AP na Reuters)

Tunajifunza Nini?

a. Bahari si kikazo cha kuunganisha sehehu mbili za nchi moja.
b. Gharama ya kujenga daraja kama hili kuunganisha Tanzania moja ziko ndani ya uwezo wetu na ninaweza kuargue kuwa tunaweza kufanya kwa fedha zetu wenyewe japo utaalamu na wataalamu tunaweza kuwashirikisha rafiki zetu wa China - tukiwapa BAES!
c. Gharama ya dola bilioni 1.5 ni sawa na fedha zilipotea katika ufisadi kwa mwaka mmoja uliopita tu. Tukichanganya fedha zilizopotea kwa miaka kumi iliyopita tungeweza kabisa kuunganisha Zanzibar mara tatu - kutokea Tanga kwenda Pemba, kutoka Dar (au Bagamoyo-the closest points to the mainland from Unguja?) na Pemba na Unguja! - by the Way kwa miaka kumi iliyopita ufisadi umegharimu zaidi ya bilioni 10 (dola!!)
d. Kwenye kile kinachoitwa Mpango wa Maendeleo ambao uko tayari kutumia shilingi trilioni 42 hakuna mpango wa kuthubutu kama huu.
e. Tunapoelekea miaka 50 ya Uhuru hakuna kitu kitakachoonesha Muungano wetu kuwa umehimiri vishindo na matatizo kama kuzinduliwa kwa daraja la Muungano (Union Bridge) japo sehemu yake mwaka 2014 huku likikamilika 2015.
f. Naamini ujenzi wa daraja/madaraja ya kuunganisha Zanzibar na Bara utasaidia sana katika kuleta maendeleo visiwani na kuusogeza ule udugu wa damu kati yetu karibu zaidi kwani kwa mara ya kwanza bahari itaondolewa kama alama ya kutengana kwetu, watu wa Zanzibar na bara wataweza kwenda nchini mwao wakati wowote na mahali popote bila kutishiwa sana na masuala ya usalama kama ilivyo sasa.
g. Bara nako kutanufaika sana na kufunguliwa kwa njia hii mpya.


Maswali ya Kutafakari:
Je kuna uongozi wowote ndani ya CCM wenye mawazo ya namna hii au mwitikio wa kwanza 'hatuwezi?
Je, Rais Kikwete anaweza kuja na mpango kama huu madhubuti wakati daraja la kuunganisha Kigamboni na Kivukoni tu pale limeshindikana hadi hivi sasa licha ya kuwa katika mipango kwa muda mrefu?
Je, yawezekana wazo hili haliwezi kuletwa, kutetewa wala kusimamiwa na viongozi wetu wa sasa - kwani hawana uwezo wa kulisimamia kama Nyerere alivyosimamia kujengwa kwa reli ya Uhuru (of course lazima nirushe dongo kidogo tu!)?
Je, yawezekana Chama cha Mapinduzi kimepoteza kabisa uwezo wake wa kuthubutu mambo makubwa na sasa kimeamua kufanya mambo madogo kama "mabarabara ya juu kwa juu"?
Je, tusubiri uongozi mpya ambao utakuwa tayari kuliunganisha taifa letu.

Jambo pekee ambalo tuna uhakika nalo kwa kuangalia China ni kuwa inawezekana kuunganisha kwa daraja umbali wa kilomita 42 (au hata zaidi) kwani Zanzibar iko kati ya Maili 16-31 sawa na kilomita 25-50 hivi (kutegemeana na eneo unalosimama kutoka bara). Hii ina maana tukiangalia mahali ambapo ni shortest distance. Hivyo swali la kama inawezekana kiteknolojia au vinginevyo limeshabiwa. Kwa upande wetu ni swali la kisiasa zaidi - je tuna viongozi ambao wanaweza kubuni, kusukuma na kusimamia mpango huu?

Tuna mengi ya kuyafanya mazuri na ya muhimu kuliko hili. Ama kwa kujifunza kwa wanayofanya wenzetu basi pia yapo zaidi ya hili tukianzia na msongamano wa jiji la Daresalaam. Tutafanya hili hapo tutakapokuwa tumeshasawazisha mengi yanayotukabili, na hao wenzetu wa China walifanya mengi ya muhimu zaidi na kufuatiwa na hili.
 
Ndugu yangu hizi ni kelele za mfa maji, taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa kuna mkakati wa nguvu (tena una ufadhili wa nchi moja ya Kiskandinavia) wa kuvunja muungano kwa ajili ya mafuta na inasemekana tukigawana maji ya bahari ndugu zetu watapata eneo kubwa la kina kirefu!


Usitafute mchawi kwa hili la Muungano. Njia rahisi ya kuendelea na Muungano(ili msikose mafuta na bahari) mbona ni rahisi tu. Kuweni wa haki katika huu Muungano huku mkijuwa kuwa rasilimali ziliopo hapa Tanzania si mafuta na bahari peke yake bali kuna madini, gesi na vyenginevyo, Hivi tuamuwe kwa umoja wetu kuwa ni vya pande zote kama mnavyotaka ieleweke kwa mafuta na bahari.
 
Hahahaha

Serikali imeshindwa kutengeza daraja la kigamboni iweze la kuunganisha na zanzibar ? Seriaki imeshindwa kuwapa umeme wa uhakika iweze daraja ? Serikali imeshindw akukupa sehemu ya kulala na elimu bure,afya ijenge daraja kwa misingi ipi ?

Hivi zanzibar na wazanzibari wenyewe tupo katika kujipapatua,ikiwezekana muungano tunauvunja,hatutaki hasa kuungani na nyinyi kwa sababu hamuna nia njema kama vile walivyokubwalina viongozi wetu karume na nyerere walipounganisha mataifa haya mawili tanganyika na zanzibar.

Kwa hiyo tumeshuhudia sasa hivi vingozi wenu wanaikandamamiza zanzibar kiuchumi,pia hata kuizalilisha zanzbar na watu wake,sisi wazanzbar tumeuchuikia muungano,nafikiri muandishi jenga hoja kujengwa rail za kisasa kuwanganisha mikoa yenu, pamoja na taraja la kigamboni.
 
Base ua uchumi na mendeleo ya uchina yaliazishwa na Serikali hasa kutumia Jeshi.

Hivi maengeer wetu wa JWTZ toka waanze ku assbly zile gai za nyumbu mpaka le zimetolewa ngapi

Sasa tujuiulize best brain za Tanzania ziko taasisi gani au sekta gani. ? Jibu Siasa

Sasa unakuta wale mangeneer na watu wenye Phd, dr wanotakiuwa uandika paper kutoa consultancy kwa serikali wao ndio mawaziri wabunge . teh teh teh
 
Stimulus package ya Tanzania ilikuwa around Tsh 1.7 trillions. Ukijumlisha na hivi vijicent vinavyopotea EPA, Kagoda, Meremeta, Rada, Vasco da Gamma travels, vitafunwa na ndugu na jamaa wote wanaohusika, Tanzania inaweza kabisa kugharamia Daraja kama hili. In fact umbali wa DAR-Zanzibar ni 40km. (2km less than huu umbali wa daraja china). But being a nation cursed with non-visionary leadership tutaendelea kusoma China leo, Cambodia kesho, Malayasia keshokutwa. Maybe we should try the other household- CDM that is!


Hiyo daraja ni ya nini mbona hakuna tabu ya usafiri kwenda sehemu mbili hizi. Nilidhani tunahitajia shirika la ndege na Reli kuliko hili daraja na kama kungekuwepo na uwezo basi tuunde shirika la ndege na tuwe na reli ya uhakika.
 
naona ndio uzuri wa kujijengea reputation ya u GT angeweka hu uzi hapa mwingine angeonekana anaongea pumba na mashambulizi kibao.

Umeweza kufahamu hilo kwa muda mfupi uliopo hapa au ulikuja upya baada ya hiyo mitikisiko unayosema? Ndugu yangu kunataka moyo kubaki humu unless ............!
 
Halitakuwa na umuhimu wowote,kama tuna $1bn,tuanzishe mgodi wetu wa dhahabu,au tutaifishe migodi ya north mara na nzega,daraja kwenda zanzibar la nini wakati mashua tunazo mvua!
Samahani kama nimewaudhi washabiki.
 
Tusifikiri kidogo, tusijifunge kwenye kufikiri vidogo; CCM imetufanya tufikiri kidogo, viongozi wetu hawafikiri tena makubwa! wanataka ya wastani! Well mataifa ya kisasa hayajengwi na watu wenye kufikiri kidogo au kwa wastani! Muungano ukivunjika mnaweka vituo vya mpaka na forodha katikati ya bahari kwenye hizo barabara! au hili linahitaji ugenius kulifikiria nalo? Au Muungano ukivunjika maana yake Zanzibar inazama baharini!?

Hebu tupe faida hasa ya kujengwa daraja hili au ndio kama ulivyosema Zanzibar iungwe na Bara ili iwe moja?
 
guys get serious.... why would you want to spend 2 Trillion eti ku-connect zanzibar? kuna economic activities gani zitakazorudisha hiyo investment!!!! kwanini hiyo hela isiunganishe mikoa ya magharibi kwa lami. Mwanakijiji achana na porojo
 
Umeweza kufahamu hilo kwa muda mfupi uliopo hapa au ulikuja upya baada ya hiyo mitikisiko unayosema? Ndugu yangu kunataka moyo kubaki humu unless ............!


hio status isikupotoshe mimi ni mwenyeji humu ndani bada ya mapumziko ya mda mrefu bada ya ban nimeona nianze upya na jina lilngine hivyo

members wengi na tabia za wana jf nazijua ndani nje. hawa hawa GT wangekuta nimeweka post kama hii hii ingekua hapatoshi hapa kwa short

statements na kejeli toka kwa members hapo ndo hua wananichosha kabisa dynamicism ya ubongo na ufikiri wao.
 
jamani waacheni hawa watu washughulikie sual umeme mkiwapeleka huko wataacha umeme na kutangaza mradi huu kumbukeni kuna ahadi nyingi bado hazijaguswa hii itakuwa sera ya 2015 kuweni wapole
 
Mzee Mwanakijiji, makadirio ya umbali kutoka Zanzibar hadi bara ni pungufu ya km au maili hizo. Inawezekana daraja likapufishwa kwa kuunganisha usafiri wa Bagamoyo na Zanzibar ambapo ni karibu zaidi kuliko Dar. Nakubaliana sana na wazo lako, ni wazo mwafaka, lakini nani kati ya viongozi wetu waliopo wako tayari kubana matumizi ili kuleta maendeleo hayo?
 
Back
Top Bottom