Tanganyika unayoiuliza iko wapi? aliiua Nyerere. Kuidai hivi sasa ina maanisha fikra za Nyerere zife na si zidumu tena.
Ni Watanzania wangapi leo hii wanaoweza kupinga fikra za Nyerere kwa makusudi kabisa?
Kuirudisha Tanganyika ni kuzidi kumpeleka mbali na utakatifu mwenyeheri Nyerere.
Muujiza wa kumfikisha Nyerere kuwa mtakatifu unakuwa rahisi sana nchi ikitoka kwenye serikali mbili ikawa moja. Itakuwa ni muujiza wa Nyerere umetimia, kuitawala nchi yenye zaidi ya asilimia 98 Waislaam na kuiingiza kwenye Serikali moja isiyo na dini.
Kumbuka, serikali ya Zanzibar ina dini na dini yake ni Uislaam na kadhi wanae.
Kufanya nchi iwe na Serikali tatu ni kuiuwa ndoto ya wanaompenda Nyerere awe mtakatifu. Linawezekana hilo?
Mimi natamani hata muungano usiwepo kama inawezekana, ikishindikana basi hizo tatu ndio pendeleo langu. Nakuhakikishieni na hilo ndilo pendeleo la Waislaam walio wengi.
Nani alikuambia utakatifu wa Nyerere unategemea muungano kwepo au kutokuwepo? Nyerere alimaliza shughuli yake akaondoka, ikiwa ni mtakatifu huwezi kubadili kitu kwa yanayoendelea sasa. Usijadili mambo ambayo huyajui, swala la utakatifu wa nyerere waachie wakatoliki, wao wanajua wanachoongea. Hata uikiandkika kitabu hutaelewa mpaka uwe mkatoliki. Jadili siasa na mambo unayojua hapa usionyeshe ushamba wako na udhaifu wako wakutojua mambo hapa. Kama unataka kujua wanamaanisha nini wakatoliki wanapomwita mtu ni mtakatifu, nenda kawaulize kwa hekima watakufahamisha.