Zanzibar hiyooo, Tanganyika kimyaaaa

Zanzibar hiyooo, Tanganyika kimyaaaa

Labda wewe tukurudishe Malawi.

Mimi ni Mtanganyika na si Mzanzibari na nnakuhakikishia hata hao Wazanzibari muungano ukifa leo hii huna uwezo wa kuwapeleka kokote. Ungeanza na wachina kwanza ambao huna muungano nao na wapo hapa wanauza mpaka karanga. Kinakushinda nini?

Jipe moyo tu. tanganyika ikija tunaweka travel restriction kwenda zenj. Ukienda tu kumtembelea babu yako tunakuweka kwenye terrorist watch list.
 
Kwani huu Muungano ni lazima??? Kwani hatuwezi kushirikiana kwanjia nyingine nilazima iwe Muungano??? Nilikuwa nasoma kilochotokea jana kwenye Hutuba ya Maalimu Seif inaonyesha kama Zanziber wamechoka na huu Muungano ila sisi tunawalazimisha waungane na sisi.

Inawezekana mimi sijuii ama ni mgeni sana katika siasa naomba kuuliza.
HIVI TANGANYIKA INAFAIDIKA NA NINI KWENYE HUU MUUNGANO???
 
Hivi watanganyika wote mnotetea muungano hebu toeni sababu za maana zinazowafanya kutetea huu muungano, obviously wazanzibari hawautaki na wala hawamung'unyi maneno katika hilo, sisi ndo tuonekana kuwalazimisha na wala faida tunayopata haijulikani. Tusijifunge na mawazo ya Nyerere, kwani sisi wenyewe hatuwezi kufikiria? Muungano huu ulikosewa tangu mwanzo, na wanzanzibari wameshonyesha kuwa hawautaki, tuuvunje tu, hauna faida zaidi ya kuleta misuguano isiyo na msingi.

Mfano sasa hivi kwenye katiba mpya tulitakiwa tuwe tunaongelea jinsi ya kuboresha mifumo ya TAKUKURU, mahakama, TRA, tume ya uchaguzi na vinginevyo vyenye jita katika maendeleo ya wananchi, lakini badala yake tunatumia pesa na muda mwingi kujadili muungano usio na faida.
 
Aisee wazej hatari. Mnaamia Tanganyika mpaka na babu zenu. Lakini bado serikali ya Tanganyika ikija wewe na babu yako Operation Kimbunga Itawapitia.

Isiwe hivyo Mkuu.Kila mtu ataruhusiwa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano
 
Mom nashauri koti livuluwe na watanganyika wapewe Zanzibar kwa miaka 50 ijayo
 
Zanzibar itabakia kua Zanzibar milele na wazanzibar watabaki kua wazanzibar hao wasaka tonge wanamwisho wao
 
KAMA tunataka kuzungumzia kero za muungano zilizopo na zinazoweza kujitokeza baadae nilazima turudi kwenye msingi kuwa TUUNDE SEREKALI YA MUUNGANO Ambayo haijapata kuwepo ILIYOPO NI SEREKALI YA TANGANYIKA ndugu iliyobadilishwa jina na kuitwa ya muungano tu.. sisi huku zanzibar tunaita SEREKALI YA BARA. huo ndio ukweli ambao watanganyika wengi hawaujui na ndio kero mama ya muungano huu. hata wale wanaotaka s2 ziendelee hawatoi jibu vipi tanganyika itavua koti la muungano ndani ya S2.
na kwa maoni yangu kama halikufanyika hili muungano unakwenda kuzimu na utakuwa historia mda si mrefu.
 
Tanganyika unayoiuliza iko wapi? aliiua Nyerere. Kuidai hivi sasa ina maanisha fikra za Nyerere zife na si zidumu tena.

Ni Watanzania wangapi leo hii wanaoweza kupinga fikra za Nyerere kwa makusudi kabisa?

Kuirudisha Tanganyika ni kuzidi kumpeleka mbali na utakatifu mwenyeheri Nyerere.

Muujiza wa kumfikisha Nyerere kuwa mtakatifu unakuwa rahisi sana nchi ikitoka kwenye serikali mbili ikawa moja. Itakuwa ni muujiza wa Nyerere umetimia, kuitawala nchi yenye zaidi ya asilimia 98 Waislaam na kuiingiza kwenye Serikali moja isiyo na dini.

Kumbuka, serikali ya Zanzibar ina dini na dini yake ni Uislaam na kadhi wanae.

Kufanya nchi iwe na Serikali tatu ni kuiuwa ndoto ya wanaompenda Nyerere awe mtakatifu. Linawezekana hilo?

Mimi natamani hata muungano usiwepo kama inawezekana, ikishindikana basi hizo tatu ndio pendeleo langu. Nakuhakikishieni na hilo ndilo pendeleo la Waislaam walio wengi.

Kumbe uko nyuma ya UKAWA kimyakimya!na unapingana na mwenyekiti!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
wanzanzibari wahuni sana wakiwa nje ya nchi huku wakitumia passport ya jamhuri ya muungano wa tanzania eti wanajitambulisha wao ni wanzanzibari.
kwenye passport wanayotumia imeandikwa wao ni wananchi wa jamhuri ya muungano wa tanzania
 
Zanzibar uhuru umepatikana kwa risasi Tanganyika uhuru umepatikana kwa mate, nchi mbili hizi haziwezi kuungana CCM wanajihangaisha bure,Karume kafa hao mgeni na Nyerere kisa mungano
 
Zanzibar itabakia kua Zanzibar milele na wazanzibar watabaki kua wazanzibar hao wasaka tonge wanamwisho wao

Ni aibu kubwa kwa sababu Wazenj wanaishi kwa udanganyifu bila haya. Wao ni Watanzania na pia ni Wazanzibari, Bara kuna Watanzania tu. Maana yangu ni kuwa Zanzibar ndiyo wenye Serikali mbili, yao na ya Jamhuri, wakipewa uongozi katika Serikali ya Muungano wanajiita WaTz na hata mambo yasiyo ya muungano wanayafyatukia. Vuai Ali Vuai alliteuliwa na Mwinyi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Bara kwa madai kuwa yeye ni Mtanzania. Hussen Mwinyi sasa hivi ni Waziri katika Wizara ya Afya, siyo ya Muungano, kisa ni MTz, aibu kubwa hii. Muungwana haendi kasoro za namna hiyo kwa kukutana na rafiki yake Kikwete, ni Wizara ya watu milioni 40 wa Bara hiyo, siyo ya Kikwete. Lakini wenzetu Wazenj HAYA YA USO HAWANA.

Bara wote ni Watanzania tu kwa hiyo wao wana serikali moja tu. Poleni Wazanzibari kwa kuwa Wahuni taifa lote hadi mkaishi kwa uongo kila wakati. Halafu mkikutana na mijadala yenye hoja za kutaka kuwanyang'anya tonge lenu la wizi mnageukia matusi ili kupoteza malengo.
 
Kagera wahamie Rwanda, kigoma wahamie Burundi au Kongo Rukwa wahamie Zambia Mbeya wahamie Malawi,Mtwara wahamie Msumbiji,mwanza wahamie Uganda,Mara, Kilimanjaro,Arusha wahamie Kenya ! Baadae huke mbeleni ile mikoa iliyopakana na hao ihamie huko walipo ! Huu muujiza ukiikumba Tanganyika na ukafanikiwa kuna Hatari Ramani za Dunia zikavurugika

Sahihisho: Mtwara,Lindi na Ruvuma itaunda nchi moja itakayoitwa REPUBLIQUE DE MAKONDE...kwa makaa ya mawe, madini ya uranium, korosho,uvuvi,kilimo cha mpunga&mahindi pamoja na gesi hakika itakuwa zaidi ya BARMUDA natamani hili litokee hili hata leo.
 
Iko wazi kabisa kuwa ili kuulinda mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar imekuwa ikijichomoza kila uchao kama nchi kamili. Kutokana na vuguvugu la mara kwa mara kutoka kwa Wazanzibari,CCM na Serikali yake imekuwa ikiharakisha kuwapa wanachopinga ili kuulinda mfumo wa Muungano uliopo. Ni kama Wazanzibari hubembelezwa na kupendelewa.

Iko wazi kuwa, Zanzibar ina wananchi wathubutu.Wananchi wanaoweza kusema kile wanachokiamini.Wananchi ambao wanaweza kumkosoa yeyote iwe kule kule Zanzibar au katika ngazi ya Muungano. Ipo mifano mingi ya akina Mzee Moyo,Shamhuna,Maalim Seif,Jussa na wengineo. Hawa hawapepesi macho wanapotaka kusema ukweli wanaouamini kuwa hivyo.

Ndiyo maana sasa Zanzibar wana bendera yao,wana wimbo wao wa Taifa,wana vitambulisho vyao vya ukaazi,wana mizinga yao ya sherehe mbalimbali za kitaifa,wana majeshi yao kama JKU na KMKM,wana Katiba yao inayowatambulisha kama nchi kamili na kadhalika na kadhalika. Nasema,wenzetu wa Zanzibar,pamoja na kuwa na Serikali yao tangu siku ya kuanza Muungano, wanaendeleza mapambano yao ya kutaka 'uhuru kamili' wa Zanzibar yao.

Sasa Zanzibar imebaki na dukuduku kubwa moja: ushirikiano wa kimataifa. Zanzibar inataka kuwa huru kujumuika kimataifa,kuingia katika mikataba ya kimataifa kama Zanzibar na kukopa kama Zanzibar,kwa kutaja machache. Kwa hali ilivyo hivi sasa na kung'ang'aniwa kwa mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar haiko mbali kupata nguv kamili kama Taifa linalojitegemea. Ushirikiano wa kimataifa tu ndiyo ndoto iliyobaki kwa Zanzibar.

Tanganyika yetu iko wapi na itarudi vipi?

Kwa maneno yako Zanzibar ilishaukataa Muungano tangu Mwinyi aliupomwondoa Salmin Amour uMakamu wa Rais wa Jamhuri na kumwondoa kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri la Jamhuri. Hapo ndipo walipokwenda kuunda Katiba, Bendera yao na Wimbo wao wa Taifa. Kikwete anajifanya haelewi haya kwa sababu anatamani kipindi kingine Ikulu kwa kupanga vurugu za makusudi ikiwemo yeye Rais kupingana na Tume aliyoiunda mwenyewe na kutangaza msimamo wake Bungeni kuwa yeye anataka Serikali 2. Mbaya zaidi ni pale aliporuhusu vitisho vya jeshi kupindua nchi, mtu aliyetoa vitisho hivyo alistahili kuhukumiwa na kuwekwa jela.

Bahati mbaya sana siasa ya nchi imeingia mikononi mwa wanajeshi kinyemela, Kikwete ni Kanali, Kinana ni Kanali, Nape mtoto Brigadia, akina Komba ndiyo haooo tena. Leo wanatuambia Watz tukiamua Serikali 3 Jesi litapindua nchi. Lukuvi na Tyson wamepata wapi kauli hizi kama siyo kwa Kikwete mwenyewe akiwa Kanali anayepanga mapinduzi kwa kuyatangaza mwenyewe hata kabla hayajatokea?

Mimi sijawasikia makamanda wa majeshi ya ulinzi na usalama wakiingia katika siasa na kutaka Serikali 2. Lukuvi na Tyson waliwasikia wapi?

Tamaa hushinda kudra!!!! Kikwete angeacha kuwafanya WaTz watoto wadogo, atangaze kabisa kuwa Ikulu imemkolea hataki kuondoka. Yalisemwa haya wakati wa uchaguzi!
 
Back
Top Bottom