Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Iko wazi kabisa kuwa ili kuulinda mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar imekuwa ikijichomoza kila uchao kama nchi kamili. Kutokana na vuguvugu la mara kwa mara kutoka kwa Wazanzibari,CCM na Serikali yake imekuwa ikiharakisha kuwapa wanachopinga ili kuulinda mfumo wa Muungano uliopo. Ni kama Wazanzibari hubembelezwa na kupendelewa.
Iko wazi kuwa, Zanzibar ina wananchi wathubutu.Wananchi wanaoweza kusema kile wanachokiamini.Wananchi ambao wanaweza kumkosoa yeyote iwe kule kule Zanzibar au katika ngazi ya Muungano. Ipo mifano mingi ya akina Mzee Moyo,Shamhuna,Maalim Seif,Jussa na wengineo. Hawa hawapepesi macho wanapotaka kusema ukweli wanaouamini kuwa hivyo.
Ndiyo maana sasa Zanzibar wana bendera yao,wana wimbo wao wa Taifa,wana vitambulisho vyao vya ukaazi,wana mizinga yao ya sherehe mbalimbali za kitaifa,wana majeshi yao kama JKU na KMKM,wana Katiba yao inayowatambulisha kama nchi kamili na kadhalika na kadhalika. Nasema,wenzetu wa Zanzibar,pamoja na kuwa na Serikali yao tangu siku ya kuanza Muungano, wanaendeleza mapambano yao ya kutaka 'uhuru kamili' wa Zanzibar yao.
Sasa Zanzibar imebaki na dukuduku kubwa moja: ushirikiano wa kimataifa. Zanzibar inataka kuwa huru kujumuika kimataifa,kuingia katika mikataba ya kimataifa kama Zanzibar na kukopa kama Zanzibar,kwa kutaja machache. Kwa hali ilivyo hivi sasa na kung'ang'aniwa kwa mfumo huu wa Muungano wa Serikali mbili,Zanzibar haiko mbali kupata nguv kamili kama Taifa linalojitegemea. Ushirikiano wa kimataifa tu ndiyo ndoto iliyobaki kwa Zanzibar.
Tanganyika yetu iko wapi na itarudi vipi?