Waandishi wengi kwenye mada hii hawana hisia kabisa ya jambo linaloendelea Zanzibar. Inasikitisha kuona watu wazima wanaandika kama watoto wa nasari skool. Hebu tupeni hoja. Jambo lolote lina sababu. Hawa vijana hawakuamka asubuhi wakaamu kufanya walivofanya. Kuna pande mbili husika nani alifanya nini ikasababisha hayo yaliotokea. Badala kuwalaumu wazanzibari in GENERAL, kwanini haingaliwi usawa wa jambo. Kama tuliungana nchi mbili, heshima iwepo na kama ni koloni la tanganyika, pia ukweli uelezwe mchana sio kujificha jificha. Wazanzibari wanadai haki yao ya kujitawala kwenye Taifa lao. Kuna makosa mtu kudai chake?.