Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,316
- 33,812
Hapana ndugu yangu hakuna anaye wng'ang'ania.Mkuu ndo maana nikasema nyinyi hamuwezi kufanya maamuzi magumu bado munataka kutunyonya kama nchi ndogo na pato lake dogo haiwezi kuchangia katika serekali ya muungano kwanini bado munanganga nayo si iwacheni halafu how many times wazanzibar washaonyesha hisia za wazi kwamba muungano hatuutaki mfano ni jumbe huyo huyo ulomtaja ndo aloingia matatizoni kwasababu ya kuhoji muunga wangapi wengine wameingia matatizoni kwa kuhoji muungano HADI SASA MUUNGANO KUUHOJI NI DHAMBI NA SHERIA HAIRUHUSU KUZUNGUMZIA KUUVUNJA na ndo maana unakuta tunatumia ujanja kama kuuvunja ni kesi basi leteni muungano wa wa mkataba unakuta wengine wanajitoa fahamu hawajui eti nini muungano wa mkataba halafu sisi wazenji tumeuzunguza wazi kabisa kama muungano hatuutaki na baraza la wakilishi wameongea kwamba hauna faida na sisi.
HATA KAMA KUNA BAADHI YA WAZANZIBAR WANATAKA MUUNGANO LAKINI MUUNGANO GANI si huu wa kudharauliana kwamba kijinchi kadogo sijui uchimvi gani sasa kama mulijua nchi ndogo ilikuaje mukaungana nao nyinyi mababu hapo ndo utaona kwamba mulikua hamna dhamira njema na hilo tuliliona mapema tulipomaliza kuungana tuu mwaka mmoja tuu mukaanza kubadilisha na kuongeza vitu kwenye mkataba wa muungano na mwisho wake mzee karume alivyoshtuka mukaona ahh ataharibu kila kitu ndo MR X akamaliza kila kitu.
SWALI lini nyinyi watanganyika (jina hamlitaki munataka tanzania bara) mulokaa bungeni mukaongea kwamba muungano hauna faida kwenu tuachane nao hamuwezi na wala hamutaweza sisi ndo tutakaouvunja muungano kwasababu kuna jambazi moja linajifanya kubwa na janja.
TUACHIWE TUPUMUE MIAKA 50 INATOSHA YA UNYONYAJI
Tume ya Warioba mumetaka usawa wa wajumbe.
Badala ya kudai kura ya maoni ninyi mkaamua kuwachagua akina Ally Saleh wa BBC. Sasa hivi kimyaa
Ninyi mnadai muungano wa mkataba. Sasa kama hamtaki muungano mnataka mkataba wa nini wakati mnatakiwa mkaijenge znz ya kabla ya mwaka 1963.
Bunge la katiba mumedai wajumbe zaidi. Khaa! sasa kama hamtaki muungano mnataka wajumbe waje kufanya nini?
Mlipeleka wajumbe wa tume kwa Warioba wakafanye nini. Mnataka mkataba wa nini.
Ndugu yangu, hebu onyesha wapi Tanganyika ina mnyonya mzanzibar!
Sheni kauliza hivi katika 4.5 mnazopata za pato la taifa ninyi mnachangia kiasia gani?
Mwenyekiti wa kamati ya fedha anasema mapato yenu ni bilioni 240 kwa mwaka. Kwa bajeti ya ulinzi na uslama ambayo ni zaidi ya bilioni 1,300 ina maana kuwa znz bila kuondoa hata senti tano katika 240 haiwezi kuenedha wizara hizo kwa miezi 3.
Hapo nina maana bila kuondoa hata senti tano ya mshahara wa Sheha au ndege za kubeba mikaa kutoka Pemba.
Bajeti ya znz ya mwaka 2013 mapato ya ZBR ni bilioni 100. Hebu onyesha wapi unanyonywa tena naomba uzungumzie TRA
Hebu tueleze wapi mnanyonywa hasa.