Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Nadhani hujui unachokiongea na kama umeelimika basi wewe ni mvivu wakufikiri. Tunaoijua unguja basi tunasema katika mambo ya msingi Mzee karume aliyofanya basi nikukubali muungano na Tanganyika, alijua anachokifanya hata kama muungano huu ulikuwa na maslahi ya Marekani lakini naye aliona una maslahi makubwa kwa hatima ya znz wakati huo; walaah! nikuambie tu mara baada ya mapinduzi ya znz kitu kikubwa kingefuata ni migogoro na hata kuchinjana kati ya wapemba na unguja na ingekuwa kama somalia tu. Nadhani maisha yangekuwa yanarudiwa basi tungerejea nyuma baada ya mapinduzi halafu muungano na Bara ungefanyika miaka ya 80 leo hii naamini tungempiga mawe mtu yeyote anayebeza muungano. Pia tuelewe kuwa Dunia inazidi kubadilika hali ya hewa, hivi ikitokea natural calamities kama inavyotokea kwenye nchi za wenzetu hasa VISIWA, tutafanya nini, visiwa vyetu ni vidogo sana ikitokea thoruba ya siku tatu tu inatosha kuosha kila kilichopo kisiwani. SO TUSIFIKIRIE WAZUNGU WANAPOSEMA TANZANIA IMEJALIWA NA KUPENDELEWA NA MUNGU UKAFIKIRI NI WAJINGA, TENA HAWAMAANISHI VISIWANI ILA NI BARA KWANI LICHA YA NATURAL RESOURCES ILIZONAZO TU BALI PIA GEOGRAPGICALY IT IS SECURED. Nahitimisha kwakusema hivi-: kiukweli kati ya Tanganyika na Zanzibar anayemuhitaji na atakayemuhitaji mwenzake hata isingekuwa muungano ni Zanzibar na kama maisha yanajaribiwa basi hebu tujaribu kuvunja muungano.
Kwani ni nani aliefanya na kupanga Mapinduzi ? Yale ya kuipindua Serikali halali ya Zanzibar na hata yale ya kumpindua Karume ni nani Liepanga Mapinduzi hayo ???
Mgogoro mbona haukutokea ? Na hata kama ungetokea ni haki yake kutokea kwani wakati huo mambo ya kupinduaa serikali yalikuwa ni fashion katika nchi chingi za Kiafrika .
Hivi ni nani aliesema Muungano mwisho Chumbe ? Huyu alikuwa na maana gani ?Nyerere alikuwa msomi Karume alikuwa ni mtu aliekuwa hana elimu ,sasa kama nikikwambia Nyerere alimlaghai Karume nitakuwa nakosea ?
Habari ya Dhoruba isikupe tabu sana kwani asilimia 99 ni waislamu ,hivyo hatima yao inategemea Mwenyezi Mungu haina wala haihitaji ni wapi wewe upo kijiografia au kisaikolojia ,ukame unauelewa,maradhi unayajua ,kimbunga unakifahamu na mvua umewahi kuiona yote hayo hata uwe juu ya mlima basi yanaweza kabisa kukumaliza uhai na kuharibu uso wako wa arhi,natumai umewahi kusikia tetemeko la ardhi nalo ni baa kubwa lisilo na sumile.
Sasa tatizo ni kitu gani ,kuhitajiana ? Hapo sioni ubaya ,kwani tukiwa nje ya Muungano kutaondoka huko kuhitajiana ?
Na kama kutaondoka basi nyie mtakuwa mna roho mbaya sana na nia zenu sio nzuri , Umeona Philipines ,mbona wamesaidiwa sana tu na wao kimbunga kimewaweka katika hali mbaya.
WaZanzibari hawapo katika kujaribu kuuvunja Muungano .wapo katika nia ya kuukataa Muungano na nia na madhumuni ni kuuondoa usiwepo na kama ukiwepo basi wa makubaliano sio wa kiulaghai.