Zanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara’

Zanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara’

Nadhani unaona ushahidi mwenyewe, hivi jamii inapoamini kuwa waziri wa mambo ya nje anatoa VISA hapo kuna kitu gani kwa lugha nyepesi.
Jamii inapoamini kuna ghost minister wa mambo ya nje wa SMZ hapo kuna nini kwa lugha yenu.

Nitajie kongamano, warsha, jumuiko, kiongozi au mzanzibar yoyote ambaye katika mjadala wa muungano ameshaweka namba na kuzijadili.

Nionyeshe wapi Maalim, Jusa, Manosur, Ahmed Rajab, Himid n.k. wamewahi kutamaka namba za kuendesha muungano uwe wa mkataba, uswiss, ujerumani na china n.k niambie wapi. Never
Wao ni kupanga nafasi za vyeo na ajira tu, utamaduni wa starehe na kubebwa tu

gombesugu hivi mtu anapochangia 0 na kutaka apewe 50 mtu huyo anajua hesabu kweli?
Watu wanalala hawajui bili ya umeme
Wanalipiwa mishaharaa
wanasomeshewa watoto
Wanapewa ulinzi wasiojua gharama zake
Halafu wanapewa 4.5 ambayo ni kubwa kuliko walichovuna kwa miezi 12(240) buree!
Wanapewa nafasi kwasababu ya uzanzibar na si academic qualification

Bado wanasema wanataka zaidi hata kile wasichochangia. Bilioni 240 ndizo zipo mbele yetu
Mwambie
Barubaru taarifa ya JFC ipo hapo tunamsubiri afungue kinywa, keshakimbia kwasababu kuna namba

Ninafurahi sana mnaponishambulia mimi binafsi na si hoja zangu kwasababu mnajua ni ukweli.
Nitapiga mfupa mimi sina haya na kupe.

Narudia bila kumung'anya maneno ukitaka kuongea na mzanzibar ongea hadithi, ngano, mahoka na uzushi. Ukitaka aondoke katika jamvi mtupie namba 1-10. Na urafiki unaweza kwisha.

Tuacheni tupumue jamani, zigo la karafuu miaka mingi migongo imepinda. Tuacheni chonde chonde

Nguruvi3.

Ahali yangu kila wakti nakwambia acha kukurupuka na chuki zako hizo . Je umeshindwa kuisoma hiyo iliyowekwa ni RIPOTI YA STADI YA VYANZO VYA MAPATO YA MUUNGANO. Sasa nilichokwambia utafute ni RIPOTI YA MAPATO YA MUUNGANO ambayo inatoka kila mwaka. Hiyo itakuongoza.

Lakin sikuweza kukuacha hivi hivi hata hiyo nimeiweka hadhwarani uone namna waZnz wachache (chini ya 1.4 mil) wana makusanyo makubwa kuliko wa Tz (zaidi ya 45 mil). Pitia jedwali la 2 uone hayo.
 
Joka kuu.

Ahsante sana kwa Uliyotuwekea LAKIN ULICHOWEKA SIO RIPOTI YA MAPATO YA MUUNGANO NA ZNZ. Bali umetuwekea RIPOTI YA STADI YA VYANZO VYA MAPATO YA MUUNGANO.

Ulichokiweka kinaonyesha mapato ya muungano tu hivyo itakuwa taabu sana kujuwa mapato ya Znz ambayo akina Nguruvi3 wanasema ni Bil 240.

Lakin kwa kusaidia kidogo hebu pitia jedwali la 2 ambalo linaonyesha makusanyo ya ushuru wa forodha. hapo utaona Znz wanakusanya zaidi kutokana na idadi yake ya watu ukilinganisha na Tanganyika ambayo ina idadi kubwa ya watu.

lakin cha kujifunza hapo katika stadi hii ni mapendekezo ambayo yameweka bayana haya:

Stadi hii imetoa mapendekezo mbalimbali ya kuboresha Vyanzo vya Mapato ya Muungano vilivyopo, na kupanua wigo wa kodi kwa lengo la
kuongeza Mapato ya Muungano. Mapendekezo hayo ni pamoja na yafuatayo:-
i)
Kuweka utaratibu utakaowesha kutenganisha mapato ya Muungano na yasiyo ya Muungano, kwa Asasi ambazo hazina utaratibu huo.
ii)
Kukuza mapato ya ndani ya Kodi na yasiyo ya Kodi kwa lengo la kuongeza mapato ya Muungano, ili kukabiliana na tishio la upungufu wa mapato yatokanayo na Ushuru wa Forodha kutokana
na Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya za ushirikiano wa Kikanda.
iii)
Sera na Sheria zinazotoa vivutio vya uwekezaji kwa kutoa misamaha ya kodi kupitiwa upya kwa lengo la kuziba mianya ya upotevu wa mapato.

..ndugu yangu kuna majedwali ktk hiyo ripoti yanaonyesha kinachokusanywa Znz na kinachokusanywa Tanganyika.

..any way, mimi na wewe tumetoka mbali. nakuelewa unachotaka kusema. tuachane tu na huu mjadala kwasababu naona hausongi mbele.

cc gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,

..OK, nimekuelewa kuhusu msimamo wako kwambo MOU ni sehemu ya mjadala huu.

..sasa nina maswali yafuatayo:

1. je Znz ina uwezo wa kuchangia masuala ya muungano sawa na Tanganyika?

2.je Znz ina uwezo wa kuchangia MOU na masuala ya muungano sawa na Tanganyika?

..mwisho, kwa msaada niwasilisha ripoti ya Joint Finance Committee ambayo Barubaru aliomba tuiwasilishe.

http://jfc.go.tz/downloads/mapato.pdf

cc Nguruvi3

Ndugu yangu Joka kuu.

Hebu soma mwenyewe ulicho attach . Je ni RIPOTI YA MAPATO YA MUUNGANO HAYO?

Usikurupuke na hiyo stadi ya vyanzo vya mapato ya muungano.

Pole sana.
 
..ndugu yangu kuna majedwali ktk hiyo ripoti yanaonyesha kinachokusanywa Znz na kinachokusanywa Tanganyika.

..any way, mimi na wewe tumetoka mbali. nakuelewa unachotaka kusema. tuachane tu na huu mjadala kwasababu naona hausongi mbele.

cc gombesugu, Nguruvi3

Kwa kukusaidi kidogo unatakiwa kujua Idadi ya watu wa nchi mbili husika kabla kujua wanakusanya nini. Kwani mnapokuwa wengi na matumizi yenu yatakuwa makubwa ukilinganisha na wachache.

RIli uelewe zaidi lazima ujue makusanya na idadi yake ya watu kupata uwiano. ndio maana mimi nakwambia Znz wanakusanya sana kuliko Tanganyika. Pitia jedwali namba 2 lenye kuonyesha makusanyo ya ushuru wa forodha utaliona hilo.

Kumbuka uchumi ni taaluma inayomtaka mja kwenda skuli na sio porojo

Ndugu yangu Joka kuu.

Hebu soma mwenyewe ulicho attach . Je ni RIPOTI YA MAPATO YA MUUNGANO HAYO?

Usikurupuke na hiyo stadi ya vyanzo vya mapato ya muungano.

Pole sana.

Barubaru,

..usiishie kwenye kichwa cha habari cha ripoti.

..ndani ya hiyo ripoti kuna jedwali linaloonyesha makusanyo ya kodi ya mapato, na makusanyo ya ushuru wa forodha, toka Zanzibar na Tanganyika.

..mimi nadhani ripoti hiyo siyo ya kupuuzwa moja kwa moja kama unavyotaka kufanya.

cc gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kwa kukusaidi kidogo unatakiwa kujua Idadi ya watu wa nchi mbili husika kabla kujua wanakusanya nini. Kwani mnapokuwa wengi na matumizi yenu yatakuwa makubwa ukilinganisha na wachache.

RIli uelewe zaidi lazima ujue makusanya na idadi yake ya watu kupata uwiano. ndio maana mimi nakwambia Znz wanakusanya sana kuliko Tanganyika. Pitia jedwali namba 2 lenye kuonyesha makusanyo ya ushuru wa forodha utaliona hilo.

Kumbuka uchumi ni taaluma inayomtaka mja kwenda skuli na sio porojo

..nakuelewa.

..lakini hapa hatuzungumzii uwiano, tunazungumzia jumla ya mnachokusanya huko Zanzibar, na kama mnaweza kuchangia 50% ya gharama za kuendesha muungano.

..ndiyo maana mimi naendelea kusisitiza kwamba muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika hauwezekani kutokana na tofauti za kieneo na idadi ya watu baina ya mataifa haya mawili.
 
Barubaru,

..usiishie kwenye kichwa cha habari cha ripoti.

..ndani ya hiyo ripoti kuna jedwali linaloonyesha makusanyo ya kodi ya mapato, na makusanyo ya ushuru wa forodha, toka Zanzibar na Tanganyika.

..mimi nadhani ripoti hiyo siyo ya kupuuzwa moja kwa moja kama unavyotaka kufanya.

cc gombesugu, Nguruvi3

JokaKuu.

naona sassa una macho huoni, una masikio usikii , sasa unapua Nusa sasa.

Punguza jazba nisome vizuuuri sana utanielewa kwani pasi na shaka umeghumiwa wewe kiasi ujui ulifanyalo.

Binafsi nimekubainishi kuwa hiyo sio RIPOTI YA MAPATO NA MATUMIZI YA MUUUNGANO ya JFC. bali hiyo ni RIPOTI YA STUDI YA VYANZO VYA MAPATO YA MUUNGANO.
Hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa.

Lakin sikuibaza nimeichambua kukwambia soma jedwali namba 2 nimeliwekea bayana yake na mwisho nikabainisha hata mapendekezo ya stadi hiyo kuhusu vyanzo vya mapato.

sasa ukitaka uhondo pitia RIPOTI ya kila mwaka ya JFC inayozungumzia MAPATO na MATUMIZI ya muungano kwa kila nchi.

Pitia afisi za JFC zipo Dar Posta jengo la Sukari house.

Pole sana au ndio ulitaka kutufunga kamba kwa kuita hiyo ndio ripoti? Umenoa

..nakuelewa.

..lakini hapa hatuzungumzii uwiano, tunazungumzia jumla ya mnachokusanya huko Zanzibar, na kama mnaweza kuchangia 50% ya gharama za kuendesha muungano.

..ndiyo maana mimi naendelea kusisitiza kwamba muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika hauwezekani kutokana na tofauti za kieneo na idadi ya watu baina ya mataifa haya mawili.

JokaKuu.

labda nikuulize JE na misaada mnayopewa au mikopo mnagawana sawa kwa sawa? au wewe unataka muungano muchangie sawa kwa sawa lakin mikopo naisaada Znz wapewe 4.6%.

Je inawezekana watu wawaili wakaungana na watu ishirini kisha wakachangia muungano pasu kwa pasu especially katika uchumi?

Kinachoweza kuchangia pasu kwa pasu ni maamuzi lakin sio uchumi na hicho ndicho kilichopo baina ya muungano wa nchi mbili hizo huru.

Kwa wachumi idadi ya watu ni muhimu sana katika kupanga matumizi na kujua income per C . Kwani hakuna mapato yasiyo na matumizi.

Pole sana kwa kukosa ilmu ya uchumi.
 
either tuungane kuwa nchi moja au tuachane, vingine vyote porojo tu.
 
Barubaru,

..kwa kifupi ni kwamba labda, labda, mnaweza kujigharimia wenyewe.

..lakini hamuwezi kuwa pamoja na sisi milioni 40++ halafu tukagawana gharama za matumizi 50/50.

..Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha ya baraza la wawakilishi amekiri hivyo.

..hata takwimu toka TRA kama zilivyonukuliwa ktk ripoti ya JFC zinabainisha suala hilo.

..ningekuwa nataka kumfunga mtu kamba nisingeleta taarifa ambazo zina ushahidi wa kitakwimu.

..hizo takwimu ni facts. tunaweza kuwa na different interpretations, lakini hatuwezi kubadilisha hizo facts.

cc gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu.

labda nikuulize JE na misaada mnayopewa au mikopo mnagawana sawa kwa sawa? au wewe unataka muungano muchangie sawa kwa sawa lakin mikopo naisaada Znz wapewe 4.6%.

Je inawezekana watu wawaili wakaungana na watu ishirini kisha wakachangia muungano pasu kwa pasu especially katika uchumi?

Kinachoweza kuchangia pasu kwa pasu ni maamuzi lakin sio uchumi na hicho ndicho kilichopo baina ya muungano wa nchi mbili hizo huru.

Kwa wachumi idadi ya watu ni muhimu sana katika kupanga matumizi na kujua income per C . Kwani hakuna mapato yasiyo na matumizi.

Pole sana kwa kukosa ilmu ya uchumi.

..nakubaliana na hoja yako kwamba idadi ya watu ni muhimu.

..kama ni hivyo mbona mnataka mpewe 10% ya misaada toka nje?

..mbona mnataka mpewe 20% ya ajira ktk serikali ya muungano?
 
..nakubaliana na hoja yako kwamba idadi ya watu ni muhimu.

..kama ni hivyo mbona mnataka mpewe 10% ya misaada toka nje?

..mbona mnataka mpewe 20% ya ajira ktk serikali ya muungano?

JokaKuu.

Unajua kwetu wachumi. jedwali hilo namba 2 linaweza ibua mengi sana. Machache yakiwa hayo ulobainisha. lakin usikurupuke. Je unaweza sema hayo ya 20% na 10% umeyatoa wapi? mbona kwenye stadi uliyoweka hayapo?

Angalizo kwako: Kumbuka kuna mambo ya kiuchumi na mambo ya kiutawala. sasa naomba sana utenganishe hivi vitu viwili katika mvungano wenu

Au ndo vijineno vya kwenye vilabu vya ulevi?

Kumbuka kiuchumi kila kitu kinajengwa na facts ambazo mara nyingi ni DATA.

Kumbuka uchumi ni taaluma inayomtaka mtu aende skuli na sio BLA BLA.

Pole sana

..tuanzie basi na data za idadi ya wa-Tgk vs wa-Znz.

..je kwa kuzingatia idadi unafikiri Znz inastahili asilimia ngapi ya misaada toka nje?

..kwa kuzingatia idadi unafikiri Znz inastahili asilimia ngapi ya ajira ktk serikali ya muungano?
 
Hiyo kazi mbona imeshafanywa na wataalamu wa nchi hizo mbili wa uchumi a kila mwaka wanatoa taarifa.

narudi pale pale waulize JFC watakupambanulia yote hayo.

usiwe mvivu mkuu au unataka nikutafunie kabisa?

..siyo uvivu tu, utaalamu wa uchumi nao sina.

..ndiyo maana nimekuuliza maswali haya wewe duktuuri wetu wa uchumi.

..kwa kuzingatia idadi ya watu wa Znz vs Tanganyika, unafikiri Znz inastahili asilimia ngapi ya misaada toka nje, na nafasi za ajira ktk serikali ya muungano??

cc gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Yaani hizo kashfa,stereotypes na prejudices ndo ulizofundishwa!?

Hivi ni kweli kwa yakini unayaamini hayo uloandika hapo;yakuwa Wazanzibar hawajui asilan hisabati/takwimu!? Duh!!

Pole yako!

Mufti Barubaru naUlamaa Boko Haram...tafadhali wala nyie msichambue lolote/chochote,maana sie "hatujasoma" pia ati ni "wavivu" wa kusoma..."hatujui! kusoma wala kuandika!? Ndo yaleyale!

Al Akhiy,hawa jamaa zetu hamuwawezi kwa malumbano yaso tija,shughulikeni nao tu pale mjisikiapo mna fursa/wasaa wa kuchezea...khasa huyu Nguruvi3!

Ahsantani.

gombesugu

Al akhy walahi nakusoma taratibu "jazakum laah khair" Inshaalah
 
Nguruvi3.

Ahali yangu kila wakti nakwambia acha kukurupuka na chuki zako hizo . Je umeshindwa kuisoma hiyo iliyowekwa ni RIPOTI YA STADI YA VYANZO VYA MAPATO YA MUUNGANO. Sasa nilichokwambia utafute ni RIPOTI YA MAPATO YA MUUNGANO ambayo inatoka kila mwaka. Hiyo itakuongoza.

Lakin sikuweza kukuacha hivi hivi hata hiyo nimeiweka hadhwarani uone namna waZnz wachache (chini ya 1.4 mil) wana makusanyo makubwa kuliko wa Tz (zaidi ya 45 mil). Pitia jedwali la 2 uone hayo.
Wewe uliyo nayo kwanini huweki?
 
..siyo uvivu tu, utaalamu wa uchumi nao sina.

..ndiyo maana nimekuuliza maswali haya wewe duktuuri wetu wa uchumi.

..kwa kuzingatia idadi ya watu wa Znz vs Tanganyika, unafikiri Znz inastahili asilimia ngapi ya misaada toka nje, na nafasi za ajira ktk serikali ya muungano??

cc gombesugu, Nguruvi3
Na kwa kuzingatia mchango wake kwa taifa pia.
 
Back
Top Bottom