Nadhani hujui unachokiongea na kama umeelimika basi wewe ni mvivu wakufikiri. Tunaoijua unguja basi tunasema katika mambo ya msingi Mzee karume aliyofanya basi nikukubali muungano na Tanganyika, alijua anachokifanya hata kama muungano huu ulikuwa na maslahi ya Marekani lakini naye aliona una maslahi makubwa kwa hatima ya znz wakati huo; walaah! nikuambie tu mara baada ya mapinduzi ya znz kitu kikubwa kingefuata ni migogoro na hata kuchinjana kati ya wapemba na unguja na ingekuwa kama somalia tu. Nadhani maisha yangekuwa yanarudiwa basi tungerejea nyuma baada ya mapinduzi halafu muungano na Bara ungefanyika miaka ya 80 leo hii naamini tungempiga mawe mtu yeyote anayebeza muungano. Pia tuelewe kuwa Dunia inazidi kubadilika hali ya hewa, hivi ikitokea natural calamities kama inavyotokea kwenye nchi za wenzetu hasa VISIWA, tutafanya nini, visiwa vyetu ni vidogo sana ikitokea thoruba ya siku tatu tu inatosha kuosha kila kilichopo kisiwani. SO TUSIFIKIRIE WAZUNGU WANAPOSEMA TANZANIA IMEJALIWA NA KUPENDELEWA NA MUNGU UKAFIKIRI NI WAJINGA, TENA HAWAMAANISHI VISIWANI ILA NI BARA KWANI LICHA YA NATURAL RESOURCES ILIZONAZO TU BALI PIA GEOGRAPGICALY IT IS SECURED. Nahitimisha kwakusema hivi-: kiukweli kati ya Tanganyika na Zanzibar anayemuhitaji na atakayemuhitaji mwenzake hata isingekuwa muungano ni Zanzibar na kama maisha yanajaribiwa basi hebu tujaribu kuvunja muungano.
Ukweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.
Kitu cha ajabu sana ni hao hao wanataka tume iwe asilimia 50, wanataka bunge la katiba liwe asilimia 50. Wanataka viongozi wa muungano na wafanyakazi wa serikali ya muungano wawe nusu kwa nusu.
Tumewahi kuwaeleza mara nyingi sana wazanzibar akiwemo Jusa na Ahmed Rajab kuwa Tanganyika haihitaji znz kwa lolote. Hatuhitaji znz ila znz inatuhitaji sana.period.
Ona sasa imefika wakati wa gharama wanajichafua nguo hovyo. Wale wanaosema Tanganyika inawanyonya znz wajiulize kama mwenyekiti wa kamati anasema hawana uwezo, Tanganyika inawanyonya wapi.
Hawa watu wamefundishwa ujinga wa kuamini maneno ya mitaani bila ushahidi wa kiuchumi.
Tunasema hivi serikali ni tatu na kila mmoja achangie sawa.
Muda wa kubeba watu migongoni wakitukana hovyo iumekwisha.
Hiki ni kijimkoa tu lakini kelele tu wamejaaliwa. Tutakomaa hadi mtaomba radhi kwa maneno yenu machafu.
Wananyanyua pua eti muungano ni nchi mbili wabia sawa. Thubutu, wabia sawa wakati wewe unachangia maneno na kelele ! usawa wa ubia upo wapi.
Wewe unavia kodi za Mtanganyika halafu unasema ubia sawa. Hawa watu waajabu sana.
Leo wanasema hawana uwezo na wakati wa kujadili muungano hali ya uchumi iangaliwe.
Ni hawa hawa walikomaa tume iwe na wajumbe sawa. By the way hawajui gharama za tume wala za bunge la katiba.Kelele zitawatokea puani this time
fungeni midomo na muwe na adabu. Shikeni adabu, muungano uchumi si mipasho na taarabu.
Leteni kitu mezani si kuvizia nafasi za urais wa zamu na uwaziri. Kupe wakubwa mninyi.
Mkome kusema mnanyonywa, nani anyoinye mnasikini wa mapato kama yenu.
Mkome kudai vyeo msivyojua gharama zake. Matabaki chini ya kivuli cha Tanganyika kwasababu hamna uwezo.period
GHIBUU takashi Jusa Jasusi JokaKuu Kakke Jasusi Nonda gombesugu Zinedine FJM
Kwani ni nani aliefanya na kupanga Mapinduzi ? Yale ya kuipindua Serikali halali ya Zanzibar na hata yale ya kumpindua Karume ni nani Liepanga Mapinduzi hayo ???
Mgogoro mbona haukutokea ? Na hata kama ungetokea ni haki yake kutokea kwani wakati huo mambo ya kupinduaa serikali yalikuwa ni fashion katika nchi chingi za Kiafrika .
Hivi ni nani aliesema Muungano mwisho Chumbe ? Huyu alikuwa na maana gani ?Nyerere alikuwa msomi Karume alikuwa ni mtu aliekuwa hana elimu ,sasa kama nikikwambia Nyerere alimlaghai Karume nitakuwa nakosea ?
Habari ya Dhoruba isikupe tabu sana kwani asilimia 99 ni waislamu ,hivyo hatima yao inategemea Mwenyezi Mungu haina wala haihitaji ni wapi wewe upo kijiografia au kisaikolojia ,ukame unauelewa,maradhi unayajua ,kimbunga unakifahamu na mvua umewahi kuiona yote hayo hata uwe juu ya mlima basi yanaweza kabisa kukumaliza uhai na kuharibu uso wako wa arhi,natumai umewahi kusikia tetemeko la ardhi nalo ni baa kubwa lisilo na sumile.
Sasa tatizo ni kitu gani ,kuhitajiana ? Hapo sioni ubaya ,kwani tukiwa nje ya Muungano kutaondoka huko kuhitajiana ?
Na kama kutaondoka basi nyie mtakuwa mna roho mbaya sana na nia zenu sio nzuri , Umeona Philipines ,mbona wamesaidiwa sana tu na wao kimbunga kimewaweka katika hali mbaya.
WaZanzibari hawapo katika kujaribu kuuvunja Muungano .wapo katika nia ya kuukataa Muungano na nia na madhumuni ni kuuondoa usiwepo na kama ukiwepo basi wa makubaliano sio wa kiulaghai.
Ndugu yanguUkweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.
Kitu cha ajabu sana ni hao hao wanataka tume iwe asilimia 50, wanataka bunge la katiba liwe asilimia 50. Wanataka viongozi wa muungano na wafanyakazi wa serikali ya muungano wawe nusu kwa nusu.
Tumewahi kuwaeleza mara nyingi sana wazanzibar akiwemo Jusa na Ahmed Rajab kuwa Tanganyika haihitaji znz kwa lolote. Hatuhitaji znz ila znz inatuhitaji sana.period.
Ona sasa imefika wakati wa gharama wanajichafua nguo hovyo. Wale wanaosema Tanganyika inawanyonya znz wajiulize kama mwenyekiti wa kamati anasema hawana uwezo, Tanganyika inawanyonya wapi.
Hawa watu wamefundishwa ujinga wa kuamini maneno ya mitaani bila ushahidi wa kiuchumi.
Tunasema hivi serikali ni tatu na kila mmoja achangie sawa.
Muda wa kubeba watu migongoni wakitukana hovyo iumekwisha.
Hiki ni kijimkoa tu lakini kelele tu wamejaaliwa. Tutakomaa hadi mtaomba radhi kwa maneno yenu machafu.
Wananyanyua pua eti muungano ni nchi mbili wabia sawa. Thubutu, wabia sawa wakati wewe unachangia maneno na kelele ! usawa wa ubia upo wapi.
Wewe unavia kodi za Mtanganyika halafu unasema ubia sawa. Hawa watu waajabu sana.
Leo wanasema hawana uwezo na wakati wa kujadili muungano hali ya uchumi iangaliwe.
Ni hawa hawa walikomaa tume iwe na wajumbe sawa. By the way hawajui gharama za tume wala za bunge la katiba.Kelele zitawatokea puani this time
fungeni midomo na muwe na adabu. Shikeni adabu, muungano uchumi si mipasho na taarabu.
Leteni kitu mezani si kuvizia nafasi za urais wa zamu na uwaziri. Kupe wakubwa mninyi.
Mkome kusema mnanyonywa, nani anyoinye mnasikini wa mapato kama yenu.
Mkome kudai vyeo msivyojua gharama zake. Matabaki chini ya kivuli cha Tanganyika kwasababu hamna uwezo.period
GHIBUU takashi Jusa Jasusi JokaKuu Kakke Jasusi Nonda gombesugu Zinedine FJM
Sasa Baraqhas ... mnachotaka ni nini? Kwa nini uwe wa mkataba? Kwa nini msiseme hamtaki muungano kabisa tujuwe moja? Muungano wa mkataba ndio ukoje? Tafadhali fafanua
gombesugu,
..suala la mapato ya Tanganyika vs Zanzibar lilishaletwa hapa JF ambapo tulipitia taarifa za chombo kinaitwa Joint Finance Commission. Tulichokiona ktk taarifa hizo kinashabihiana na maoni ya huyo mwakilishi.
..baadhi ya wachangiaji hupenda kucheza-cheza vifungu vya sheria na maneno. sasa watu kama hao hukwama pale takwimu zinapowekwa wazi. katika suala la mapato/makusanyo ya fedha za ndani ukishatoa mahesabu ya Zanzibar kilichobakia ni jasho la wa-Tanganyika.
..mwisho, naendelea kusisitiza kwamba muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar hauwezekani kutokana na tofauti ya eneo na population baina ya mataifa haya mawili.
..Znz inaweza kusimama yenyewe na kupiga hatua za maendeleo nje ya muungano. kinachotakina ni Znz kuwa na sera nzuri na utekelezaji makini ktk matumizi ya rasilimali zake. kama Seychelles, na Mauritius wameweza, sioni kwanini Zanzibar ishindwe.
NB:
..nimekusamehe kwa kutukejeli na kutuita "wadanganyika", na kuifananisha Tanganyika na maiti.
cc Barubaru
Ndugu yangu
Kwa maoni yangu ni kwamba zanzibar haina uwezo wa kuchangia asilimia 50 katika muungano, sio kwamba haina uwezo wa kuchangia bali kutokana na mfumo mzima wa muungano, lakini uwezo inayo zanzibar kama muungano utakuwa wa haki na usawa, isiwe kama sasa zanzibar inapewa asilimia 4.5 katika magao ya mungano, katika bank kuu ambayo zanzibar imechangia asilimia 11 inapewa 4.5 ,kwa hilo zanzibar haitaweza kuchangia katika muungano.
Hivi sasa zanzibar vile vitu ambavyo vya kuikwamua kiuchumi vimebanwa au vimebebwa na muungano, kwa maana hio zanzibar haitaweza kuchangia asilimia 50 ya muungano.
Kama zanzibar itapewa mamlaka kamili tukaja na mfumo wa muungano wa shirikisho kama wa mkataba zanzibar inayo uwezo wa kuchangia asilimia hamsini.
Hivi sasa zanzibar inapewa kwa maneno tu 4.5 katika muungano, lakini asilimia hio hio 4.5 zanzibar haipati hata nusu kwa kila mwaka toka muanzishwe huu muungano, hivi kweli tutaweza kuchangia asilimia 50 ? Muungano huu ni wa vyama vya siasa tu, sio muungano wa ukweli na wa haki.
Zanzibar inaweza kama tutakuwa wakweli, nadhani bwana Salim hakuweza kuchangia au kutoa maelezo zaidi vipi zanzibar itashindwa kuchangia katika muungano,kwa kulinda card yake ya ccm, na tonge yake.
MUUNGANO NI wa mkataba tu.
Joka Kuu.
labda unieleze taarifa ya JFC imewekwa katika mada gani? Kwani siku zote nimekuwa nawaeleza ukitaka taarifa sahihi za Finance ta TGK na Znz pitieni ripoti zao ambazo zinakuwa zinajieleza vizuri sana lakin sijui kama kuna mtu aliyepitia zaidi ya watu kuleta maneno ya mitaani kuisemea vibaya Znz.
Niambie ni uzi gani ili niipambanue zaidi kwa kutumia taaluma yangu kwa faida ya wengi.
Sasa anataka report ya JFC ili kupata nini zaidi? Pili, yeye hajaweka lakini anadai iwekwe, na nani. Kama anadhani kuna jambo kubwa katika JF Barubaru aliweke hadharani...kwa kumbukumbu zangu wewe ndiye uliyeibua suala la Joint Finance Committee.
..nadhani mjadala wa taarifa za kamati hiyo tulishaumaliza. sidhani kama kuna kitu kipya kitajitokeza.
..hoja yangu ni kwamba Znz is too small kulinganisha na Tanganyika. kwa mazingira hayo muungano si jambo rahisi kwa mataifa haya. It is next to impossible.
..mimi nadhani kila upande uende kivyake vyake, ila tushirikiane kupitia EAC na SADC. kwenye vyombo hivyo kuna mambo yote ambayo Znz inayahitaji ktk "muungano wa mkataba", mfano masuala ya ulinzi, ardhi, biashara, etc etc.
cc gombesugu, Nguruvi3
Wenzenu pesa zote wanapeleka katika makanisa kupitia MoU ya Serikali ya JMTz na kanisa iliyosainiwa na Lowasa. makanisa kwa sasa yanachukua Bilioni 1.2 kila mwaka kutoka katika kodi za wananchi achilia mbali misamaha ya kodi na ulaghai mwingine.
Someni bajeti za JMTz muone hayo.
Sasa anataka report ya JFC ili kupata nini zaidi? Pili, yeye hajaweka lakini anadai iwekwe, na nani. Kama anadhani kunwa jambo kubwa katika JF Barubaru aliweke hadharani.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya BLW kasema mapato ya znz ni bilioni 240.
Nimeweka bbajeti ya znz kwa mwaka 2013 katika uzi mwingine. Inaonyesha mapato ya ZRB na TRA ambayo kwa pamoja na mapato hayajafikia bilioni 500.
Rais sheni kasema wznz wasidharau hiyo 4.5 wanayopata katika muungano. Akauliza znz inachangia kitu gani hadi ilalamike?
Ukisoma bajeti ya zna mambo yafuatyo hayamo
Ulinzi na usalama
Mambo ya ndani
Elimu ya juu
Na bado wana access katika mambo yasiyo ya muungano kama afya.
JFC itasaidia nini kwa hesabu za bilioni 240!
Hakuna usawa kati ya Tanganyika na znz hata siku moja. Ni mwendawazimu peke yake anayeweza kudhani kitu kama hicho kipo.
Hawa watu ni kuachana nao, hatuwezi kuishi kwa malalmiko kila siku. Hatuna tunachopoteza.
Tuwaache wajenge Dubai yao ya wakati wa Sultan. Znz yenye uchumi imara inawezekana kabisa lakini lazima wawe tayari kujikomboa kwa kuukata muungano si kuodai idadi ya wajumbe bunge la katiba, kamati ya Warioba, vyeo au ajiira.
Let them go !
Ninakubaliana na wewe ila kuna kitu sikuelewi.Sasa anataka report ya JFC ili kupata nini zaidi? Pili, yeye hajaweka lakini anadai iwekwe, na nani. Kama anadhani kuna jambo kubwa katika JF Barubaru aliweke hadharani.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya BLW kasema mapato ya znz ni bilioni 240.
Nimeweka bbajeti ya znz kwa mwaka 2013 katika uzi mwingine.
Inaonyesha mapato ya ZRB na TRA ambayo kwa pamoja na mapato hayajafikia bilioni 500.
Rais sheni kasema wznz wasidharau hiyo 4.5 wanayopata katika muungano. Akauliza znz inachangia kitu gani hadi ilalamike?
Ukisoma bajeti ya znz mambo yafuatyo hayamo
Ulinzi na usalama (ambao wenyewe tu unaweza kuchukua 1/2 ya 240)
Mambo ya ndani (1/4 ya 240)
Elimu ya juu (1/8 ya 240)
Na bado wana access katika mambo yasiyo ya muungano kama afya.
JFC itasaidia nini kwa hesabu za bilioni 240!
Hakuna usawa kati ya Tanganyika na znz hata siku moja. Ni mwendawazimu peke yake anayeweza kudhani kitu kama hicho kipo.
Hawa watu ni kuachana nao, hatuwezi kuishi kwa malalmiko kila siku. Hatuna tunachopoteza.
Tuwaache wajenge Dubai yao ya wakati wa Sultan. Znz yenye uchumi imara inawezekana kabisa lakini lazima wawe tayari kujikomboa kwa kuukata muungano si kudai idadi ya wajumbe bunge la katiba, kamati ya Warioba, vyeo au ajiira.
Let them go !
Barubaru , JokaKuu kakata mzizi wa fitna kwa kuweka hadharani kila mtu aone.Barubaru, gombesugu, Nguruvi3,
..ripoti ya Joint Finance Committee hii hapa nawaletea.
..i hope 3 months later hatutarukana kwamba ripoti hii haikuletwa.
..fuata linki hii:http://www.jfc.go.tz/downloads/mapato.pdf
Technically Tanganyika ndiyo Tanzania.Ninakubaliana na wewe ila kuna kitu sikuelewi.
Daima unakuwa katika hoja ya kuwa Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika na unaitetea hoja yako vizuri sana (kimtazamo wangu) ila ninapokosa kukuelewa ni pale unapowapa Wazanzibari ambao ni "mzigo" privilege ya kuuvunja Muungano!
Katika hali ya kawaida ni Tanganyika "mbeba" mzigo ndiyo ambayo ingekuwa au kujipa privilege ya kuutua mzigo, mbona imekuwa kinyume tena?
Kama Wazanzibari hawataki kuitumia privilege mliyowapa ya kuuvunja Muungano na badala yake wakaamua kuchezacheza na maneno, je mtaendelea kuubeba "mzigo" mpaka lini? hakuna ukomo?
Hii nyuzi haihusu mambo ya dini. Unachotaka kufanya ni kutuondoa katika mada na ukweli. Tafadhali kama huna hoja kaa kimya.Wenzenu pesa zote wanapeleka katika makanisa kupitia MoU ya Serikali ya JMTz na kanisa iliyosainiwa na Lowasa. makanisa kwa sasa yanachukua Bilioni 1.2 kila mwaka kutoka katika kodi za wananchi achilia mbali misamaha ya kodi na ulaghai mwingine.Someni bajeti za JMTz muone hayo.