Zanzibar Business and Property Registration Agency( BPRA) nahitaji majibu kutoka kwenu

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
206
Leo nimejaribu kufungua account ya kimtandao ya Online Registration System (ORS) katika taasisi ya Business and Property Registration Agency(BPRA).Taasisi hii iko Zanzibar na inafanya shughuli zinazofanana na zile za BRELA.

Katika utambulisho wa mfunguaji akaunti kwa maana ya utaifa(Nationality) list inaanza na "ZANZIBARI" na inaendelea kuorodhesha utaifa wa nchi zote duniani. Sasa ukiendelea na hiyo orodha utakutana na utambulisho wa "TANZANIAN" Je huu utambulisho wa utaifa wa "ZANZIBARI" na "TANZANIAN" umekaaje?

BPRA nipeni majibu!!!!!!!
 
Nadhani ungeangalia sheria inayosimamia hiyo BPRA. Kwa vile si chombo cha muungano, inawezekana kuwa ime'define mfano " For the purpose of this law, Tanzanian means....or Zanzibari means... Huwa wanasemaga hivyo wanasheria na maana yake ni Kwamba kwa 'sheria hiyo tu' Mimi mwenyewe ilikuwa inanichanganya hadi nikauliza wanasheria mfano utasikia kumiliki ardhi Zanzibar ni lazima uwe mzenji, ukiangalia tafsiri ya mzanzibari, kumbe ni mtanzania aliyeishi Zanzibar kwa kipindi kishochopungua miaka 10 na sio mfululizo au bila ya kutoka!
 
Back
Top Bottom