KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Mkuu 'Detective J' Asante kwa mchango huu; lakini hapa kila mtu sasa ni bingwa wa aina zote ya magonjwa haya, na Profesa wetu mkuu ni 'Dr Rais, PhD'.Huwez kuishi na ugonjwa ambao ni pandemic uka u treat kama endemic. Itakula kwako
Akisema tu "tuzoee kuishi na huu ugonjwa" tunamuelewa na hakuna wa kubisha.
Akisema 'coronavirus' ni kaugonjwa kasikotutisha, sote tunadakia na kuimba wimbo huo huo.
Akisema dawa ni "kujifukiza na kula malimao", kwa nini mtu asiamini.
"Vipimo ni feki" n.k., sote tunadakia na kuanza kampeni dunia imtambue kwa mchango wake kiongozi wetu huyu.
Hapa sasa unatuwekea 'endemic na pandemic', hata tukijua tofauti yake itasaidia kitu gani huku kiongozi wetu akielekea kushinda 'vita'.? Huko sio kutaka kumpunguzia sifa zake alizojizolea duniani?