Amani na utulivu,
Ndio kauli za viongozi wa Tanzania ambao wanahisi wanalinda amani na utulivu kumbe Watanzania ni waoga wa kudai haki zao za msingi.
Angalia chaguzi za Zambia na Malawi utajua hao walistaraabika muda mrefu sana na katiba zao ni imara kuliko sisi wakumbatia ujamaa hewa.
Haiingii akilini jitu kama polepole au bashiru waliovuruga chaguzi zote kuanzia serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu leo wapo uraiani na wanachangamana na sisi raia waliotukanyagia na kusigina haki zetu za msingi.
Chaguzi za Tanzania imekua maigizo makubwa sana na Tume inafanya maigizo hayo bila woga, rejea swaga za mahela na wenzake kwenye chaguzi zote.
Chaguzi za Tanzania haziko huru na hazina haki wapinzani hunyanyasika kuanzia kampeni hadi kwenye kupiga kura.
Polisi kuacha kulinda Raia na mali zao wanabaki kukimbizana na wapinzani mara wakimbizane kuzuia mikutano ya ndani unawacheki unaona hawa akili zao ziko nyuma mno, Polisi acheni wanasiasa wapambane kisiasa kazi yenu kulinda amani tu tena mpo kwenye nchi isiyo na vikundi vya waasi lakini mnabehave worse.