Zamani ilikuwa raha

Zamani ilikuwa raha

Ahahaaaaa.
Nakumbuka kaka angu alikuaga ananituma kumpelekea barua demu wake.Siku1 niliisoma kisha nikakopy maneno ili na mm niwe natongozea!!!!
Dah kweli bhana,kila demu niliyekua nikimtongoza kwa kutumia ile sound copy ya ma bro alikua hachomoi.
Nakumbuka moja ya sound eti "SILI SILALI HAPPY,NIKINYWA MAJI NAKUONA KWENYE GLASI.
WEWE NI MREMBO KULIKO YONDO SISTER!!!!!
 
Zamani saa unarekebisha, kulingana na redio. Baada ya zile ngoma unasikiliza: ti, ti, ti, tiiiiiiiiiiiiiiii. Hi ni Redio Tanzania Dar es salaam

umenikumbusha marehemu babu yangu nilikuwa nalala nae alikuwa ana saa ambayo haitumii betri ila baada ya siku kadhaa anaikoki kwa kutumia mshale wa saa kabla ya hako kamlioo kaa ti ti ti tiiiiii kisha anarekebisha marija, kipindi nilichokipenda sana ktk redio ni chemsha bongo na pilika pilika ila alikuwa akinifinya karibia kila siku asubuhi akinitaka niamke kwenda shule nilikuwa darasa la 4 mwaka 2004 kwan kijj kuna barid kali hivyo usingizi wa asubuh mtamu kweli Mungu amrehemu
 
Kwenda sekondari ilikuwa ni heshima kwa jamii inayokuzunguka. Wakati wa kwenda shule husindikizwa na kundi la watu huku umesaidiwa sanduku. Tulipanda treni.

Tiketi tulitunza kwani nauli tulirejeshewa baada ya safari. Makonda wa treni (tt) walikuwa ni wahindi.

Mwl.alipohamishwa shule ilipikwa pilau, pia mashairi yaliimbwa.

Picha tulipiga studio tena baada ya kusevu kwa muda mrefu.... Tofauti na siku hizi ''selfie''.

Tulisikiliza RTD, kwa miziki idhaa ya biashara.

Range rover haikuruhusiwa ku paki benki. Peugeot 504 iliaminika ni gari ya wahuni/majambazi.
Namba za serikali ilikuwa stb, stc, std, stg. Za wahisani ilikuwa tx - plate number nyekundu.

Sikukuu ya saba saba ilifana sana kitaifa ilifanyika. Na mikoa mingine ilishiriki pia.

Vitabu madaftari shule za msingi ilikuwa bure. Daftari likijaa unapeleka kwa mwl.wa darasa anakupa jipya
ole wako karatasi zikutwe pungufu, viboko vilitawala mashuleni na nidhamu ilikuwepo pia.

Wanafunzi shule ya msingi baadhi walikuwa wananyoa ndevu.

Inaendelea hapa
shule za boys mnakumbuka mafuta ya taa kwenye msosi habari za puchu kisimani
 
Ha ha ha ha ha Mkuu wewe umenikumbusha mbaaali sana na zile ladha zao sauti za watangazi wa Redio Tanzania Dar Es Salaam na kale kamlio wa ti ti ti ti tiiiiiiiiiiiiiiiii
Walikuwa wanaanza hivi, "Hivi sasa ni saa mbili kamili za usiku, hii ni taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania Dar Es Salaam,

Kigoma

Waziri Mkuu wa Tanzania Ndugu John Malecela amewataka wakulima wa zao la mawese mkoani Kigoma kuongeza kwa bidii uzalishaji wa wa zao hilo....."

Daaah nimekumbuka sana enzi hizo hahahaha!

Mkuu,umesahau kidogo hapo
Hii ni taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania Dar Es Salaam,
Msomaji Abdul Ngarawa.
 
Mabasi binafsi hayakuwepo, yalikuwepo mabasi ya KAMATA aina ya FIAT na malori ya BEDFORD ya KAJIMA.

BEDFORD na ISUZU lori nyingi zilikuwa za serikali ,na mlangoni zimeandikwa hivi mfano : OFISI YA MKUU WA WILAYA,
ELIMU
KILOMBERO.
Hilo neno elimu , ni Idara ambapo hilo lipo mikononi mwao.
Kama lipo chini ya idara ya Ujenzi, linaandikwa ujenzi.
 
nani analikumbuka lile tangazo la sabuni ya Mshindi..: mshindii sabunii mpyaa yenyee nguuuvuu..yenyee kutakasaa kulikoo zooote...mshindiii iiii eeeeeehhh...!!!

Afu Mama na mwana je na zile hadithi za jini mla watu?
 
Hapo kwenye Red panahitaji ufafanuzi ile wanetu waelewe vyema by the way nitaongeza hapa;

  • Kuhamishiwa Mtwara au Sumbawanga kwa mfanyakzi ilikua laana tosha
  • Tulitishwa kupelekwa Mafya (kisiwani)
  • Ukivaa chumpi mpya hasa za Zabron au 007 lazima kale ka chuma kaonekane ili washikaji wajue umenunuliwa mpya
  • Matozi waliitwa magwangwe na maranyingi walikua hawatawazi
  • Wakuu wa wilaya waliweza kukutandika bakora mbele ya mkeo
  • Ubakaji ilikua tendo la kawaida tuuu lilitwa Mande au mtungo
  • Tulisafiri kwa juma kwenda Mtwara
  • Wakazi wa Kigoma walijivunia biasha ya homela homela wenyewe wakiita pia BIZE
  • Form 4 alikua msomi na angeweza oa mtoto wa mwenyekiti wa kijiji
  • Ma bwana mifugo walitutibu GONO pia kwa sindano za ng'ombe na tulipoa
  • Tulipanda foleni ili tupate kipande cha sabuni ya Ilula
  • Chai walikunywa waungwana wa town sis zetu uji kwa asali
Safi sana mkuu. Hiyo doti namba tatu nakumbuka siku nilipo vaa wasichana waliniadmire sana kiasi kwamba nilifanikiwa kujiokotea wanne kwa zamu kwani nilionekana babu kubwa. Nyakati zile kutongoza ilikuwa ni kazi mpaka uandike barua uchore na maua na hasa lile umbo la moyo kisha unapitisha mshale katikati. Ulikuwa unaweza kuchukua hat mwezi kabla hujampata msichana. Lakini kwa chupi hiyo ilikuwa inakupunguzia usumbufu! Yaani ilikuwa ni kama mtu mwenye gari sasa hivi ingawa wasichana wa sasa hivi hata gari hawamind. Pesa tu!

Hiyo doti namba tano umenikumbusha marehemu Kleruu aliye kuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa. Huyu alikwenda kwa Mwamwindi siku ya Krismas akataka kuleta za kuleta akijua atatetemekewa. Mwamwindi hakuwa mtu wa kuramba miguu ya wakubwa. Aliingia ndani akatoka na gobole na kumfumua kisha akamuweka kwenye budi na kumpeleka kituo cha polisi Iringa.
 
Hao jamaa wachapishaji wa hilo gazeti walikuwa wanakaa hapo Kariakoo jirani na FaizaFox.Mtaa fulani hivi.
Hizo ndio zilikuwa burudani za wakati huo. Magazeti ya habari wakati huo yalikuwa UHURU/MZALENDO, DAILY/SUNDAY NEWS, MFANYAKAZI na KIONGOZI. Magazeti mengine ya burudani yalikuwa kama BUSARA na MISAKATO lililokuwa linachapishwa ligi kuu inapoisha. Redio ilikuwa RTD tu. Hakuna TV nyakati hizo
 
Suruali za jeans hazikuwepo kulikuwa na suruali za codrai na surual za mabuga luuu, ndo zilikuwa fashion.

Zilikuwepo pia mkuu ila kwa uchache zikijulikana kwa jina la DANGLIZI na label iliyotawala ilikuwa ni moja tu LEE na hazijawahi kutokea tena jeans kama zile maana zilikuwa very strong
 
Hapo kwenye Red panahitaji ufafanuzi ile wanetu waelewe vyema by the way nitaongeza hapa;

  • Kuhamishiwa Mtwara au Sumbawanga kwa mfanyakzi ilikua laana tosha
  • Tulitishwa kupelekwa Mafya (kisiwani)
  • Ukivaa chumpi mpya hasa za Zabron au 007 lazima kale ka chuma kaonekane ili washikaji wajue umenunuliwa mpya
  • Matozi waliitwa magwangwe na maranyingi walikua hawatawazi
  • Wakuu wa wilaya waliweza kukutandika bakora mbele ya mkeo
  • Ubakaji ilikua tendo la kawaida tuuu lilitwa Mande au mtungo
  • Tulisafiri kwa juma kwenda Mtwara
  • Wakazi wa Kigoma walijivunia biasha ya homela homela wenyewe wakiita pia BIZE
  • Form 4 alikua msomi na angeweza oa mtoto wa mwenyekiti wa kijiji
  • Ma bwana mifugo walitutibu GONO pia kwa sindano za ng'ombe na tulipoa
  • Tulipanda foleni ili tupate kipande cha sabuni ya Ilula
  • Chai walikunywa waungwana wa town sis zetu uji kwa asali
Hapo kwenye red mkuu pana maelezo mengi sana. Lakini ni kuwa Nyerere alipendwa, kuheshimiwa, kuwaadmired na kuheshimiwa na kila mtu. Alichokisema kilikuwa ndiyo dira na kilitekelezwa na kila mtu bila ubishi. Alikuwa ndiye chanzo cha fikra ambapo baadaye tuliimba "zidumu fikra sahihi" ambapo kwa sehemu kubwa zilikuwa sahihi kweli. Huyu ndiye alianza kuongoza nchi akiwa mchanga na nchi ikiwa changa pia. Alijitahidi sana kutuunganisha kama taifa kwa kuua ukabila na udini. Alipigigania ili kila mwananchi afaidi kile kidogo tulicho nacho kwa usawa. Alianzisha Azimio la Arusha ili kuhakikisha kuwa kwa sehemu kubwa viongozi wanajali wananchi kwanza kwa kuweka maadili makali ya uongozi. Kwa kutumia rasmali za nchi na misaada kutoka kwa nchi rafiki, alitoa elimu kuanzi ya msingi hadi chuo kikuu na afya bure. Hivo ndizo nyakati ambazo kila kitu kilikuwa kinapatikana shuleni kuanzai daftari, kalamu, vifutio na vitabu bure. Daftari likiisha unakwenda kwa mwalimu anakupa jingine. Hakukuwa na maduka ya dawa enzi hizo kwani dawa zote zilikuwa zinapatinaka katika hospitali bure. Mkuu wengi wetu tunaochangia uzi huu kama sio Nyerere tusingejua hata maana ya Jamii Forums kwani tusingekwenda shule kutokana na umasikini na huenda tungekuwa tulishakufa zamani kwa maradhi kutokana na kushindwa kujitibu kama ilivyo sasa. Hata hawa viongozi wakubwa ambao wanaifisidi nchi wasingekuwa katika nafasi hizo kama si kazi ya Nyerere.

Nyerere alijenga viwanda vingi na mashirika mengi ambamo wasomi na wasio wasomi waliajiriwa. Wakulima walikuwa na uhakika wa soko la mazao yao kwani tulikuwa na viwanda vingi hapa nchini na pia kulikuwa na utaratibu wa kuuza nje wakati huo chini ya Gapex. Mzee yule aliuvunjilia mbali ukabila na udini kupitia elimu na ajira. Ukimaliza shule ya msingi unapelekwa mkoa mwingine kabisa na ukiajiriwa unapelekwa mkoa mwingine kabisa. Kwa mtindo huo tukajikuta tunaoleana na hivyo kuwa taifa moja. Hii ilifanikiwa kutokana na kuvunja uongozi wa kikabila wa machifu ambao katika nchi nyingine umeendelea na kuleta mapigano ya kikabila. Alijenga heshima kubwa sana ya nchi nje ya mipaka yetu hata ikulu paliheshimika sana mpaka akapaita mahali pa takatifu. Tena yeye kwa miaka zaidi ya 24 alikuwa pale bila fensi lakini palikuwa na heshima kubwa sana. Kama binadamu alikiri kuwa kuna maeneo alikosea lakini si kwa kusudi la kujinufaisha bali katika mkondo wa kumsaidia mtanzania masikini na akasema viongozi wanaomfutia wanapaswa kuchikua mema na kuyaacha mabaya ingawa mwishoni mwa maisha yake alisikiktika sana kuwa viongozi wanaacha mema na kuchukua mabaya ikiwa ni pamoja na kuliua Azimio la Arusha. Mzee yule aliteseka sana kuisimamisha nchi bila hata kujipendelea yeye ndiyo maana huwezi kusimama mahali ukasema Nyerere alijinufaisha yeye kwa kuiba au kuifisidi nchi hii. Nyakati zile zilikuwa ni za chama kimoja hivyo angekuwa na roho ya tamaa na wizi kama waliomfuatia angeweza kuchukua hata sehemu kubwa ya Dar es Salaam kuanzia Ubungo hadi Kiluvya na kusema ni eneo au shamba lake. Angekuwa na utajiri wa majumba na mali nyingi nyinginezo bila hata kuwepo mtu wa kumuuliza au kumuhoji kwani hakukuwa na uhuru wa kuhoji kama ilivho sasa. Huyo ndiye Nyerere ambaye nimesema alikua kama Mungu kutokana na hayo niliyasema. Mungu amrehemu, Amini.

Sasa mkuu angalia kimbunga cha madalali, mafisadi, wezi na wauaji waliokuja baada ya Mwalimu walichokifanya walipoingia ilkulu:
- Wakalivunjilia mbali Azimio la Arusha na kuanzi kujitajirisha wao na familia zao
- Wakajiuzia nyumba za serikali alizojenga Nyerere kwa ajili ya watumishi wa serikali
- Wakapiga mnada viwanda, mashamba na mashirika yote ya umma aliyoanzisha Mwl ikiwemo benki iliyokuwa kubwa kabisa ya NBC
- Ikulu palipokuwa pa takatifu wakapageuza pango la wanayang'anya na sehemu ya biashara. Kutoka hapa ndipo dili za EPA, Richmond, Rada na hatimaye Escrow zilipopigwa. Wake zao wakatumia ikulu na rasmali zake kuanzisha NGO zao kwa migongo ya masikini wa nchi hii, Wengine kama haitoshi wakaanzisha na makampuni binafsi na wake zao na kujimilikisha baadhi ya mashirika ya umma kwa bei ya kutupa
- Migodi yote wakabinafsisha
- Elimu na afya vikageuzwa biashara ndio maana si ajabu ukasikia mtua anaomba msaada wa Sh laki 3 au 5 ili akatibiwe katika hospitali ya umma kama Muhimbili na kukosa hatimaye kufa lakini wakati huo huo utaambiwa kuna mtu analipwa sh. 1.5 kwa siku kwa kusimamia ufungaji wa viti vya bunge la katiba mpya
- Wakulima wakaachwa wajifie wenyewe kwa kukosa masoko ya mazao yao lakini hata pale wanapopata masoko serikali inawazuia kuuza kwa kisingizio cha njaa au magendo wakati huo huo ikichukua ushuru mkubwa na kuwaacha wakulima na umasikini wa kudumu
- Serikali ikageuka muuaji wa raia kwa kuwalipiua kwa mabomu na risasi za moto wanapiokuwa katika shughuli zao za amani za kisiasa na kijamii. Mifano ni mingi - Zanzibar, Arusha, Morogoro, Iringa, Songea, Mbeya, operesheni tokomeza nk
- Uongozi ukageuzwa ni biashara badala ya utumishi. Wakajiita waheshimiwa. Wenye pesa sasa ndiyo wanaoununua uongozi na wengi wako kazini na mabilioni yao wakiwanunua wananchi kwa njia mbali mbali ili wawa unge mkono
- Chama kilichokuwa cha wakulima na wafanyakazi kikageuzwa kuwa cha wafanyabiasha na matajiri. Sasa hivi ndio ajabu unasikia viongozi wa chama wakihubiri sera za udini, ukabila na ukanda kuonesha jinsi walivyofilisika kisiasa
- Wananchi kufurushwa, kuumizwa katika maeneo ya asili ili kuwapisha wanyama kwa kisingizio cha hifadhi ya wanyama
nk. nk.

Hivyo mkuu hakuna kiongozi anayeweza kupewa heshima kama alizopewa Nyerere kwa kazi kubwa aliyofanya kwa sasa. Sasa hivi si ajabu ukasikia au kusoma kuwa kiongozi mkubwa kabisa anaitwa fisadi, mwizi, mwongo, dhaifu, mwoga, msafiri, omba omba, vasko da Gama, nk nk. Kwasababu hizi ndizo nyakati ambapo wezi wanatetewa kuwa hawakuiba kwakuwa ndizo nyakati ambazo pesa za umma zinageuzwa kuwa za binafsi, ndio nyakati ambazo wezi wanaiba na nyingine wanazipeleka pahala pa takatifu alipopaacha Nyerere, ndio nyakati ambazo unasikia wezi wanapewa muda wa kujirekebisha, ndizo nyakati ambazo wezi wanaambiwa warudishe walichoiba halafu watafichiwa siri na hawatashitakiwa, ndizo nyakati unazosikia tapeli wa serikali(richmond) anakaribishwa pahala pa takatifu alipopaacha Nyerere, ndizo nyakati unazosikia tuhuma zote ovu zianatokea pahala patakatifu. ndizo nyakati unazosikia kuwa watu wanabeba pesa za migao kutoka benki kwa maboksi, lumbesa na mifuko ya sandalusi. Madudu na maajabu yote hayo yangepita mlango gani nyakati za Nyerere? Nina imani majina yatakapotoka tutashangaa mshangao wa kufa kwani hayo ya wenye milioni 10 za mboga, maaskofu na majoka yenye makengeza ni cha mtoto! Time'll tell!
 
Mkienda 77 tulikuwa tunafurahia kununua mikate ya siha kwa bei nafuu. shamrashamra za 77 zilipambwa kwa bidhaa toka viwandani kwa bei ya kiwanda kama vile mwatex. urafiki n.k.
 
Wakati huo tulichamba kwa gunzi la mahindi,kunya ilikuwa popote tu,vyoo vifupi,basi la kwenda Mufindi-Iringa Mjini-Malangali ni Mkombozi Express na linapita Mara mbili kwa wiki wenyewe kule walikuwa wakiliita Mkombosi,...Shule ilikuwa mchana tunarudi Kula then mchana unabeba jembe ni kupalilia,....Wasioenda zamu wakati wa likizo ilikuwa ni bakora Kali sana mbele ya assemble tuliyoiita 'mistarini' enzi hizo 1992 shule ya mazoezi masebe Ushirika TUKUYU,alikuwepo mwalimu kibona anakutandika bakora hata 20 kisha anakwambia "kamwambie baba yako nimekutana na Linyambuuta"...Michezo ilithaminiwa sana kv tufe,riadha,mkuki,soka,kuruka viunzi,nk Kati ya shule na shule kata na kata au tarafa na tarafa enzi hizo UMITASHUMTA,...Chupi tulizovaa ziliitwa Vipi hizo zinavutika kama manati...viatu maarufu zilikuwa raba za DH aka Dingi Hanauwezo mtaani kiatu maarufu zilikuwa ndopa brands kv Benque...Burudani ya kijanja soukous music za kongo kina harusimabele,yondo sister,shalamwana,boziboziana etc...Movie maarufu Commando John Ile alocheza na Jane,pia kipenzi,Synsia,Jet Li,Tai Chi,nk enzi hizo Mbeya Mjini Chonicho anavuma kuonyesha hizo pale Uyole...Majambazi waliogopwa sana kv kina Jombi,_Bob G. Kule Mbeya walikuwa ni smugglers sana wa bidhaa kutoka Malawi kv sukari na bia za Carlsberg "probably the best beer in the world"....Ukiona Pikipiki enzi hizo ujue Bwana shamba anapita...ilikuwa rahisi kuokota pesa sio siku hizi hata sh 50 bahati...pesa ilikuwa na nguvu eg gome la shingi 20 au dala unanunua vitafunwa vya kutosha kv vimbama...tulivaa kaptula mbili shule tukiziita 'dabali' ili mboko zisikolee...Jirani alikuwa anaweza kuomba chumvi,moto hata mafuta au unga akiishiwa sio siku hizi rate ya majungu na choyo imeongezeka...tulisave pesa manunuzi ni siku ya gulio...Rais akiwatembelea wote ni kukata matawi na kumngoja barabarani...Kodi ya maendeleo na ya Baiskeli zilisumbua sana...sukariguru,buruga zilinoga sana na kuokoa bajeti ya sukari...kiswahili hakikuharibiwa kama hivi leo...Daaah nitaendelea
 
mabasi yalikuwa yanaondoka Moshi saa 10 au 11 jioni na kufika Dar saa 2 asubuhi, njia mbovu mpaka dereva anatumia gea namba 1 au 2, keria iko juu. Enzi hizo mabasi yalikuwepo OTC linapiga ruti Nairobi - Dsm, Kibo Bus, Lang'ata Bus, Ngorika. Kwa taarifa, kampuni ya mabasi ya Ngorika ndiyo kampuni ya zamani kuliko zote iliyobaki njia ya Arusha - Moshi - Dsm.
 
Mkuu samahan ila mbna sjakuuluza ww.au huyo mr ni ndugu yako?

Bila ya samahani Mkuu hukutakiwa kuuliza hivyo kwa yeyote ni kama unapinga anachokiongea kitu ambacho ni kweli ila labda hukuwepo kipindi hicho na kama ulikuwepo basi ilikuwa mdogo sana. Pili usipende kujihakikishia kuwa huyu ke na huyu ni me ndio maana tunatumia 'mkuu' pole kwa kukukwaza
 
-Matibabu ilikuwa bure. Hospitali za binafsi hazikuwepo labda za misheni.
-Ukivaa chupi ilikuwa ni dili kubwa!
-Hakukuwa na skini taiti
-Viatu ilikuwa tunanunua Bora
-Nyumba 10 alikuwa anaheshimika kama hakimu. Ukigombana na mkeo anakwenda kushitaki na kulala kwa mjumbe
-Ukimwi ulikuwa hakuna zaidi ya kisonono na kaswende
-Wasichana wa kazi walikuwa bwerere siku hizi ni shida!
-Hakukuwa na magril kwenye milango na madirisha
-Nyerere alikuwa kama Mungu
-Kawawa alikuwa alionekana kama kichekesho kwa stori za "Kawawa funika kikombe"
-Tulifanywe tuamini kuwa Kambona ni adui wa nchi yetu na nyimbo tuliimba
-Wakati ule wanafunzi kwenda kufanya kazi za mwalimu nyumbani kwake ilikuwa ni heshima kubwa, sasa hivi ni kesi
-Mashairi ya "Karudi baba mmoja" na "Sizitaki mbichi hizi" yalikuwa kichwani kwa kila mwanafunzi
-Jioni zilikuwa ni nyakati za kupiga hadithi na vitendawili au michezo ya kujificha. Siku hizi ni kuangalia TV
Nitaendelea......

umetisha mkuu...!!!!
 
Back
Top Bottom