Kwenda sekondari ilikuwa ni heshima kwa jamii inayokuzunguka. Wakati wa kwenda shule husindikizwa na kundi la watu huku umesaidiwa sanduku. Tulipanda treni.
Tiketi tulitunza kwani nauli tulirejeshewa baada ya safari. Makonda wa treni (tt) walikuwa ni wahindi.
Mwl.alipohamishwa shule ilipikwa pilau, pia mashairi yaliimbwa.
Picha tulipiga studio tena baada ya kusevu kwa muda mrefu.... Tofauti na siku hizi ''selfie''.
Tulisikiliza RTD, kwa miziki idhaa ya biashara.
Range rover haikuruhusiwa ku paki benki. Peugeot 504 iliaminika ni gari ya wahuni/majambazi.
Namba za serikali ilikuwa stb, stc, std, stg. Za wahisani ilikuwa tx - plate number nyekundu.
Sikukuu ya saba saba ilifana sana kitaifa ilifanyika. Na mikoa mingine ilishiriki pia.
Vitabu madaftari shule za msingi ilikuwa bure. Daftari likijaa unapeleka kwa mwl.wa darasa anakupa jipya
ole wako karatasi zikutwe pungufu, viboko vilitawala mashuleni na nidhamu ilikuwepo pia.
Wanafunzi shule ya msingi baadhi walikuwa wananyoa ndevu.
Itaendelea.
MUENDELEZO.
Nyakati za sikukuu tulisheherekea pamoja...kama ni Eid hata wakristu walisheherekea na kama ni krismasi hata waislamu walisheherekea.
Cartoon katika gazeti alikuwa ni chakubanga...kwa yeyote aliyenunua gazeti alianza kucheki kibonzo cha chakubanga.....na mitaani utasikia,jamani kuna mtu ameona chakubanga ya leo
kwa aliyeona basi huwasimulia wenzake.
Picha za wacheza mpira katika magazeti zilikatwa vizuri na kubandikwa ukutani hasa kwenye vyumba vya vijana(picha ilikuwa black &white)...uzalendo huu leo hakuna watu ni Man U na chel..nini sijui.
Gazeti la Sani lilikuwa ni burudani tosha kwa enzi hizo,Lodi lofa ,Pimbi,kipepe,Ndumilakuwili.,,na mitaani baadhi ya watu walipewa majina haya.
Kulikuwa hakuna mauaji kama sasa hivi,kwa waliofanya ujambazi walijulikana kiurahisi na wengi walikuwa hawauwi,jiwe Fatuma lilihusika kuvunjia milango.
Ilikuwa nadra sana kwa vijana kufariki,na iwapo jambo hili likitokea basi wazee hukusanyika kwa pamoja na kujadili ''what went wrong''?
Viwanda vingi vilifanya kazi Kiltex,Mwatex,Morogoro shoes,pia kulikuwa na mafuta ya Mara ambayo yalikuwa yakiwekwa kwenye wali au kupikia chapati basi majirani woote watajua.
Kulikuwa na shirika la ndege la Afrika mashariki,liliheshimika sana,nakumbuka kulikuwa na dege kubwa la mizigo liliitwa ''Simba''...baada ya kutoka Dar,KIA na Nairobi basi moja kwa moja mpaka kwa malkia.
Kwa vijana waliobalehe siku ya kulamba papuchi hakuna gesti,biashara huishia katika vichaka,mashamba ya mahindi au mapagale..nyumba ambazo bado hazijakamilika kujengwa.
Kulikuwa hakuna UKIMWI watu walichomwa sindano na zilichemshwa kabla ya kuchoma wengine.
Hospitali ilikuwa bure kwa maana ya Bure kweli.Hutoi hata senti tano.Ingawa za kulipia zilikuwepo pia.
Senti hamsini iliitwa thumuni,sumni.
Kipindi maarufu cha mahoka redioni kilivutia wengi.Mahokaaaaaaa A A A.
Mida ya saa nane nane mchana kulikuwa na kipindi cha kuimba mashairi redioni...kilikuwa kinawaboa watu wengi sana,ila kwa sasa.....
Itaendelea........