Zaidi ya wanafunzi 200 waliokuwa China waanza safari ya kurejea nchini kwa usafiri wa ATCL

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,130
823
Kutokana na kupanda kwa nauli za ndege kulikotokana na janga la Corona, ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na Shirikisho la Watanzania waishio nchini humo (TASAFIC) wamefanikiwa kuandaa usafiri kwa wanafunzi na Watanzania wengine waliokuwa China kupitia Shirika la Ndege la Tanzania.

Wengi wa wanaorejea ni wale ambao wamehitimu elimu zao kutoka vyuo mbalimbali vya nchini China, na pia wangekuwa shakani na maisha ya nchini humo kutokana na kuisha kwa hati zao za kuishi.

Safari ya kurudi nchini Tanzania imeanza muda mfupi uliopita, kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou (Baiyun International Airport) kwa ndege nambari TC 2402.

Tunawatakia Safari Njema, na kuwakaribisha katika nchi tuliyoishinda Corona.
 
Back
Top Bottom