Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,012
- 121,292
Ni zaidi ya mwezi sasa tokea yule rais wa TLS [read: CHADEMA], ambaye aliingia madarakani kwa kila aina ya mbwembwe, ambaye ushindi wake wa hicho cheo cha hicho kichama cha wanasheria baadhi ya watu waliushangilia utadhani ni ujio wa pili wa Yesu [wakati hakuna lolote], atangaze kuwa eti watampeleka mheshimiwa Paul Makonda mahakamani na kumfungulia mashitaka kadhaa mojawapo likiwa ni kudanganya kuhusu vyeti vyake.
Lakini mpaka sasa mimi [sijui nyie wengine] sijasikia hayo mashitaka yakifunguliwa kwenye mahakama yoyote hapa nchini.
Kama kawaida yao, kwa jinsi walivyo ni watu wa kudandia matukio, kwa sasa jambo linalobamba ni hili la makinikia. Hili nalo wamelidandia kwelikweli.
Si ajabu kabisa kama watakuwa washasahau kuwa walisema wataenda mahakamani kwenda kumshitaki mheshimiwa Makonda.
Sasa mimi sidhani kabisa kama hata wakienda mahakamani, hiyo kesi yao itafanikiwa. Kama wakienda basi itakuwa ni kesi ambayo tayari ni mfu [dead on arrival].
Mwezi mzima ushapita tokea watamke rasmi kuwa wataenda mahakamani...mbona mpaka sasa hawajaenda?
Nyie makaka na wadada wasomi, inachukua muda gani kumfungulia mashitaka mtu kama kweli ushahidi upo?
Au yalikuwa ni makelele ya kasuku na chiriku tu?
Hebu mwoneni hapa huyo Tundu Lissu akisema wataenda mahakamani...