Zabuni za ununuzi wa ndege hutangazwa wapi?

Zabuni za ununuzi wa ndege hutangazwa wapi?

Hivi ununuzi wa ndege mbili aina ya Bombadier ulifanywa kwa kutumia utaratibu wa kutangaza tender?

Ununuzi wa ndege tatu/nne zilizobaki nao utafanywa bila tender kutangazwa?

Manunuzi ya umma yamewekewa utaratibu wa kutumia tender ambapo kampuni inayoshinda ndio inapewa kazi au jukumu la kufanya manunuzi kwa niaba ya serikali.

Sasa wadau kwenye ununuzi wa ndege hizi,utaratibu huu unafuatwa na kama haufatwi, inatosha tu sisi kuridhika na kuamimi kuwa kila kitu kiko sawa?

Kwanini makampuni ya utengenezaji wa ndege hizi yasishindanishwe kwa uwazi?

Yetu macho na masikio.
Mbona unauliza huku umekata tamaa? [emoji12] [emoji13]

Ni kwamba ngosha ni mhimili uliojichimbia zaidi ya mingine miwili! Hivyo yeye ndiye procurement officer, ye ndio tender board, ye ndio kila kitu
 
Watanzania kweli sisi malofa
Hivi lini tutaacha kukosoa aisee
Tulipokuwa hatuna ndege mlikuwa mnalalamika
Leo tumepata mh Rais anayenunua ndege
Bado mnakosoa
Huo ni ufala
Tumsupport mh Rais
Ni hatua kubwa na ya kujivunia
Msapoti wewe na mama yako, ukute hujapanda hata ndege
 
Asante baba. Kweli wakosoaji wanakuudhi, mpaka umeongea Kiingereza kuonesha msisitizo.

Pogba kaamua kuanza upya anadai palichafuka sasa anasafisha asiulizwe anatumia sabuni gani wala ni usafi wa aina gani unafanyika, wengine watawanyike kukimbizana mikoani yeye ataendesha nchi.

Anaulizia taratibu,kanuni na sheria za manunuzi Ya Mali Za umma zilifuatwa. Kakosea wapi? Hapa anahitaji Kujua tu kanuni na sheria za manunuzi kama zilifuatwa. Kama huna elimu pana kwenye hilo just shut up.

Hapa ndiyo unadhihirisha ujinga wako na wa boss wako.

Hat

Hatujapinga kununua ndege mkuu..mtoa mada anauliza taratibu zilifuatwa!??kesho ukisikia ilikua dili unataka tuanzie wapi!?ndege zinunuliwe ...treni n.k lkn kwa taratibu..

Ndege zinanunuliwa moja kwa moja kiwandani.
Vibaraka wa ufisadi mtapata shida sana awamu hii waambie wanaokutuma hakuna 10% kama mlivyozoea.

Akiondoka huyu tutapitia kama taratibu zote za manunuzi kama zilifuatwa you just wait n ull see

Kipekee, pamoja na nia njema, ila suala la manunuzi kwa njia ya tender ambayo iko wazi isiyo na kamisheni,mimi binafsi naona lina manufaa makubwa. Walioanzisha sheria ile ya kufuata manunuz ya Umma najua walifanya utafiti na kujiridhisha umuhimu wake. Hvyo kama kuna mapungufu katika usimamiz yaboreshwe na pia kuwe na usimamiz wa man to man, lakini tendering process ndiyo msingi wa vitu vya umma.

Kama utakua umemuelewa mtoa mada hajabeza chochote! Hiyo sheria ipo au haipo?

Ha ha ha, swali la kipuuzi hupata jibu la kipuuzi. Ulitaka jibu gani kwani?

Hivi BRN bado ipo Magogoni au ilirudi Msoga?

richmond walitumia mfumo gani?

Marekebisho katika sheria mpya ya manunuzi yanaruhusu serikali kununua bidhaa moja kwa moja toka kwa mzalishaji. Watu inabidi waelewe kuwa sheria ya manunuzi inayotumika sasa ni ya 2016 ambayo inaruhusu ofisi ya serikali kununua bidhaa moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji. Watu wasikariri ile ya 2011, sasa tunayo mpya ya 2016

"Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri
ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya
kupata thamani ya fedha na ubora wa juu,
imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma
mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji,
au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa
kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoa huduma."

www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/11188-sheria-ya-manunuzi-yaua-upigaji-dili

Mkuu,

Bila kujali wala kuzingatia misimamo na itikadi zetu za vyama, jambo lolote linalofanywa bila kufuatwa taratibu, sheria na kanuni, hata liwe zuri/jema kiasi gani, halihalalishi upatikanaji/ufanyikaji wake.

Kaka ...
 
WANACHOFANYA WANANGALIA AINA ZA NDEGE WANAZOZIITAJI

WANACHAGUA KAMPUNI TATU

WANAANGALIA NA UIMARA PIA NA HISTORIA YA NDEGE ZA HIO KAMPUNJ

KAMPUNI ITAKAYOLETA ZABUNI BORA KABLAYA KUCHAGULIWA WANAKAA MAJOPO WA NDEGE HAPANCHINI WANAJADILIANA NA KUAMUA HII

ELSE BEI NAZO ZINAMATA PIA.... SOMKI
 
Nadhani katika awamu zote zilizopita huu ndo utawala ulioongoza kwa kuvunja katiba na sheria za nchi for Good.
 
Wanaangalia vingi kuchagua

Beii najinsiyamalipo nayoo inachangia kuteuliwa
 
Hivi ununuzi wa ndege mbili aina ya Bombadier ulifanywa kwa kutumia utaratibu wa kutangaza tender?

Ununuzi wa ndege tatu/nne zilizobaki nao utafanywa bila tender kutangazwa?

Manunuzi ya umma yamewekewa utaratibu wa kutumia tender ambapo kampuni inayoshinda ndio inapewa kazi au jukumu la kufanya manunuzi kwa niaba ya serikali.

Sasa wadau kwenye ununuzi wa ndege hizi,utaratibu huu unafuatwa na kama haufatwi, inatosha tu sisi kuridhika na kuamimi kuwa kila kitu kiko sawa?

Kwanini makampuni ya utengenezaji wa ndege hizi yasishindanishwe kwa uwazi?

Yetu macho na masikio.
Hivi mbowe alishalipa deni lake la NHC na la Twiga bank?
 
ZA MENDOKASI ULIJUAWALIPATAJE

ZILE RADAR AIRPORT

ZILE ZA SARE ZA...... ULIJUA WALIPATAJE
 
Marekebisho katika sheria mpya ya manunuzi yanaruhusu serikali kununua bidhaa moja kwa moja toka kwa mzalishaji. Watu inabidi waelewe kuwa sheria ya manunuzi inayotumika sasa ni ya 2016 ambayo inaruhusu ofisi ya serikali kununua bidhaa moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji. Watu wasikariri ile ya 2011, sasa tunayo mpya ya 2016

"Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri
ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya
kupata thamani ya fedha na ubora wa juu,
imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma
mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji,
au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa
kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoa huduma."

www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/11188-sheria-ya-manunuzi-yaua-upigaji-dili
Unadhani nyumbu wa Mbowe wanaelewa hayo basi? Kuwaelewesha nyumbu wa mbowe ni sawa kumpigia muziki kiziwiiiii !
 
Hivi ununuzi wa ndege mbili aina ya Bombadier ulifanywa kwa kutumia utaratibu wa kutangaza tender?

Ununuzi wa ndege tatu/nne zilizobaki nao utafanywa bila tender kutangazwa?

Manunuzi ya umma yamewekewa utaratibu wa kutumia tender ambapo kampuni inayoshinda ndio inapewa kazi au jukumu la kufanya manunuzi kwa niaba ya serikali.

Sasa wadau kwenye ununuzi wa ndege hizi,utaratibu huu unafuatwa na kama haufatwi, inatosha tu sisi kuridhika na kuamimi kuwa kila kitu kiko sawa?

Kwanini makampuni ya utengenezaji wa ndege hizi yasishindanishwe kwa uwazi?

Yetu macho na masikio.
Mkuu usikariri kuwa manunuzi lazima tender
Nakushauri toka kwenye mitandao kama nusu saa halafu pitia sheria yote na utaratibu uliotumika
Kazi yenu ni kupinga tu hamtaki kufanya research,ipo siku mtapinga hata uwepo wenu hapa duniani
 
Soma jinsi Magufuli alivyotetea ununuzi wa hiki kivuko:

MV Dar es Salaam kufa kabla ya kuanza kazi?

Time will tell.
 
Bombardier mtengenezaji ni mmoja tu na yuko canada .. kwa spea za ndege kuna vifaa vingine wewe kama operator (ATCL) lazima wakupe ambavyo vinabadilishwa kutokana na Miles ndege imeruka... na zile main Parts kama engine au sijui vioo nk hivi kuna center wanazo within mabara tofauti ili kusaidia suppy pale inapohitajika... kinachofanyika tu ni lazima MOU kati ya Operator and Manufacture...
 
Hivi ununuzi wa ndege mbili aina ya Bombadier ulifanywa kwa kutumia utaratibu wa kutangaza tender?

Mkuu, ulishasema kununua Bombadier - basi huhitaji tenda tena, unaenda kiwandani. Sawa na kununua Boeing au Airbus, hutangazi tenda unawafuata watengenezaji. Labda kama unataka used (iliyotumika) ndio utatoa tenda watu waje na ndege zao za miaka ya 47 wamezipaka rangi zinang'aa na Tanzania mnavyokimbilia vitu vya kung'aa mtalizwa tu!

Kutangaza tenda ni pale unapokuwa na multiple sources za similar products, na yaani kama bombardier ingekuwa ni generic name ya ndege zinazotengenezwa na kampuni nyingi tofauti.

Halafu watu kama Airbus na Boeing kwa kweli kwa ndege fulani wako kwenye kitu kinaitwa seller's market - hawana shida na order ya ndege moja toka Tanzania. In fact mara nyngine inabidi uwabembeleze. Fikiria Emirates wanaagiza ndege 15 za Airbus 350, na wewe unataka moja Airbus 119, watakuambia subiri utaipata ndege yako baada ya miaka 5! Tatizo hizi kampuni zinatengeneza ndege kwa order, sio kwamba zipo stoo zinasubiri wateja!
 
Kuna njia ngapi za manunuzi ya umma mbali ya tender unazozifahamu...???
Ningekushauri uwe unafanya literature review kabla ya kukimbilia jamiiforum na ungumbalu wako..
Mwekee hizo njia ili na sisi tusiozijua tuelimike. Ukimwuliza swali hatoweza kujibu na unapoteza nguvu. Naomba utuwekee hizo njia hapa tafadhali.
 
Single source unaijua? Ulitaka kununua Toyota si unajua? Kuna muuzaji mmoja tu anayezalisha gari za Toyota duniani ambaye ni Toyota .Ulitaka watu wengi walete quotation za nini wakati si wazalishaji wa Toyota? Hao watakuwa mawakala tu wanaotaka commission unanunua kiwandani moja kwa moja.Ulitaka ndege za bombardier au Boeing zinazalishwa na mmoja tu duniani huwezi taka wengi walete tends watakuwa madalali tu wanaotaka kukukalia wapige cha juu kama commission nk .Inaonyesha upeo wako wa sheria za manunuzi Mdogo mno
Ndege ni bomberdia tu au boing pekee yake acha ushamba, tuna sheria na taratibu zimebadirika?
 
Back
Top Bottom