Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,327
- 24,209
Nakumbuka wale wafanya biashara, tena watanzania pale Tunduma.Sio Manji pekee Wafanyabiashara wengi wamekimbilia Zambia,Uzuri wa Zambia ukiwalipa kodi hawakusumbui tena na hawana EFD wala ujinga wa risiti na ndio Nchi ambayo mizigo mingi inaingia kutoka SA na China kupitia Durban maana Tanzania walikimbia baada ya kuwekewa VAT kwenye transit goods sasa imefutwa wao washazoea tena SA...bandari zipo nyingi mnaleta usumbufu watu wanaangalia kwenye unafuu tu..
Baada ya kusumbuliwa na TRA muda mrefu wakasema uzalendo siyo dili kwa usumbufu wanaoupata, na wakahamia Nakonde Zambia.
Zambia wakawakaribisha kwa kodi stahiki kiduchu, na hawajarudi hadi leo.