fredmlay
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,849
- 391
Kwa ujumla EL sio tatizo kwangu, hata watanzania mpaka sasa wanachanganyikiwa hivi kweli Richmond ni yeye au Jk, maana JK alipaswa kumkataa na hoja zake wakati wa vikao vyao Dodoma, lakini Jk alinyamaza kuonyesha anakubaliana na alilosema EL, shida yangu kubwa ni ccm na mfumo wake wa kifisadi, hakuna namna unayoweza kumtenga mwana ccm na mfumo fisadi, hata leo akapewa Mwakyembe, Sitta nk watakumbwa na mfumo fisadi ndani ya ccm, njia pekee ya kuepuka hilo ni kuikataa ccm kwa kura ili tubadili mfumo fisadi uliokolea Tanzania.