Japo simkumbuki Kaemba lakini Udsm ya 2006-2010 ilikuwa balaa tupu kila semista lazima mgomo na maandamano na kila mwaka chuo kufungwa... peoplez kama Mtatiro(PM), Deo Daud (rais), Odong, Bush, Dady Igogo, Owawa, Silinde, Aristotle, n.k ziliyumbisha utawala wa chuo na serikali. karibu kila mwanachuo alikuwa mwanaharakati naikumbuka Red guard ya Mtatiro nikiwa first year tulifanya makubwa ya kuwatia mboko students na malekchara wapinga migomo. katika uwepo wangu udsm chuo kilifungwa mara 2 sababu ya migomo tukarudishwa nyumban 2007 na 2008. saa hizi sijui matatizo yameisha chuoni au wanafunzi radicals ndo wameisha??