Yupo wapi kada maarufu wa CCM Nicodemus Banduka

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,598
3,671
Naomba kufahamishwa alipo ndugu Nikodemus Banduka kada wa CCM. Shupavu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa miaka ya nyuma ila amepotezwa ghafla.
 
Jamaa hakupotezwa. Amestaafu anakula matunda ya utumishi wake. Jamaa aliona uzushi kujihusisha na utawala wa magamba!
 
Jamaa hakupotezwa. Amestaafu anakula matunda ya utumishi wake. Jamaa aliona uzushi kujihusisha na utawala wa magamba!

Mmoja kati ya waliokuwa ma-RC wababe sana enzi zake.

Akiwa Ruvuma aliwahi kumfanyia njama mwandishi habari wa kujitegemea, Adam Mwaibabile Mwana (rip) na kumfunga jela. Hii ilikuwa ni baada ya kuyalipua sana mabomu ya RC huyu ndipo akamwekea nyara za serikali na kutuma askari kumkamata na baadaye mahakama kumfunga 4 yrs.

Hata mie sijui alipo!!
 
Mwita25 hizo dharau sasa lol!

Viongozi wababe mi nadhani ndo wanatakiwa katika nchi hii si viongozi wanaofanya mchezo na akili za watu na ofisi za umma na kujilimbikizia mali
 
Jamaa hakupotezwa. Amestaafu anakula matunda ya utumishi wake. Jamaa aliona uzushi kujihusisha na utawala wa magamba!

alipotwezwa na jk huyu! Jamaa ilikuwa hakum support jk huyu! Alikuwa kambi ya sumaye! Alijaribu kushawishi baadhi ya wakuu wa wilaya, kafa nao wote baada ya uchaguzi!
Kuna siku nilikutana nae pale NSSF, inaonekana alikuwa anafuatilia Pension ya kustaafu
 
Hivi hiyo ishu ya yeye na mwaibabile ilikuwaje? kisa nini? mwenye ishu zaidi atupe
 
Historia inaonyesha kuwa ukishndana na prof. Maghembe, akikushnda unapotea.
Alishindana na Maghembe 2000 kugombea ubunge wilaya ya Mwanga.
 
Banduka huyu alisababisha tunyang'anywe viwanja tulivyokuwa tumenunua kihalali pale Kibaha maili moja baada ya yeye kujihalalishia viwanja zaidi ya mia kwa jina lake, akiwa mkuu wa mkoa wa pwani. Serikali iliposhindwa kumnyang'anya ( kwa sababu ya mfumo wao wa kubebana ki magamba) ikaamua kuvifuta viwanja vyote. Baada ya juhudi kubwa na kuwatishia kuwapeleka mahakamai watu wa ardhi wakatupimia viwanja vingine kule mkoani karibu na makaburi ya air msae. alikuwa na tabia fulani za hovyo huyu.
 
Yupo Buigiri anajihusisha na ufugaji wa uduvi na dagaa wa maji chumvi. Amechoka mbaya kiasi kwamba pikipiki yake haina hata 'side mirrors'

ni mmoja wa wastaafu wa ccm mbona.... sasa wewe upo upande gani mkuu,mbona hueleweki kabisa au ni mtindio wa ubongo unakusumbua!!!! buigiri ya wapi tena kwanza?
 
Kwa wananchi wa kawaida, mnamkumbukaje Mhe. Nicodemus Banduka? Kama kiongozi bshupavu au kamanda mahiri anayeamnini katika ukomunisto
 
Umenikumbusha wakati akiwa Shy dah sitaki kumzungumzia alinitenda mbaya. Sitaki hata kumkumbuka


nasikia alipokuwa Pwani alijitakia ule msitu wa kupanda mnaouona mkipita pale.
KWa kuwa alikuwa adui wa waandishi wa habari, jamaa walimtundika akalazimika kuurudisha!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom