MASHANJARA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 379
- 499
Nakumbuka kwenye siasa za jimbo la Same ambapo marehemu Chediel Y Mgonja (RIP) alikuwa mshiriki (Mbunge kwa miaka mingi), Bwana Nicodemus Banduka alikuwa akizunguka kwa wananchi na mstari wa Biblia wa Ezekiel 7:7 kwa ajili ya kumwangusha Mgonja, ingawa hawakufanikiwa na lengo lao ovu kwa miaka mingi. Washirika wengine waliokuwa nyuma ya Banduka walikuwa Kisumo Peter, Cleopa Msuya, Mgaya wa Same Elephant Motel, Marehemu Samwel Mdee na Judge kiongozi Nassor Mzavas. Ilibidi Mzavas atumie njia ya Mahakama ya Rufaa Tanzania na hatimaye kumkomoa Mgonja. Anyway Banduka alishiriki siasa za chuki kuu kule Same.