Yupo wapi Jasusi Apson Mwang'onda

Apson,Juma Ighondu[kama sijakosea].Haya majina yalikuwa kwenye 'font fed' ya Mwanahalisi enzi zile Ulimboka anahamasisha yake. Siasa za watu wasiojulikana zikaasisiwa rasmi.Kweli tunaendelea kula chumvi.Mungu atuongezee muda mrefu zaidi wa kuishi.Ameeen
 

Unajuaje kama lengo la kuanzisha uzi huu ni kujulisha watu kilichomkumba Apson?
 

Mkuu natofautiana na wewe! Apson kukataliwa kwenda kutibiwa nje na rais kwako ilitakiwa iwe SIRI? Siri hii inaathiri au kuhatarisha vipi USALAMA WA TAIFA?

Mbona wamekataliwa wengi wakiwamo mawaziri wakuu wote wastaafu na wengine wa vyeo mbalimbali na haikuwa siri? Lakini itambulike kwamba kuvujisha siri kwa uchache wake (wenyewe wanaita leaking) ni moja ya njia ya kupata siri nyingine nzito. Makachero wengi hutumia njia hii, wewe utaona siri kumbe mtoaji anafanya kitu inaitwa fishing (chambo na ndoano). Ogopa siri zinazokosa nyama, zaweza kuwa mitego.
 
Eagle wing ni makao makuu ya kitengo, Mzena hospital ipo kijitonyama kwenye makazi ya watumishi wa kitengo.
 
Sio ajabu naye ni Mtu wa kitengo, hata barmaids wote hapo pia huenda wapo kazini.
 
Yupo kwake mkoani Songwe mji wa Vwawa na kila siku kwake kuna misafara ya viongozi wakuu wakiingia na kutoka kwake.....
 
Huyo mzee mwacheni apumzike kustaafu yupo nyumbani acheni kumsumbua humu mitandaoni
 
Yupo kwake mkoani Songwe mji wa Vwawa na kila siku kwake kuna misafara ya viongozi wakuu wakiingia na kutoka kwake.....
Mwacheni mzee wa watu apumzike kijijini kwani ni mda wake wa kukaa kulea wajukuu
 
Huyo ni mtoto wake,Mbeya wamemkataa ubunge zaidi ya Mara nne,sasa anaanza kumpenyeza mwanae Dr.Tulia.Wana mbeya kumbuka nyoka mdogo na mkubwa wote wana sumu.
Du mkuu umeandika kwa kujiamini kama kweli vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…