Yupo wapi "first lady"?

Yupo wapi "first lady"?

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,320
Ni kweli siku hazigandi. Katika awamu ya Tatu tulimwona Mama Anna Mkapa akizunguka huku na kule kwa mwamvuli wa "Fursa sawa kwa wote".

Hakuchi Hakuchi mwisho hucha, Muda ulipofika Mama Anna Mkapa akaondoka na Mama Salma Kikwete akashika usukani. Yeye kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake alizunguka huku na kule kwa mwamvuli wa WAMA. Lengo na nia ni kuwainua wanawake na kuchochea juhudi zao katika kujiletea maendeleo.

Awamu ya Tano imeingia kwa kishindo. Tofauti na awamu mbili za nyuma "First lady" wa awamu hii hajionyeshi kama ni mtu mwenye kupenda kuonekana. Hili lilijionyesha katika kampeni za uchaguzi lakini linadhidi kudhihirika kadri Muda unavyosonga.

Swali la kujiuliza "Yupo wapi First Lady"? Je, angali anajipanga kuona aifanyie nini jamii au atakuwa kimya kama wakati wa kampeni?
 
Yupo anapika huko si unajua kitengo cha mapishi ikulu kimefutwa
 
Yuko na Mme wake sijui unataka nn zaidi ya hapo
 
Wabongo bwana kipindi Cha EOTF baadaye WAMA mmepiga Kelele weweeeee Leo magu kafanya mlicho kitaka mana lalamika sasa mnataka niniiiii????
 
yule mama ni mlokole safi hawez kushiriki cheo cha wiz anajua first lady halali ni regina
 
wake za watu unawaulizia nini aisee kua na adabu kidogo.
 
yule mama ni mlokole safi hawez kushiriki cheo cha wiz anajua first lady halali ni regina

Acha unyumbu wewe,Regina aendelee kumvalisha mchunga ngombe wake pampers na muacheni Janety ale maisha yake ikulu.
 
Mwalimu(Madam) Janeth jamani mmmh!hata haonekani?
 
Back
Top Bottom