Wale ambao walipewa kazi ya kumtetea wakati wa kampeni, walifanya kazi ya bure kabisa ya kumkashifu kabla hajapigwa chini CCM, waswahili wanasema mchawi mpe mwana amlee, ndicho alichokifanya Lowassa. Aliamua kwenda kujiunga na CHADEMA, chama ambacho kilitumia nguvu kubwa katika kumchafua kabla hajaamua kujiunga nacho. Naona unajaribu kuikwepa pointi yangu ambayo umei quate, tena kwa makusudi kabisa, Lowassa ni mmoja wa watuhumiwa wa mwembe yanga, sasa waliomtaja kama ni fisadi kule mwembe yanga ni wana CCM?. Kwanini hao hao ambao waliiambia public kwamba Lowassa ni mmoja wa watuhumiwa, wameshindwa kumsafisha kwa kutumia njia ile ile waliyotumia kumchafua?. Theatre ndogo inaanzia CHADEMA, kabla ya uongozi wa juu wa serikali haujaanza kutafuta mikasi na pamba ziko wapi.