Yuko wapi Tabasam Ngongoseko

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Nilikuwa nasikiliza radio. Hata hivyo bado nasikiliza. Ni ka kchibo kangu baada ya ngeleja kunitokea hadi muda huu akini haunt (kiswahili chake sijui ni kipi). Sasa nikamsikia mwana fa na wimbo wake wa miaka hiyoo wa mabinti. Fikra zikarudi nyuma nikamkumbuka huyu mrembo wa enzi hizo-Tabasamu. Alishiriki karibu mashindano yote yaliyoitwa ya urembo. Kipindi hicho niko Moshi, bwana mdogo, nikimsoma tu magazetini. Nakumbuka alikuwa mzurii halafu black beauty. Yupo huyu mrembo wa enzi hizo?
 
Ulishawahi kumsikia Lucy kihwele wa multichoice?ndie Tabasamu alibadili jina i dont know lakini hizi ni taarifa kwa mmoja wa watu wake wa karibu
 
Ni lucy kihwele yule alikuwa manager mahusiano something like that ndio Tabasamu ngongoseko....confirmed this day yuko kwenye bank moja town hapo.
 
Anaitwa Lucy Kihwele, zamani akijulikana kama Tabasamu Ngongoseko. NI mdada wa heshima sana kuliko mamiss wengi waliowahi kupitia fani hiyo. Ameshaondoka Multichoice baada ya kufanya kazi nzuri kuitangaza Tanzania na akahamia Standard Chartered Bank akaungana na Hoyce Temu katika Idara moja ya uhusiano pale, lakini Hoyce akapata shavu shirika moja la kimataifa hapa Dar idara ya uhusiano, so amemuacha Lucy Kihwele peke yake pale. Ni mchapakazi sana maana tangu aondoke Multichoice sasa kampuni hiyo inafifia taratibu na inaanza kutokusikika tena. Umeridhika mkuu au una maswali zaidi??
 
Duh! Kumbe ni lucy? From Tabasamu to Lucy dah! Nashukuruni kwa taarifa hizo
 
Anaitwa Lucy Kihwele, zamani akijulikana kama Tabasamu Ngongoseko. NI mdada wa heshima sana kuliko mamiss wengi waliowahi kupitia fani hiyo. Ameshaondoka Multichoice baada ya kufanya kazi nzuri kuitangaza Tanzania na akahamia Standard Chartered Bank akaungana na Hoyce Temu katika Idara moja ya uhusiano pale, lakini Hoyce akapata shavu shirika moja la kimataifa hapa Dar idara ya uhusiano, so amemuacha Lucy Kihwele peke yake pale. Ni mchapakazi sana maana tangu aondoke Multichoice sasa kampuni hiyo inafifia taratibu na inaanza kutokusikika tena. Umeridhika mkuu au una maswali zaidi??

Mkuu hata na mimi umenisaidia, maana jioni hii nilikuwa naulizana na office mate mwenzangu kuhusu huyu dada alipo (mara baada ya kumuona huyo sijui Bhoke kwenye press conference na mwanadada mwingine aliyejitambulisha kama Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania), maana hata jina lake la sasa tulikuwa tumelisahau!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom