Yuko wapi mwandishi Stanley Katabalo?

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,153
2,000
Wadau,

Nikiwa bado mdogo miaka ya Tisini kulikuwa na gazeti linaitwa Motomoto! Na jingine likiitwa Mfanyakazi. Kwenye kurasa za magazeti haya kulikuwa makala za mwandishi aliyekuwa akiitwa. Stanley Katabalo.

Je, kuna mtu ana habari za kutosha kuhusu mwandishi huyu?

Nawasilisha.
 
mwalidebe

JF-Expert Member
Mar 27, 2016
404
250
Kabla sijakudadavulia wewe binafsi umefikia wapi katika kufuatia kuhusu huyu mwandishi yaani hatua ambazo umeshachukua mpaka sasa.
 
Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,674
2,000
Kabla sijakudadavulia wewe binafsi umefikia wapi katika kufuatia kuhusu huyu mwandishi yaani hatua ambazo umeshachukua mpaka sasa.
Haya ni masharti ya kiganga kama kuna unalojua wewe sema ,hutaki watakuja wengine tu kutupa somo juu ya Stan hii ndio Jf
Nilicho sikia aliuwawa kwa sababu ya saga ya Loliondo
 
getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,153
2,000
Ki ukweli nimebakia na kumbukumbuku za mistari kadhaa tu ya makala zake nadhani kwa wakati huo nikikuwa darasa la tano. Hivyo sikuwa na jingine la ziada. Ila ni jina ambalo huwa halifutiki kabisa katika akili na kumbukumbu zangu natamani kufahamu zaidi kuhusu yeye.
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
7,287
2,000
Stan Katabalo ndie aliefichua uozo wa Loliondo kuuzwa kwa mkataba wa miaka mingi alichambua ule mkataba vizuri sana baada Wananchi kuelewa na kuanza kulipigia kekeke kilichotokea mbele ni sikumbuki..ni mmoja kati ya Waandishi bora waliowahi kutokea Tanzania...
 
getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,153
2,000
Duuh,!Kilichofanya nisiweze kumsahau ni mistari miwili au mitatu ya mwisho ya makala yake ya mwisho. Nanukuu.
"Najua nitakufa lakini..........!!!"
 
getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,153
2,000
Stan Katabalo ndie aliefichua uozo wa Loliondo kuuzwa kwa mkataba wa miaka mingi alichambua ule mkataba vizuri sana baada Wananchi kuelewa na kuanza kulipigia kekeke kilichotokea mbele ni sikumbuki..ni mmoja kati ya Waandishi bora waliowahi kutokea Tanzania...
Ahsante sana ndugu.!
 
isotaaaa

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,925
2,000
Wadau,

Nikiwa bado mdogo miaka ya Tisini kulikuwa na gazeti linaitwa Motomoto! Na jingine likiitwa Mfanyakazi. Kwenye kurasa za magazeti haya kulikuwa makala za mwandishi aliyekuwa akiitwa. Stanley Katabalo.

Je, kuna mtu ana habari za kutosha kuhusu mwandishi huyu?

Nawasilisha.
ama yuko wapi mtangazaji ezekiel malongo
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,814
2,000
Wadau,

Nikiwa bado mdogo miaka ya Tisini kulikuwa na gazeti linaitwa Motomoto! Na jingine likiitwa Mfanyakazi. Kwenye kurasa za magazeti haya kulikuwa makala za mwandishi aliyekuwa akiitwa. Stanley Katabalo.

Je, kuna mtu ana habari za kutosha kuhusu mwandishi huyu?

Nawasilisha.
Yuko wapi Ben
 
getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,153
2,000
Stan Katabalo ndie aliefichua uozo wa Loliondo kuuzwa kwa mkataba wa miaka mingi alichambua ule mkataba vizuri sana baada Wananchi kuelewa na kuanza kulipigia kekeke kilichotokea mbele ni sikumbuki..ni mmoja kati ya Waandishi bora waliowahi kutokea Tanzania...
Mkuu isanga nimeona uzi mwingine humu JF ukimhusu daah, anyway Mungu anajua Mengi zaidi ninaleta wazo kwa watu wa uandishi wa kiuchunguzi kuanzisha Tuzo ya Stanley Katabaro.!! Iwe ni tuzo ya heshima kwa mwandishi bora wa habari za kiuchunguzi...
RIP katabaro naamini tupo tunao kukumbuka japo tulikuwa wadogo jina lako halikuwahi kufutika katika kumbukumbu zetu,
Ipo siku tutakuenzi kwa heshima uliyostahili kuipata hata kama sio mimi naamini mwanangu atasoma uzi huu na kufufua nia na maono yangu.
Pumzika kwa Amani
Amen.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom