Msumbuko ni mwanasheria huyu.
Mara ya mwisho nimemkuta mahakama ya Kariakoo akitetea wezi wa kuku.
Kavaa koti linalomtosha mwanawe na miguuni makubadhi.
Wallah dunia tambara bovu!
Naikumbuka ile kesi akiwa NCCR alivyofanikiwa kumng'oa ubunge kupitia CCM, Bw. Kihiyo baada ya kumbana ataje japo classmate au mwalimu mmoja anaemkumbuka VETA alikodai kupitia.
Kumbe jamaa/mbunge alifoji vyeti, ndo hadi leo wafoji vyeti wanaitwa KIHIYO
Hongera Kipipi umesema kweli. Hakika ni Mwanasheria lakini busara za uongozi hana. Jambo dogo la mezani na wanafunzi yeye anakifunga chuo. Je mahakimu wangefanya hivyo kwa wateja wake ingekuwa vipi? Ni faculty dean lakini chuo hakina Maktaba. Hatumii elimu yake kuweka ubia na vyuo vingine ili hao watoto wa wakulima waende kujisomea ktk maktaba zenye vitabu vya sheria. Haiitaji PhD ilikujua hilo.
Alijitahidi sana kujipendekeza kwa JK wakati wa primaries za CCM hadi mkutano mkuu Dodoma. Kwa wale mlioona kwa Runinga siku JK anapitishwa rasmi kuwa mgombea wa CCM 2005, huyu jamaa aliweka PHD yake chini ya kubazi akaamua kujidhalilisha kwa kukimbia huko na huko ukumbini. Muda ule familia ya JK inatakiwa kupiga picha alihangaika sana kwenda huko na huko kuwakusanya watoto wa JK alikuwa kama yule mzungu Marius Weyers wa filamu ya Gods must be crazy.
Baada ya kuapishwa JK alikuwa na mpango wa kumkumbuka Lamwai, lakini wazee wa CCM Dar wakiongozwa na mzee Mwenyekiti wa Bodi Consultant wa shirika hilolo (only in TZ) ya serikali'' wakasema haiwezekani Lamwai apatiwe cheo ndani ya CCM kwasababu damage aliyofanya kwa CCM akiwa NCCR mageuzi haitakaa ifutike kamwe. JK akmafutilia mbali on similar grounds alizomfuti;ia mbali Twaha Ulimwengu
Huyu jamaa aliniudhi sana. Nilimpigia sana kampeni 1995 nikidhani ni mwana Ukombozi wa kweli. Nilitembea sana jimbo la Ubungo kutafuta kura na wala sikutaka hata senti kutoka kwake. Nilikuwa na imani kuwa anaweza kuwa chachu ya kuibadili Tanzania. Aliporudi kwenye magamba niliishiwa nguvu.
ya masumbuko lamwai ndio ya kina tambwe hiza, lamwai alidhan atapewa uwaziri akihamia ccm na pia tambwe hiza alidhan atapewa kugombea ubunge temeke, wote wako matopeni kabisa wakat nyota zao kisiasa zilikua zinawika!
Alikuwa noma km Lisu bungeni, wakambana sana.
Alitimuliwa kufundisha UDSM, kisha wakamzuia ku practice uwakili.
Njaa ikazidi, akarejea gambani na kupewa ubunge wa viti maalumu na Rais Mkapa.
Kuna kipindi nilisikia ni mwanasheria wa CCM.
Yumo kwenye kaburi la kitaaluma (academic grave) tangu alipohongwa ubunge wa dezo na hatimaye kupewa talaka. I used to like this guy. But when he started turning his knowledge into chap chap biz, I totally was fed up and pissed off. RIP Lamawai.