Young Dee akiri kutumia dawa za kulevya, aomba radhi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Rapper Young Dee hatimaye amethibitisha tetesi za miaka mingi kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya na kukiri kuwa ametumia kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

xYoung-Dee.jpg.pagespeed.ic.fmzrCLRK2Y.webp


Akiongea na waandishi wa habari leo, Escape One jijini Dar es Salaam, rapper huyo amewaomba radhi watanzania kwa vitendo hivyo na kuahidi kubadilika.

Amedai kuwa ni marafiki ndio waliompoteza na kumuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Amesema amepewa ushauri nasaha na wataalam na kwamba ameachana na matumizi hayo.

Pia rapper huyo amerejea rasmi kwenye uongozi wake wa zamani, Million Dollar Boyz, MDB alioachana nao mwaka jana.

x13398965_259931741052515_1071474077_n.jpg.pagespeed.ic.MuK75NZZMX.webp

Young Dee na meneja wake Max Rioba

Kwa muda mrefu rapper huyo alikuwa akikanusha tetesi hizo.
 
Kama amejitambua aache ila kama bado mwache aendelee mpaka yamfike yaliyowafika wengine. Hawa watu wakiambiwa hiyo kitu sio wala hawaelewagi
 
Aombe radhi kwa aliowah kuwakosea wakat akiwa kwenye stimu za unga na sio watanzania kwavle tu watanzania hatukumtuma akatumie madawa ya kulevya kwanza atuoneshe nan anayemuuzia
 
Hongera Young D, kujitambua kuwa umeathirika na madawa ya kulevya na kutaka msaada ni hatua ya kwanza ya kuacha matumizi yake!
 
Eti amewaomba radhi watanzania, aache kujipa ujiko sio wake, kwani bangi zake zina uhusiano gani inji hii?
namshangaa akawaombe wazazi wake waliohangaika tangu kusaka mimba yake mpaka kumfikisha alipoijua ngada akishafanya hivyo atapata baraka zote watanzania hatuna habare na wala ngada
 
Back
Top Bottom