Max Rioba adai ameshindwa kufanya kazi na Young Dee Kwa kuwa hana Nidhamu

Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,364
35,005
By Yasin Ngitu on January 7, 2017

Uongozi wa label ya Millian Dollar Boys ‘MDB’ iliokuwa unamsimamia rapper Young Dee, amedai hawafanyi tena kazi na rapper huyo kwa madai rapper huyo hana nidhamu.

Max Rioba ambaye ni mkurugenzi wa label hiyo, wiki moja iliyopita alionekana kulalamika katika mitandao ya kijamii akidai rapper huyo amerudi tena katika matumizi ya Madawa ya kulevya.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha FNL cha EATV, Max amedai habari za rapper kurudia matumizi ya Madawa ya kulevya na yeye anaziona katika mitandao ya kijamii kuhu akikiri kutofanya kazi tena na rapper huyo kwa madai ya kuwa hana nidhamu.

“Kwa sasa Young Dee hayupo tena kwangu,” alisema Max. “Sikumfukuza Young Dee kutoka kwangu, nilimwambia aondoke, kuna tofauti kati ya kumfukuza na kumwambia aondoke, sababu ni nidhamu.,”

Pia Max alidai kama rapper huyo atahitaji msaada wa pesa kutoka kwake ataendelea kumsaidia lakisi sio tena kuwa pamoja kama zamani.

“Young Dee akihitaji msaada wa kifedha nitamsaidia, hata binti aliyezaa naye akikwama kifedha mimi nitamsaidia, simchukii Young Dee,” alisema Max.
Katika hatua nyingine Max amedai kwa sasa hadhani kama atakuwa na nafasi tena ya kupokea msanii yeyote na kumsimamia.
d7f71cb03a731f8c70ce75436562c924.jpg

Source: Bongo5
 
Young Dee amerudia tena madawa hilo liko wazi.. Huyu dogo nilimfahamu vizuri sana kipindi yuko close na Chibu alikuwa anakuja sana sinza wcb..

And asipoangalia atafuata nyazo za chidi! Maana young dee msaada wake mkubwa hapa town ni Max.. Sasa stress za kukosa hela ma show za uhakia zinaweza kumfanya akaongeza matumizi ya madawa kupitiliza!
Ndicho kilichomponza Chidi pia.. Chidi alikuwa anatumia madawa kitambo tu, ile cocaine ya kusniff.. But alipoingia kwenye migogoro na media na umaarufu wake kuporomoka zile stress zilimfanya aongeze matumizi na tunaona matokeo yake..

Alafu hamjui kinacho mfanya max alie.! Ishu nzima iko hapa; Young Dee + tunda - max... Hapa ndipo kwenye kokoro!! Ila huyu tunda, she is a very bad influence.. Ukimuona mshakaji wako ana hangout na haka kamalay* hujue unampoteza mshkaji wako..
 
max alilia baada ya kuona investment aliyofanya inapotea.

jana amejikaza na akasema halii tena.
 
Back
Top Bottom