Young D: Sijakamatwa na polisi ila nilikuwa nashoot video ya wimbo wangu mpya

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,661
21,639

Msanii mdogo mwenye mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya muda mchache amekanusha habari zinazosambazwa na watu wasiompenda kwamba amekamatwa na poliisi. Akitolea maelezo suala hilo kutoka kwenye nyumba yake anayomiliki maeneo ya Sinza alidai kwamba hajakamatwa na mtu yeyote yule ila alikuwa akishoot video ya wimbo wake mpya unaoitwa "Jirani nitakuvunjia simu yako" ambapo director alishauri simu ivunjwe ili kuleta uhalisia ."Unajua director alikuwa too authentic,hata sisi ilibidi tuvunje simu ya jirani"

Pia Young D ametolea ufafanuzi suala la madawa kulevya na kusema yeye angekuwa anatumia madawa ya kulevya asingekuwa anafukuzana kwenye chati na Diamond na Wizkid hapa Afrika pia kuweza kumiliki mtoto mkali Afrika Mashariki .
 
Pia young D aliongezea kuwa wameamua kushoot video hiyo kwa kutumia camera ya simu ili kuleta kitu cha tofauti kwenye tasnia ya muziki duniani..
Kama kipi mkuu?sio kila MTU anajua.?!
 
Hongera Young D kwa kumiliki ghorofa na VX umeepuka ugomvi wa LUKU kwenye nyumba za kupanga.
 
Nyie ma young hamniwezi,mtazidi kupeng'a kisa stress mpaka totorooo........
 
Pia young D aliongezea kuwa wameamua kushoot video hiyo kwa kutumia camera ya simu ili kuleta kitu cha tofauti kwenye tasnia ya muziki duniani..
Dah mkuu umenifurahisha sana mpaka nimecheka kwa sauti kama mwehu vile.
 
Back
Top Bottom