Wakati mashabiki wa Simba wakiendelea kusherehekea sare ya bao 1-1 waliyopata Yanga dhidi ya Zesco United juzi, mabingwa hao wa kihistoria bado wataendelea kuwatesa watani zao hata ikitokea wameondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa
Mashabiki wa Simba wanaiombea Yanga 'dua baya' ili iondoshwe kwenye michuano ya Kimataifa baada ya timu yao kushindwa kupenya hatua ya awali wakitolewa na UD Songo
Baada ya kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga walijihakikishia tiketi mbili
Ya kwanza ni kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kama watapata matokeo ya ushindi Zambia
Lakini ya pili, kama wakitolewa na Zesco, watahamia kwenye michuano ya kombe la shirikisho
Utaratibu wa CAF uko hivi;
Timu 16 ambazo zitashinda raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, zitatinga hatua ya makundi
Nyingine 16 ambazo zitatolewa raundi hiyo, zitaungana na tmu 16 zilizofuzu raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho
Zitacheza raundi moja ya kusaka timu za kutinga makundi kombe la Shirikisho
Msimu wa 2015/16 Yanga walitolewa na Zanaco raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, wakapangwa na Sagrada Esperanca ya Angola hatua ya mtoano wa kufuzu makundi kombe la Shirikisho na wakatinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1
Wakarudia tena msimu wa 2017/18 kwa kutinga makundi kombe la Shirikisho kwa kuindosha Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa kuifunga mabao 2-1 baada ya kutolewa na Township Rollers kwenye ligi ya mabingwa
Hivyo hata kama watakosa nafasi ya kutinga makundi ligi ya mabingwa, wataendelea kubaki anga za Kimataifa wakisaka nafasi nyingine ya kutinga makundi kombe la Shirikisho