Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Klabu ya Yanga jana imemsainisha mkataba wa miaka miwili, beki wa kati raia wa Kongo, Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ambaye alikuwa kwenye majaribio katika timu hiyo kwa muda mrefu.
Usajili huo unakuja siku moja baada ya safu ya ulinzi ya Yanga kuruhusu bao la tano katika Ligi Kuu Bara jana wakilazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Usajili wa Kayembe unazima kabisa uwezekano wa beki Mtogo, Vincent Bossou kurejeshwa Jangwani, licha ya kupigiwa debe na wadau mbalimbali wa klabu hiyo, arejeshwe kikosini.
Inasadikika kuwa hali mbaya ya kiuchumi ilisababisha Yanga kutompa mkataba mpya Bossou, lakini kitendo cha klabu kumsajili Kayembe anayetokea Balende FC ya kwao, Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC) kinaashiria imeamua kuachana na Mtogo huyo moja kwa moja.
Kupitia ukurasa wao wa Instragram, Yanga wameandika ujumbe huu: “Fiston 'Festo' Kayembe Kanku amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na [HASHTAG]#mabingwamara27[/HASHTAG] @yangasc akitokea Balende Fc ya DR CONGO.
 
Kizuri tukiige umefika wakati sasa timu kuendeshwa kwa hisa ili iende kibiashara Zaidi
 
Yanga naipenda ila duh haitabiriki. All the best kubaki chamani.
Hahahaa. Pole sana rafiki. Huwa saa nyingine tunaumia ila ndio hivyo upenzi uko damuni.

"Daima mbele nyuma mwiko"

Mie nilikuwa nashabikia zamani EPL ila kwa sasa nishaacha mwaya.
 
IKIWAKOSA nyota wake watano muhimu kwenye kikosi cha kwanza, Yanga itajitupa uwanjani leo Jumapili kuikabili Mbao FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo ni muhimu kwa Yanga ambayo itataka kurudisha heshima yake baada ya kufungwa mara mbili katika msimu uliopita huku ikitoka sare mchezo mmoja. Miwili ilikuwa ligi na mmoja Kombe la FA.

Timu hizo, zinavaana katika Uwanja wa CCM Kirumba huku Yanga ikimkosa Kelvin Yondani, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma wenye majeraha, Ibrahim Ajibu mwenye kadi tatu za njano na Obrey Chirwa ambaye alisusa akaenda kwao Zambia.

Lakini Yanga ambayo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa kutokana na George Lwandamina kufiwa na mwanae, italazimika kutumia masha-mbulizi ya kushtukiza pamoja na kuweka ukuta mzito kutokana aina ya wachezaji ilionao.

Hiyo, ni kutokana pia na uimara wa kikosi cha Mbao kinachou-ndwa wachezaji wengi chipukizi wenye kasi wanao-cheza soka la pasi nyingi huku wakisha-mbulia kwa wakati mmoja.

Katika mazoezi ya mwisho, Nsajigwa alionekana akiwaandaa mabeki wa pembeni Juma Abdul akicheza namba mbili na Hassan Kessy ambaye ataanza kama ilivyo kwa Pius Buswita ambaye atatumika kama kiraka.

Wakati akiibadilisha safu ya ulinzi ya kulia, kocha huyo alionekana akimuandaa Gadiel Michael kucheza namba tatu huku Haji Mwinyi akipangwa namba kumi na moja akichukua nafasi ya Emmnauel Martin na lengo la kocha huyo kuona wachezaji wake wakicheza kwa kushambulia na kulinda goli lao ndani ya dakika 90 mchezo ili kuwapunguza kasi Mbao.

Wakati akiimarisha safu ya pembeni, katikati napo huenda kukawepo mabadiliko ambako beki mkongwe, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliondolewa na kumpisha Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye ni kijana mwenye kasi atakayeweza kuendana na kasi ya wachezaji hao vijana wa Mbao.

Safu ya kiungo wa kati, Papy Kabamba Tshishimbi ambaye tegemeo aliyerejea hivi karibuni akitoka kwenye majeraha ya enka yeye ataanza kucheza namba sita huku Raphael Daudi akicheza nane.

Na Buswita yeye ataingia kucheza namba kumi ambayo ametolewa na Kessy katika namba saba ambayo anaicheza tangu ajiunge na Yanga akitokea Mbao katika msimu huu na Yohana Nkomola atacheza namba tisa baada ya Mrundi, Amissi Tambwe kujitonesha goti lake mechi iliyopita ya Kombe la FA dhidi ya Reha FC iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0 kati ya hayo moja likifungwa yeye.

Akizungumzia mechi hiyo, Nsajigwa alisema kuwa “Malengo yetu ni kuchukua pointi muhimu zitakazotuweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi,ninaamini mechi itakuwa ngumu katika pande zote kwani kila timu imejiandaa, tutaingia uwanjani tukiwa na kisasi cha kufungwa mara mbili .
BEKI MBAO

Yusuph Ndikumana raia wa Burundi amekipiga mkwara kikosi cha Yanga; “Dakika 90 ndizo zitaamua nani ataibuka mshindi. Nimejipanga kuhakikisha naisaidia timu yangu, kuimarisha ukuta wetu ili kutowapa nafasi wapinzani kutufunga.”
 
happy-new-year-2018-gif+%282%29.gif
 
Back
Top Bottom