Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Baada ya mikia fc kuponea chupuchupu, leo tuko uwanja wa Namfua mkoani Singida kumenyana na Singida United. Wanayanga wenzangu tulioko majumbani na uwanjani msiwe na wasiwasi kila kitu kimeenda sawa na tayari uhakika upo 100% kua tunashinda mechi ya leo.
 
Dirisha dogo tufanyeni usajili jamani mana naona tuna mapengo ya winga zote mbili. Kwa upande wangu mchezaji kama Buswita na Mwashiuya sio wachezaji wa kua kikosi cha kwanza cha Yanga. Tukimpata Mo Banka wa mtibwa yule na winga za kulia nakushoto nzuri tutatisha sana.
 
STRAIKA wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa ameendelea 'kung'ara' katika Ligi Kuu Bara baada ya kufunga 'Hat -trick' yake ya kwanza msimu huu kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City, jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 
Chirwa, ambaye ni Mchezaji Bora wa Kigi Kuu kwa mwezi Oktoba, alifunga mabao hayo dakika ya 19, 49 na 59, wakati Emmanuel Martine alifunga mawili dakika ya 22 na 80 na kufanya matokeo kuwa 5-0.
 
Hiyo ni Hat-trick ya kwanza kwa Chirwa tangu aliposajiliwa na Yanga msimu uliopita na hat-trick ya pili msimu huu, ya kwanza ikifungwa na Emmanuel Okwi wa Simba.
 
Katika mchezo huo uliochezwa uwanjani hapo, Yanga walicheza kwa umakini na kupata matokeo hayo yanayowabakisha nafasi ya tatu na pointi 21, nyumba ya Simba inayoongoza na pointi 22 ambazo ni sawa na za Azam wanaoshika nafasi ya tatu.
 
Kikosi cha Yanga

1 Youth Rostand, 2 Juma Abdul, 3Gadiel Michael, 4 Andrew Vincent, 5Nadir Haroub 'Cannavaro', 6Pato Ngonyani, 7 Pius Buswita, 8Raphael Daud, 9Obrey Chirwa, 10Ibrahim Ajib/Geofrey Mwashiuya, 11Eammanuel Martine
 
Back
Top Bottom