You are not my type

Hapo shida ni pesa tu.. Akiwa hana pesa hawezi kuwa type yako ila akishanyaka maneno yanabadilika kutoka kanyaboya mpaka HONEY
 
Mushi unaabudu sana pesa eeh?
Tufanye assumption ndogo tu... Hivi unafikiri kwa mfano, ni wanawake wangapi wanaweza kutoa hiyo kauli kwa mtu mwenye pesa? - assume mtoto wa Mengi hapo halafu unamwambia wewe sio type yangu... unadhani ni kitu ambacho ni possible and practical???
 

🤣🤣🤣🤣 nakumbuka tulikua mahali jamaa akawa anavuta fegi, dada mmoja akamwambia kaka moshi huo...
jamaa alimshushia matusi akammalizia na “ukimwi unaukatikia mauno afu unanibania pua kaka moshiii (huku kabana pua)”, kila mtu alicheka aiseee

mtu kama huyu ukisema umjibu namna hii utafurahi na roho yako
 
Rejection ni rejection tu.
Sema kupunguza ukali wa maneno, mtu anaweza kukuambia kwamba nina mtu au hata akakuchana ukweli kwamba moyo wake hauna hisia na wewe.
Ila wewe sio wa type yangu imekaa kimatako matako sana.
 
Kichwa huongoza mwili, nacho huponzwa na ulimi, hauna ushuru mdomo so chunga ulimi usilete mgogoro - fid Q

Hayo majibu huwa wanajibiwa wale wanaume wasumbufu sana, wale wenye sifa sana Otherwise ni masela tu tunakuwa tunawatokea mademu wenye nature ya Dharau. Hio kauli ni Dharau 100%, hata ikisemwa kwa upole.
 
Hii ndio hali halisi yaani hakuna kingine ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya hali duni kwa mfano mimi Demu aliyenitamkia hivyo tuko marafiki kabisa na ni kama tunaelewana sana labda sababu ya umaskini wangu tuu japo nafanya kazi na ninalipwa tena kipato kizuri tu zaidi ya milion ila sidhani kama yeye anajua, inashangaza lakini ndio hivyo inaniuma sana kwa kweli. Nafanya kazi usiku na mchana nikimbiane na umaskini nije nimuoneshe yule manzi kwamba nilikua na ndoto kubwa sana na ndio maana nikampenda binti mrembo na mwenye akili nyingi kama yeye. Anyway ni mipango ya Mungu wakati mwingine ila inauma sana kukataliwa na mtu unayempenda sababu unakua na mipango lukuki kichwani sema ndio mwisho wa siku zote zinabaki kuwa ndoto zisizo kuwa na tumaini lolote.
 
Kuna Dada alijibu hivyo mimi sio type yake, nikamuangalia nikasema Hiii.
Akakutana na mjanja,akampa mimba,akazalia kwao,hajakaa vizuri mimba yapili MTU mwingine,mimi namuangalia tu nasema Hiii
Sasa hivi analia lia kuomba msamaha eti anaomba tuendeleee.mimi nimemjibu KWA Sasa haitowezekana.
 
Tufanye assumption ndogo tu... Hivi unafikiri kwa mfano, ni wanawake wangapi wanaweza kutoa hiyo kauli kwa mtu mwenye pesa? - assume mtoto wa Mengi hapo halafu unamwambia wewe sio type yangu... unadhani ni kitu ambacho ni possible and practical???
Haha sasa mtoto wa Mengi hata kama sio type yako si kuna cha kujipoozea
 
Mkuu hapo mwanzoni hauko sahihi kabisa, kwamba hakuna ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya umasikini? Sio kweli kabisa ingekuwa hivyo maskini wasingekuwa na wapenzi au ndoa
 
Kwani kuna haja ya kumweleza hayo maneno maisha yanazunguka kuna siku atakuwa type yako huwezi jua maisha haya. Kama humtaki mtu tumia neno la busara achana naye. Kwa mtazamo wangu
Jibu zuri sana
 
Mkuu hapo mwanzoni hauko sahihi kabisa, kwamba hakuna ambacho mwanamke anaweza kukukataa nacho zaidi ya umasikini? Sio kweli kabisa ingekuwa hivyo maskini wasingekuwa na wapenzi au ndoa
Masikini wanapata wapenzi kwasababu ya namba yao tu lakini hamna mwanamke anayependa mwanaume maskini.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…