Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Waliotoa dhamana wote wachunguzwe; huenda majina yana link na STEWARTS scandal na mengineyo tunayoyasikia
 
Hii tone imekaa kikabila vile.... wachagga na wameru tena wamekosa nini? Unajua mwingine anaweza kusema wakristo au walutheri au wakatoliki wamefurika mahakamani..... ili kuelezea watu waliofika mahakamani.

Nadhani hii sio sahihi kuwaita hao watanzania kwa ukabila wao.


Mkuu huu ni ukweli wa watu walio furika kuwawekea dhamana hawa watuhumiwa kama wangekuwa Wasukuma si tungesema!
Hapo inaonyesha watu hawatupani mkuu wamesimama kidete mpaka jamaa zao wametoka rumande na ndo hao walio pigania mpaka wakatolewa rumande lasivyo wange endela kusota.
 
Waliotoa dhamana wote wachunguzwe; huenda majina yana link na STEWARTS scandal na mengineyo tunayoyasikia

Kweli mkuu,
Naona kuna haja UWT uwachunguze kiundani hawa walio wadhamini watuhumiwa na waangaliwe kiundani kama kweli wanalilipa taifa kodi.
 
Nimepata Breaking news....... wameachiwa kwa dhamana dk 20 zilizopita
Wachagga na wameru wamefulika kwa wingi mahakamani wakichangishana kuhakikisha mzee anafaudu harusi ya mwanae kesho.

You better check your sources again. Masharti ya dhamana yamepunguzwa mpaka 2.9 billion, sasa hivi wanaweza wakaweka cash na malii zisizohamishika kama dhamana

Verification ya dhamana imechukuwa muda mrefu na muda wa mahakama ulikuwa umekwisha, wamerudishwa Keko mpaka Jumatatu.

​
Mkuu ni kweli kabisa saizi kama 30 zimepita jamaa wapo huru wanarudi kwao kujiliwaza na machungu ya Keko.
Mahakama iliaihirishwa asb na kuendelea na kazi mchana kwa hiyo wamewapunguzia masharti ndo maana wapo wamepewa dhamana.Alafu nusu ya bilioni 11 ilikuwa ni 2.9 kwa kila mmoja kama jamaa alivyo piga hesabu hapo juu.
Again, check your sources. Unapotosha watu.
​
 
Inafanyika wapi hiyo harusi? Watanzania tusingekuwa wastaarabu watu wange-gate crush. Aibu aibu!!!! Si wange-cancel tu? Itakuwa ngumu kumaintain plastic smiles mpaka shughuli iishe!! Waalikwa mtu-postie picha pse tusome body language
 


You better check your sources again. Masharti ya dhamana yamepunguzwa mpaka 2.9 billion, sasa hivi wanaweza wakaweka cash na malii zisizohamishika kama dhamana

Verification ya dhamana imechukuwa muda mrefu na muda wa mahakama ulikuwa umekwisha, wamerudishwa Keko mpaka Jumatatu.

​

​
Again, check your sources. Unapotosha watu.
​

Confused....mkuu wamerudi Keko?
 
Pls confirm this ili nitoke kidogo nje nikanye ka-fanta kangu maana sikutaka aharibu kabisa harusi ya watoto wake; niingependa watoto wanede ktk ndoa wakiwa wasafi hivyo hivyo; confirm niende kwa mgahawa hapa nje Kirumba
 
Pls confirm this ili nitoke kidogo nje nikanye ka-fanta kangu maana sikutaka aharibu kabisa harusi ya watoto wake; niingependa watoto wanede ktk ndoa wakiwa wasafi hivyo hivyo; confirm niende kwa mgahawa hapa nje Kirumba

Confirmed, Mramba karudi Keko.
​
 
Confirmed! Jamaa wamerudishwa KEKO! source iliopo pale KEKO imeweza authenticate hii. HABARI ndiyo hiyo!
 
OK; wajumbe; naenda kupata FANTA yangu; hilo ndilo nililiwekea LOGIC kweli limefanyika; so naenda kujipongeza kwa FANTA nje hapa; Good Mahakama ya Rufaa.
 
Kama kweli wamerudi keko... na weekend wakailia ndani...basi hii ngoma mbichi.

Wakati wakulu wakisota ndani weekend.., JK mwenyewe huyooo kapaaa tena.
 
mrambayona291108.jpg
Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona, wakitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwenda kupanda basi kurejea gerezani Keko baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ijumaa. (Picha na Bernard Rwebangira).

Imetolewa mara ya mwisho: 29.11.2008 0010 EAT

• Mramba akosa harusi ya bintiye
Majira


*Yeye Yona warudishwa gerezani
*Wapata ahueni, washindwa kuitumia

Na Grace Michael

SIKU ngumu zilizojaa kila aina ya majaribu katika maisha ya mawaziri wawili waandamizi wa zamani, Bw. Basil Mramba (Fedha) na Bw. Daniel Yona (Nishati na Madini), zimeendelea tena jana baada ya jitihada yao ya kupata dhamana kupitia Mahakama Kuu kugonga ukuta.

Mramba na Yona, wachumi katika moja ya taaluma zao, wote wakiwa viongozi waandamizi waliotumikia Serikali za awamu zote kwa nyadhifa tofauti lakini wanaotofautina kiumri kwa mwaka mmoja na siku 12 tu-Mramba: Mei 15,1940; Yona Mei 3, 1941, kwa hukumu hiyo wataendelea kuyakabili maisha ya upweke katika gereza hilo kufuatia kushitakiwa kwa makosa zaidi ya 10 yanayohusu kuliingizia taifa hasara ya mabilioni kutokana na tuhuma za uzembe walioufanya wakiwa kazini.

Kurejea gereza la Keko ni dhahiri kumewaumiza kisaikolojia wote wawili, kama ambavyo pia mawakili wao walivyobainisha katika hati za viapo walivyowasilisha Mahakamani, lakini kwa Mrambo hilo ni pigo lililompa huzuni kuu kwani nasaha zake za muhimu zitakosekana leo katika harusi ya bintiye, harusi iliyopangwa kufanyika Dar es Salaam.

Ndugu kutoka familia zote mbili, walijazana mahakama hapo jana kujaribu kuwafariji wapendwa wa ambao hata hivyo walioonekana muda wote wakiwa na tabasamu lililojaa ujumbe mzito.

Mtaalamu wa masuala ya saikolojia, hasa tafsiri za mienendo na mihemko ya mwili wa binadamnu, aliyezungumza na Majira jana, alisema hali hiyo inaweza kufasiriwa kuwa iliyoficha sikitiko kuu moyoni mwao kwani mwanadamu anahulka ya kucheka anapokuwa katikati ya shida na kulia anapokuwa katikati ya furaha.

Awali upande wa waombaji ulioongozwa na wakili Bw. Joseph Thadayo uliiomba mahakama kuangalia upya kifungu cha 148 5 (e) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka (CPA) ambacho kinamtaka mshitakiwa kuweka nusu ya fedha zilizotajwa katika hati ya mashitaka kama ilivyotolewa hukumu na Mahakama ya Kisutu ambapo alisema kitafsiri fungu hilo linaruhusu pia kuwekwa mali yenye thamani husika na si fedha taslimu pekee.

Mbali na ombi hilo pia aliiomba mahakama kutowazuia washitakiwa hao kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kuwa na majukumu ya kitaifa na kimataifa na hasa Bw. Mramba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rombo ili aweze kwenda jimboni kwake na katika shughuli za Bunge mjini Dodoma.

"Wanayo majukumu makubwa ya kuwatumikia wananchi wake na kusimamia mambo mbalimbali kwa wananchi hao hivyo kubaki Dar es Salaam peke yake si kuwatendea haki wananchi wa jimbo hilo," alisema wakili Thadao akipinga sharti hilo lililowekwa na Hakimu Hezron Mwankenja wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akijibu hoja hizo Mwanasheria wa Serikali Bw. Fredrick Manyanda alisema kuwa hana pingamizi na ombi la kuweka hati ya mali isiyohamishika kama mbadala wa fedha taslimu kutokana na suala hilo kuwa wazi kisheria.

Kwa upande wa ombi la kuruhusiwa kwa washitakiwa hao kwenda nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, alipingana nalo kwa kusema kuwa sheria iko wazi inazuia mshitakiwa kutoka nje ya mkoa anaotakiwa kuwemo ila tu anaweza kufanya hivyo kwa kibali maalum cha mahakama.

"Watu wote wako sawa chini ya sheria na haibagui mtu yoyote hivyo napingana na ombi hili," alisema Bw. Manyanda.

Baada ya malumbano ya kisheria ya pande zote mbili Jaji Mwaikugile aliahirisha kesi hiyo kwa muda hadi saa saba mchana ambapo alitoa hukumu iliyokubaliana na ombi la washitakiwa hao la kuweka nusu ya fedha au hati ya mali isiyohamishika.

Alisema kuwa ombi hilo amekubaliana nalo kutokana na kuwa wazi kisheria lakini pia upande wa Serikali haukuwa na pingamizi juu ya suala hilo na kwa upande wa ombi la kutoka nje ya mkoa, alisema kuwa sharti hilo litabaki kama lilivyo kwani sheria inawaruhusu watuhumiwa kuomba kibali muda wowote watakapotaka kusafiri iwapo wana sababu za msingi.

Baada ya hayo washitakiwa waliwasilisha hati za nyaraka mbalimbali za mali zao ili kutimiza masharti hayo ambapo uhakiki ulifanyika kwa Msajili wa Mahakama hiyo, Bw. Lameck Mlache ambako hata hivyo mambo yalionekana kuwa magumu kadiri muda ulivyokuwa ukienda na matarajio ya watuhumiwa hao kurejea uraiani jana yakizidi kutoweka.

Uhakiki huo ulichukua muda mrefu huku pande zote mbili zikionekana kulumbana kuhusiana na hati za mali ambazo zilikuwa zimewasilishwa hali iliyowafanya mawakili wa pande zote mbili kuingia mara tatu kwa Msajili.

Baada ya zoezi hilo kushindikana Msajili aliwaambia waandishi wa habari kuwa washitakiwa hao watarudi rumande hadi Jumatatu ambapo zoezi la uhakiki litafanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

"Zoezi hili limekuwa gumu kidogo hivyo litafanywa siku ya Jumatatu katika Mahakama ya Kisutu," alisema Bw. Mlacha bila kufafanua zaidi.

Kushindwa kutimiza masharti hayo si tu kulionekana dhahiri kuwaachia simanzi watuhumiwa wenyewe bali pia tabasamu walilokuwa nalo ndugu, jamaa na marafi wa washitakiwa lilipotea ghafla na walionekana kuwa na huzuni wakiwashuhudia ndugu zao hao wakipanda karandiga kurudi katika gereza la Keko.

Mramba, Yona: Walikotoka

Mramba

*Kuzaliwa

Mei 15, 1940

Elimu Msingi

-Kwaleina Bush 1948-1949
-Shimbi 1951-1952
-Misheni Mkuu 1953-1954

*Sekondari

-Umbwe 1955-1960
-Sekondari ya Wavulana Tabora (A-Level) 1961-1962.

*Elimu ya Juu

-Chuo Kikuu cha Makerere-Kampala BA. (Political) 1963-1967
-Chuo Kikuu cha City-London, MBA 1967-1968
-Shule ya Biashara, Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani (cheti katika Usimamizi wa Biashara) 1971.

*Nyadhifa alizoshika

Utawala wa Awamu ya Kwanza

-Mtawala Msaidizi Williamson Diamond Mwadui 1964-1969
-Mkurugenzi Uendelezaji Raslimali watu, Shirika la Maendeleo
la Taifa (NDC) 1969-1972
-Mkurugenzi Mtendaji SIDO 1973-1980
-Mbunge 1980

Awamu ya Pili

-Mbunge 1985-1995

Awamu ya Tatu

-Mkuu wa Mkoa wa Mbeya 1995.
Waziri wa Viwanda na Biashara 1995-2000
-Waziri wa Fedha 2000-2005

Awamu ya Tatu

-Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko 10/17/2006 hadi 2/8/2008
-Waziri wa Miundombinu 1/1/2006 hadi 10/16/2006

Daniel Yona

*Kuzaliwa:

-Mei 3, 1941

*Elimu Msingi

-Bendera 1948-1950
-Kihurio 1951-1953

*Elimu Sekondari

-Minaki 1954-1959

*Elimu ya Juu

-Chuo Kikuu cha Strathclyde (Glasgow, Uskochi), BA. (Economics) 1960-1964
-Chuo cha Biashara (cheti) -1965.
-Chuo Kikuu cha Havard, Marekani (cheti) 1977.

*Nyadhifa alizoshika

Awamu ya Kwanza

-Mchumi Baraza la Fedha la Afrika Mashariki 1964-1965
-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Mchumi 1966-1971
-Mkurugenzi Mtendaji, Benki ya Nyumba (THB), 1972-1977
-Mkuu wa Chuo (IFM)-DSM 1978-1980
-Mkurugenzi Mwendeshaji Shirika la Nyumba la Sierra Leone 1983-1986

Awamu ya Pili

-Mshauri Shirika la Nyumba kwenye Visiwa vya Vanuatu 1990-1992

Awamu ya Tatu

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais. Mipango 1995-1996
-Waziri wa Fedha 1996-2000
-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais 2000-2002
-Waziri wa Nishati na Madini 2002-2005.
 
Hivi bado muheshimiwa raisi anampango wa kulihutubia Taifa mwisho wa mwezi???? Mwisho wa mwezi huu lazima nikakinunulie betri kiredio mbao changu nimsikilize, maana inaweza kuwa balaa, Wananchi raisi amekasirika jamani...?
Bila ya kusahau napenda kuwapa BigUp wale waliokuja na idea ya kumrushia mawe raisi kule Mbeya, kwani inasemekana kitendo kile kilimkera sana ndipo akaona kweli anatatizo mezani kwake.
Sisi na vyombo vyetu vyoote vya kisasa, tarakilishi, mitandao, redio, maluninga, blogu, forums, na kede wa kede, zilikuwa ni kelele za fisi tu hazikumuogopesha simba kunywa maji. Lakini mawe ya kijijini mbeya, ndio yanaanza kufukua vyoote hivi.
Sasa napata Idea kwa nini Palestina mawe ni silaha yao kuu......
 
mrambayona291108.jpg
Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona, wakitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwenda kupanda basi kurejea gerezani Keko baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ijumaa. (Picha na Bernard Rwebangira).

Itabidi Mkapa ndio akawe baba wa mtoto wa Mramba kwenye harusi, kama ambavyo alikuwa baba wa mtoto wa kwanza wa Mramba kwenye Maisha.

You couldn't write a better script for a best seller!

Nasubiri kuona kama Kikwete nae ataenda kula pilau.

Kikwete akienda harusini na msafara wa administration yake maana yake ana send a very strong message across the breath of government institutions kwamba ana sympathize na Mramba. So, magistrates and judges watch out!

Mwinyi na Warioba na Pinda na Malecela na maswahiba wa Mramba toka uhuru na Mawaziri na wabunge wengine wengine, na yeyote anaepigia kelele ufisadi akitokea kumuoza mtoto wa Mramba ina maana mnafiki - haelewi the symbolic meaning ya kuto ji-distance na mshutumiwa wizi!!

You blink, you miss the show. The title of the play: "Mockery of Justice!"
 
Back
Top Bottom