Yemenikuta Mwenzenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yemenikuta Mwenzenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sweetdada, Aug 24, 2012.

 1. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  yamenikuta mwenzenu.

  Ilikuwa ni siku ya jumatano saa tano asubuhi, nikiwa ndani ya quality centre nikaingia kwenye cash point kutoa pesa.pembeni kulikuwa na kijana anaongea na simu kwa nguvu.mimi nilikuwa na mwenzangu ambaye ndo alinifanya nikatoe pesa mana alikuwa ananidai, basi nilivyokwisha kuchukua pesa nikampa rafiki yangu za kwake zilizobaki nikaweka kwenye pulse haoo tukaondoka.

  Tulipofika kwenye gari tukasikia mtu anaita kwa nguvu ''dadaa dadaa" yule mwenzangu akamwona akamwambia aniite, kumwangalia alikuwa ni yule kijana tuliomwona pale kwenye ATMs,akaomba kuongea nami nikatoka kwenye gari nikamsikiliza,kwakuwa nilikuwa naendesha gari la kampuni ambalo ni branded nadhani ndipo alipopatia mwanya wa kuanzia akasema anataka kufanya business na blabla kibao nikamwambia kwa wakati ule nipo busy itabidi nimschedule kwa kesho yake akasema yuko serious anataka akamilishe procedures zote za kufanya biashara na kampuni yetu, basi tukapanga tuonane jioni, kwa kuwa mimi sina usafiri binafsi nikachagua tuonane karibu na kazini ambapo ni quality centre lemon tree(msinijudge nature ya kazi yangu nafanya awkward hours),ikafika mida ya miadi nikaenda, yule jamaa alikuwepo akajitambulisha kwa jina la Paul Eric Shayo anafanya kazi Prime Minister's Office akanionyesha na ID yake,basi tukakaa kidogo tukaongea mara mwenzangu akasema twende peacock hotel kuna sehemu nzuri imetulia kwa juu,ila from the minute nimeongea nae mimi sikuwa normal nikawa najihisi kama nimekunywa pombe wakati niliagiza tu maji, na kila alichosema mi nilitii,basi tukaenda peacock hotel kuna kachilling place kule juu sijui kanaitwaje,cha kushangaza yule jamaa akawa haongei business tena akaanza kunambia kuwa amekuwa akifunga ili apate mke na Mungu kamuonyesha ni mimi,huyo mume niliyenae ni muigizaji tu,kwa kweli aliongea maneno mengi ya kutisha mpaka nikahisi sio binadamu yule kijana.akija muhudumu atamwambia "huyu mchumab wangu" akiongea na simu atasema "niko na mchumba wangu",nilistaajabu sana.wakati naondoka akaomba anipe lift nikakubali,kitendo cha mimi kuingia kwenye gari lake nilihisi kuishiwa na nguvu nikajikuta nipo pale shoprite pugu road kwenye ATM machine nakumbuka kumsikia ananiambia toa laki mbili na mimi nikatoa akasema lete kadi nikampa akachukua na pesa zote nilizokuwa nazo kwenye pochi..wakati huo wote nilikuwa kama mlevi fulani.nilikuwa nina mfuko una nguo na viatu vipya tukatoka hapo shoprite akaenda kwa speed mpaka mwenge pale bamaga kuna hotel pale kuna kagarden akasimamisha gari akanambia shuka haraka nikashuka akatoa gari kwa speed na mizigo yangu ikiwa mule ila pochi nilibeba,nilistuka baada ya dakika tano nikawa nimeshila wallet yangu nikaangalia hela hakuna kadi zote hakuna na niilmtajia mpaka pin.nikarudi nyumbani ila bado nilikuwa nayumbayumba.

  Jamani kuna uwizi wa ajabu sana, jana nikaamua kumtafuta huyu mtu nikaenda polisi afu nikaenda kuulizia prime minister's office,waliulizana ofisi nzima mpaka HR wote waliangali majina ya watu wao lakini hakukuwa na jina hilo.NILITAPELIWA kwa kupumbazwa.ssa sijui ni dawa gani alitumia vipi mi sijui mana sikunyanyuka kwenda chooni tuseme ameweka kwenye kinywaji.nimekoma mie kuongea na strangers jamani nimekomaaaaa,hapa nilipo sina kadi naanza kuzunguka mapolisi na benki,kaniharibia financial situation yangu yote pumbavu zake nina hasira na nilishika namba yake ya gari kabla sijaingia kwa gari ni T 116 BGH.ninampango wa kumtafuta huyu mtu hata miaka mia nne ijayo lakini nitampata tuuu,nina hasira sana kama gari si lake basi mwenye gari atamtaja.

  Wheeew jamani yamenikuta mwenzenu.
   
 2. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  pole mkuu! Hakuna lingine kwel alilokufanyia?...kuwa mwangalifu na appointment za watu usio wajua,next time nenda na kampani nyingine usiwe alone..
   
 3. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana na hiyo namba ya gari yawezekana gari ni bovu yeye anatumia tu kesho hautaina tena.Kuwa makini sana kama mtu anahitaji biashara na ofisi mwambie aje kwa ofisi siyo mitaani.Pia hayo ndo matatizo ya kupenda cha juu...
   
 4. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  pole sana.. ulete mrejesho ukimdaka..
   
 5. piper

  piper JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!, pole sana
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa aliku-hypnotize! Ni mbinu ya juu ya kitapeli.
   
 7. Dr.kapama

  Dr.kapama Senior Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asee pole sana,ila afadhali umeweka angalizo kwa watu wengine ambao hawajakumbana nayo ili wawe makini...
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,502
  Trophy Points: 280
  Shhhhiiiiiiiiiiii!!! Mkuu hilo jingine halipaswi kusemwa hapa. Isitoshe peacock hotel hakuna vyumba vya kulala wageni.
   
 9. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  siku hizi mimi kukutana na mtu nisiyemjua na kuanza maongezi nae ni hakuna niliisha kataa kitambo maana wezi wengi siku hizi tukiongea labda niwe mita 50 na yeye sitaki ushenzi wa kujuana juana.....ila pole ndio kujifunza huko mama
   
 10. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Huyo jamaa katumia mbinu za kimazingaumbwe ambazo zinapoteza uelewa wa mtu kwa muda pale unapotokea kumkubalia matakwa yake kwa mara ya kwanza. Wamejifunza kwa ajili ya maonyesho ya kuburudisha watu lakini siku hizi wanatumia kufanyia wizi, tuweni makini.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  pole sana....

  Utapeli wa namna hiyo nishawahi kuusikia kuna binti aliibiwa pesa yake benki tena aliitoa mwenyewe kwenye atm.....

  Ila why wanaibia wadada tu?

  Kwa kuwa una namba za gari naamini una pa kuanzia, ukiwa na network hata details za mwenye gari utazipata tra

  pole mwayego
   
 12. Shixi889

  Shixi889 JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Pole sana mimeskitika kweli maana naimagine kama angekufanyia mambo mengi ya ajabu na mabaya???inabidi tuwe makini sana na binadamu wa siku izi maana wengi hawana wema!!!
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Pole sana ....
  Nimejifunza kuwa makini zaidi na kustuka unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza na kuonyesha kukuhitaji kwa jambo fulani kwa haraka.
   
 14. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni kweli aisee anaweza kuitumia TRA kumnasa huyo jamaa. Sijui kama alikumbuka kureport hilo tukio polisi?
   
 15. peri

  peri JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  pole sana.
  Jifunze kutozoeana na watu uso wajua.
  Kama mtu anataka kufanya biashara aje ofisi.
   
 16. peri

  peri JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  pole sana.
  Jifunze kutozoeana na watu uso wajua.
  Kama mtu anataka kufanya biashara na kampuni aje ofisini.
   
 17. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tatizo la watanzania wengi ni kupenda sana cha juu..... kama huyo mtu alikuwa serious kweli kufanya biashara na kampuni yenu kwanini asingelikuja ofisini??????????? :sleepy:
   
 18. C

  Chiya Chibi JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kweli yamekukuta, ukiweza watafute Bongo movie uwauzie hii stor kabla hawajakuibia mana baadh yao wamo humu, imekaa vizur kuitizama sitting room..! Pole sana, matatizo huongeza ufanisi wa kimaisha, so hiyo ni sehemu tu, usife moyo endelea kuongea na watu, ila ongeza umakini!!!!!
   
 19. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,852
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  dah,asante kwa angalizo na pole kwa yaliyokukuta. me huwa nina tabia moja, sipendi kujuana juana. mwisho wa siku wanaanza kunambia kuwa najisikia,mara naringa lakin ukweli unabaki pale pale!
   
 20. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Jamani me najua utapeli unatokea popote lakini dar naiogopa ukweli nikiwa njiani hata mtu akinisalimia siitiki pole utampata tu Mungu ni wa ajabu sana
   
Loading...