Yaya aliyemtesa mtoto Uganda aomba msamaha

Yaya aliyemtesa mtoto Uganda aomba msamaha

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,789
141208112849_uganda__640x360_bbc_nocredit.jpg

Jolly Tumuhirwe

Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.

Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto

Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.

Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.

Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.

CHANZO: BBC

 
mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini uganda, amefikishwa mahakamani leo. Mfanyakazi huyo jolly tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto arnella. Licha ya taarifa ya polisi kusema jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo. Bi tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha jolly bila malipo. Kesi hio imeakhirishwa hadi jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya jolly. Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.

wale wajuaji waliokuwa wanamtetea waungane wamuwekee wakili........shetani huyu akaozee jela!!!!!
 
msamaha utakaomfaa ni kifungo tu ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo, ule sio ubinadamu hata kidogo kumtesa mtoto mdogo vile hata kama sio wako.
 
Afunge huyo dada roho mbaya al shabab wana afadhari sababu wanaua watu wazima. Video hile inatisha.mie wanangu walishindwa kuiona bali waliishia kulia tu. Pamoja na kifungo anatakiwa kuombea atokwe pepo chafu
 
msamaha hautoshi.. revenge is good

Lakini ms chaga tukija kwenye vitabu vya dini anayeomba msamaha anapaswa kusamehewa embu tujiulize ni mangapi sisi tuliomkosea muumba na je kama yeye angekuwa na moyo mgumu wa kutosamehe unafikiri kuna mtu angebaki leo hii?
 
Sheria ingeruhusu imfanye km alivyomfanya yule mtoto
 
......apewe tu adhabu, hata kama jela miaka 5...ili atakapotoka awe raia mwema.
 
kama ameomba msamaha wamsamehee tuu huku gerezani kwa muda aliokaa atakuwa amejifunza mengi hawezi kurudia tena japo kile kitendo kilikuwa cha kinyama .
 
Lakini ms chaga tukija kwenye vitabu vya dini anayeomba msamaha anapaswa kusamehewa embu tujiulize ni mangapi sisi tuliomkosea muumba na je kama yeye angekuwa na moyo mgumu wa kutosamehe unafikiri kuna mtu angebaki leo hii?

Huyu akisamehewa watoto na wajukuu zetu wapo hatarini maana wataona mbona msamaha upo nje nje
 
Huyu angekatwa kidole cha mkono kama kumbukumbu kwa aliyoyoyafanya.
 
Kama anajutia asamehewe tu. Adhabu ya kushambuliwa na jamii ya kimataifa inamtosha sana.
 
Hakuna kifungo wala adhabu duniani hivyo vipo mbinguni baada ya kufeli duniania hapa ss duniani tuna Kambi ya matesotu hats mm naunga mkono aende kambiya màteso muuaji mkubwa huyo.
 
Kwa kipigo kile alichompa yule malaika anastahili kuionja jera kidogo hata kama kaomba msamaha!
 
kuna thread picha humu jf inamuonesha huyo dada kapasuliwa uso... sielewi
 
Back
Top Bottom