Yawezekana "NAMBA" au "HESABU" hizi zikawa ndio "TISHIO KUU" kwa chama dola

IRINGA MOJA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
503
229
Heshima kwenu wadau,

ILi kupata picha ya nilichowaletea hapa ni lazima kwanza usome na kuelewa tathmini ya namba kama ambavyo zimejipambanua hapa chini.

Tathmini ya mada hii itajikita kuanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hadi 2015 lakini pia prediction ya 2020.

Ukijaribu kutafakari kwa kina juu ya nini hasa kinachoitia hofu serikali na chama dola katika kuruhusu ustawi wa demokrasia kwa kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa hususani siasa za upinzani utagundua hakuna jambo jingine zaidi ya hofu kuu ya "NAMBA" au "HESABU" kama inavyojionyesha hapa.

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010

Kuga MzirayPPT - MAENDELEO kura 96933 (1,12)
Kikwete Jakaya - CCM kura 5276827 (61.17)
Slaa Wilbroad - 2271941 (26.34)
Lipumba Ibrahimu - kura 695667 (8.067)
Rungwe Hashim - NCCR MAGEUZI kura 26388 (0.31)
Mgaywa - TLP kura 17482 (0.20)
Dovutwa Nassoro - UPDP kura 13176 (0.15)

matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

Anna Mgwira - ACT kura 98763 (0.65)
Chief Yemba - ADC kura 66049 (0.43)
DR John Magufuli - CCM kura 8882935 (58.46)
Lowassa Edward - CHADEMA kura 6072848 (39.97)
Hashim Rungwe - CHAUMA kura 49256 (0.32)
Kasambala Malik - NRA kura 8028 (0.05)
Lyimo Elifatio - TLP kura 8198 (0.05)
Dovutwa Nassoro - UPDP kura 7785 (0.05)

tofauti iliyopo

Ukiachilia mbali matokeo ya vyama vingine ni wazi ya kwamba mpambano ulikuwa mkali kati ya CCM na UKAWA tofauti ilitopo kati yao kwa idadi ya kura za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na ule wa 2015 ni kama ifuatavyo.
  1. CCM iliongeza kura 3606108 yaani 8882935 mwaka 2015 kutoa 5276827 mwaka 2010
  2. UKAWA (CHADEMA, NLD, NCCR MAGEUZI na CUF waliongeza jumla ya kura 3078852 yaani 6072848 kutoa 2271941 (CHADEMA 2010) kutoa 695667 (CUF 2010) kutoa 26388 (NCCR MAGEUZI 2010)

kilichopelekea kuongezeka kwa kura kati ya CCM na UKAWA.
Ukiachilia mbali nguvu walizokuwa nazo wagombea ni dhahiri ya kwamba vyama vyote vilijitahidi kuongeza na kulinda kura walizozipata katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwa style ya;
Mikutano ya hadhara - vyama vyote
Maandamano - UKAWA
Kurudisha dhana ya uwajibikaji kwa wananchi - CCM

kwa picha ya nje unapata jibu ya kwamba njia ya mikutano na maandamano iliwabeba sana UKAWA na kuleta hofu kuu ndani ya chama dola na hivyo kupelekea upigwaji marufuku wa mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya siasa kwani ni tishio kwa serikali na chama dola katika kutumikia madaraka. Hivyo Namba au hesabu hizo juu ndio tishio kuu kwa wakubwa.

 
Chadema acheni unafiki ,

Kama Lowasa na Mtei wamesema Magufuli anafanya kazi vizuri, alafu kibavicha kisicho na mbele wala nyuma kinajitokeza kuwapinga hawa wazee.

Mkome
 
Chadema acheni unafiki ,

Kama Lowasa na Mtei wamesema Magufuli anafanya kazi vizuri, alafu kibavicha kisicho na mbele wala nyuma kinajitokeza kuwapinga hawa wazee.

Mkome
tupe chanzo mkuu wapi ili tukakaangalie au tukasome na sisi.
 
nikupongeze kwa uzi huu pamoja na hoja nzuri vyama vya upinzani havibebwi na maandamano ,na endapo ukaona yapo zingatia ujumbe uliopo unalenga maslahi ya nchi na watu wenye uzalendo wa kweli kwa nchi yao ,bila kujali changamoto wanazokutana nazo katika majukumu yao kisiasa .rejea kumbukumbu zako huko nyuma .
 
Watumishi wa umma na wafanyabiashara wana hasira sana kwa kuwa wamekuwa embarrassed sana bila sababu ya msingi
hata kabla ya kuulizwa matatizo yanayowakabiri tangu mwaka 1961 mpaka leo,pamoja na mchango wao wakukuza pato la taifa nakuwa waaminifu kama walipa kodi halali wa serikali zote zisizo na huruma za ccm wanakuja kuambulia fedheha badala ya maridhiano na watawala wapya
 
kama wanaompinga magufuli na upofu wake ni mawakala washetani basi ccm na magufuli ndo mfalme shetani mwenyewe,huenda sasa mawakala tumechoka kunyonywa na kukandamizwa na huyu shetani mkuu magufuli na wanae ccm
Dunia ingekuwa inaelewa kiswahili ingekumeza...i mean, nchi zingine zinataka kumuazima Magu walau kwa miezi miwili na wewe unaleta uharo hapa!
 
Dunia ingekuwa inaelewa kiswahili ingekumeza...i mean, nchi zingine zinataka kumuazima Magu walau kwa miezi miwili na wewe unaleta uharo hapa!
dunia ipi hiyo ntajie nchi moja,labda watuazime wakamtibu matatizo ya mtindio
 
Chadema acheni unafiki ,

Kama Lowasa na Mtei wamesema Magufuli anafanya kazi vizuri, alafu kibavicha kisicho na mbele wala nyuma kinajitokeza kuwapinga hawa wazee.

Mkome
Na wewe utukome kama ulivyokoma nanilii..... Mshenzi wewe
 
Mawakala wa shetani mmemwagwa kwa nguvu JF
ha ha ha ha CC
nikupongeze kwa uzi huu pamoja na hoja nzuri vyama vya upinzani havibebwi na maandamano ,na endapo ukaona yapo zingatia ujumbe uliopo unalenga maslahi ya nchi na watu wenye uzalendo wa kweli kwa nchi yao ,bila kujali changamoto wanazokutana nazo katika majukumu yao kisiasa .rejea kumbukumbu zako huko nyuma .
Noted.
 
Back
Top Bottom