Yathibitika: Kutooa au kuolewa ni kaburi la mapema…!

Yathibitika: Kutooa au kuolewa ni kaburi la mapema…!

Huu utafiti wala hauakisi uhalisia wa mambo kwenye jamii yangu labda kwa wamarekani Tu kutokana na lifestyles zao maana hata vyanzo vya vifo vilivyotajwa mostly ni lifestyle diseases.

Kama issue ni kusaidiana,then maustadhi wenye wake 2+ wangekuwa na maisha marefu zaidi yetu ma-bachelors lakini mbona wanalamba mchanga daily kama sisi Tu?

Bibi yangu mkubwa ana 97yrs now na hakuwahi kuolewa na Hana hata mtoto lakini wadogo zake wanne waliokuwa wameoa na kuolewa tushawazika.Hapa unasemaje?

Huu utafiti bado haujajitosheleza kunishawishi kuoa.
 
miss chagga, hebu soma majibu yangu kwa charminglady, huyo Bi Kidude alikuwa amezungukwa na Marafiki, ndugu, vijukuu, vitukuu na vilembwe, hakuwahi kuwa mpweke kutokana na kuwa na nasaba nyingi

Kama swala ni upweke may be... to me kaka mtambuzi marrage its a hell... totaly hell unayoiomba mwenyewe hapa duniani
 
Last edited by a moderator:
Alichosema mtambuzi kimefanyiwa utafiti acha ubishi!! .Hata TZ tukifanya utafiti matokeo ni hayohayo tena yatakuwa worse

Utafiti kwa ndoa hizo za zamani kwa sasa kuanzia ndoa za watu wenye miaka 40 ndoa zao wengi ni kuzimu ndogo... zamani nakubaliana nae.. marrage for now is hell
 
Kuna utafiti nimeusoma na nitauweka hapa umebainisha kwamba ndoa imara huponya hata kansa.....
Lakini utafiti huu uko tofauti kidogo, hapa hata wale waliooa au kuolewa wakaachana wanaweza kuwa na umri mkubwa suala hapa ni kutokuwa na upweke kutokana na kuongeza nasaba kutoka upande wa pili wa mwenzi wako. kumbuka hata kama wanandoa wameoana na kuchana bado ule mtandao wa ndugu na marafiki walioutengeneza hauwezi kufa labda tu utapungua, lakini unaweza kuwa mzuri na imara kiasi cha kuwapa faraja na hivyo kuongeza umri wa kuishi

Alichosema mtambuzi kimefanyiwa utafiti acha ubishi!! .Hata TZ tukifanya utafiti matokeo ni hayohayo tena yatakuwa worse

Hahahahah mbona mnatulazimisha tumeze hili desa lenu kisa et limefanyiwa utafiti.....haturuhusiwi kuhoji,kukosoa na kutoa maoni yetu?
 
Pamoja na mayoyoso na changamoto zote ndani ya ndoa, bado ndoa ni bora kuliko ukapera.

Ndokusema unataka kuniambia nimekalia kuti kavu? Mtambuzi, makala yako flani iliyopita ilikuwa inasema kuoa/ kuolewa sio lazima cha muhimu kuijaza dunia. Sasa hii makala inatutisha sie makapera au inaijibu/ inaikosoa ile makala yako ya nyuma?

Noja niendelee kula ujana vya mwisho mwisho kabla sijabadili maamuzi.
 
Last edited by a moderator:
Kama ndo hivi ngoja nioe wapendwa,nisijekufa mapema.
Huyu bwana mdogo mwelewa,mpole,hana jeuri,tutaelewana tu.
 
Mkuu Mtambuzi yote hayo yanategemea kama umempata mrs right au mwamanke amempata mr right zaidi utaishia kuwa na stress maisha yako yote na hutakuwa na maisha mazuri hata kidogo
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kitu kama hicho Mungu hakukosea kusema ndoa iwepo tena ya mke mmoja na mme mmoja
 
Hebu soma hapo kwenye bold halafu weka kwa kinyume chake.

Utafiti umebainisha kwamba sababu za kufa mapema, zinazotokana na kutooa au kuolewa, mojawapo ni upweke na kutokuwa na mtu wa kusaidiana kubeba mizigo ya maisha na kukumbushana kuhusu afya zetu.....

Hao Mapadri unaowazungumza wanahudumiwa kwa kiwango cha juu na wamezungukwa na masista wanaowahudumia kwa karibu sana, ina tofauti gani na mtu aliyeoa kama unaangalia swala la kuhudumiwa?

Sema tu kinachokosekana ni tendo la ndoa ambao halikuhusishwa katika utafiti huu kama ni chanzo cha kusogeza uhai.
charminglady usiniangushe bana hebu soma mada yangu between the line......... LOL

Nimekuelewa Mzee Mtambuzi, nimeisoma mada yako nikiwa natembea may be ndio sababu ya kutoilewa kwa haraka!

Afu nakutafuta ujue...
 
Last edited by a moderator:

Huu utafiti wala hauakisi uhalisia wa mambo kwenye jamii yangu labda kwa wamarekani Tu kutokana na lifestyles zao maana hata vyanzo vya vifo vilivyotajwa mostly ni lifestyle diseases.

Kama issue ni kusaidiana,then maustadhi wenye wake 2+ wangekuwa na maisha marefu zaidi yetu ma-bachelors lakini mbona wanalamba mchanga daily kama sisi Tu?

Bibi yangu mkubwa ana 97yrs now na hakuwahi kuolewa na Hana hata mtoto lakini wadogo zake wanne waliokuwa wameoa na kuolewa tushawazika.Hapa unasemaje?

Huu utafiti bado haujajitosheleza kunishawishi kuoa.

Nakuunga mkono mkuu... now days mdada kaolewa miaka mitano mingi wameshakuwa wazee stress nyingi tu
 
Hahahahah mbona mnatulazimisha tumeze hili desa lenu kisa et limefanyiwa utafiti.....haturuhusiwi kuhoji,kukosoa na kutoa maoni yetu?

Kumbuka huo utafiti ni watu.walioa 1970 na 80 sasa imagine wanaolewa na kuoa miaka hii ndoa yenyewe kudumu miaka mitano ni tatizo ndio kuishi maisha marefu kwa hili nitapinga mpaka naingia kaburini
 
Nafikiri utafiti huu ulilenga zaidi kuishi maisha yasiyo na UPWEKE au kuishi katika ukamilifu wa furaha!!!
 
Huu utafiti wala hauakisi uhalisia wa mambo kwenye jamii yangu labda kwa wamarekani Tu kutokana na lifestyles zao maana hata vyanzo vya vifo vilivyotajwa mostly ni lifestyle diseases.

Kama issue ni kusaidiana,then maustadhi wenye wake 2+ wangekuwa na maisha marefu zaidi yetu ma-bachelors lakini mbona wanalamba mchanga daily kama sisi Tu?

Bibi yangu mkubwa ana 97yrs now na hakuwahi kuolewa na Hana hata mtoto lakini wadogo zake wanne waliokuwa wameoa na kuolewa tushawazika.Hapa unasemaje?

Huu utafiti bado haujajitosheleza kunishawishi kuoa.
Ubishi mwingine wa ajabu....
Utafiti umehusisha watu 80,000, unatarajia nyanya yako aliyeko Kipatimo Kilwa naye awemo?
Pamoja na kwmaba utafiti umefanywa nchini Marekani, lakini huoni kwamba mtindo wetu wa maisha unapoelekea haraka sana tutafanana na hao Wamarekani. Huoni jinsi utamaduni wa Magharibi unavyoshika kasi hapa nchini?

Kuhusu kwamba kuoa wake wengi hakuongezi umri wa kuishi, labda hukusoma huu utafiti mwingine

Gonga hapa:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...itika-kuoa-wake-wengi-huongeza-umri%85-4.html
 
nikweli na ndo maana micba ming ya wanaokufa ni mapadri na masista c ndio?

Wanamegana wake mkuu na kulawiti so hawawezi kufa,,au hujasikia juzi tena mwanza padri kafanya yake.

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Hahahah...not hell bhana kuna ndoa watu wanainjoi hadi unatamani na wewe uombe ndoa lol

Kweli, ata kama ndoa mia zipo ICU yako iko vizuri, izo ndoa zingine zisikutishe.Tusitishane jamani kuna ndoa ukiiona asubuhi utatamani na wewe mchana ukafungue ndoa.
 
Ndokusema unataka kuniambia nimekalia kuti kavu? Mtambuzi, makala yako flani iliyopita ilikuwa inasema kuoa/ kuolewa sio lazima cha muhimu kuijaza dunia. Sasa hii makala inatutisha sie makapera au inaijibu/ inaikosoa ile makala yako ya nyuma?

Noja niendelee kula ujana vya mwisho mwisho kabla sijabadili maamuzi.

Wale ambao hawajawahi kuoa au kuolewa na wakawa hawana watoto au wakawa hawana ndugu na jamaa wengi wa kuwa nao karibu, hawa hufa mapema zaidi. Walioolewa na kuachwa au waliooa na kuacha, wanakuwa na mtandao fulani, ambao wanandoa huwa nao kwa kawaida.

Tafiti nyingi za siku za nyuma na hivi sasa zinaonnesha kwamba, kutengwa au mtu kukosa watu wa kuwa karibu naye katika masuala ya kijamii, husababisha kifo cha mapema. Ndoa hujenga ukaribu huo kwa sababu, mtu hujiongezea watu wanaomhusu kutoka kwa mwenzake.
Kasinde zingatia kwenye rangi nyekundu......
Wewe zaa tu ili usije kosa mwana na maji ya moto, yaani usije kosa mume na hata mtoto wa kukuletea maji na dawa ukiumwa

Zaa tu mwanawane kuolewa ni majaaliwa........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom