Yani nimekasirika kinomaa. Wanawake acheni hii tabia

Yani nimekasirika kinomaa. Wanawake acheni hii tabia

Juzi kati nili Import Dem mmoja toka Dar akaja Mkoa walau Abadirishe mazingira. Tulikubaliana kama atakaa wiki moja na baadae arudi Dar. Dem alifika nikampokea.

Maisha ya kigeto yakawa yanaendelea nikiwa na mwanamke ndani. Maisha yameenda poa sana. Hasa ninaporudi toka vibaruani nakuta msosi, ndani kusafi, nguo zangu zimefuliwa na huduma za usiku napata yani hadi nikaanza kujiona FAZA.

Ishu imefika wiki sioni kama Manzi ana dalili za kuondoka. Kila nikimtrance naona kama ndo kafika. Nikaona sasa hiki ni kisanga. Nikajaribu kutunga safari za kikazi ili walau aseme anaondoka nikaona bado kimya anasema nikirudi ntamkuta. Nikatia figisu weeeeee hadi akaondoka.

Lakini amekaa Almost Mwezi mzima kwangu.
Sasa kipindi yupo hapa getto alikuwa anavaa nguo zangu kama Track suit, T-shirts na baadhi ya suruali zangu.

Yani ameharibu nguo zangu vibaya mnoooo. Nimeumia sana. Yani Tshirt zangu ziwezi kuzivaa tena maana zimetanuka kifuani kwa ajili ya matiti pia zina vile vinukta vya Chuchu.

Suruali zangu zimekuwa na Misambwanda balaaa. Yani zimekuwa kubwa matakoni na kiuno kimekuwa kikubwa balaaa.

Yani Jumla ya Nguo kama 20. Zenye thamani hadi kufikia laki 7 zimeharibika kabisa yani.

Mbaya zaidi wakati anataka kuondoka akasema et hajawai kupanda ndege. Ivyo anataka achukue flight to Dar.

Nikawa sina namna maana nataka aondoke tuu. Nikafanya booking ya siku 4 before nikapata ticket ya fast jet kwa 350k

Wakati namsindikiza akat wanafanya inspection kuna viti walikataa visippande ndege. Ni kama mafuta, perfum na vitu kibao. So ikabidi anipe nirudi navyo

Baada ya kufika home nikagundua kuwa ameacha vitu vyake vingine kama kanga nilizomnunulia maana alikuja na mtandio tu na nguo maa alikuja na pochi tu na huku nilimnunulia baadhi ya vitu.

Kasema mwisho wa mwezi atakuja kuchukua vitu vyake. Yani nimekasirika kinomaaaa

Wanawake acheni maudhi jamani.

Kuna masweta yangu nilinunua Ebay toka uturuki yote ameyaharibu kisa alikuwa anavaa apigie picha/ self ili awe anapost.

Yani nimeumia wajameni balaaa.
Hii hadithi yako ya kutunga haina mashiko. Ni utunzi wa kitoto
 
Mimi ni mwanaume wa mikioani
Ulifikiri unapikiwa, unafuliwa na kusafishiwa nyumba bure????? na ule ufundi wa kukatika uliouonyesha ulidhani bure bure tu.... loooooo wanaume wa dar jueni kula na kulipa.... na badooo atarudi tena kwa kasi mpya
Ila nimekutana na mwanamke wa dar
 
Mkuu mbona vitu vya kawaida kila mtu ana mapungufu yake inawezekana labda anajua una malengo nae pia amekupenda
 
Mwenzie alikua anapiga hesabu akirudi mjini ahangaike kusaka pesa, kupambana na daladala nk so akaona bora akae huko mkoani service zote anapata gharama ni kukitumia kiuno chake tu maana hizo za kupika, usafi nk hata kwake huwa anafanya.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wakuu tusijisahaulishe Mo katekwa na watu wasiojulikana maana waliovaa maksi lakn n WAZUNGU WAWILI
 
Back
Top Bottom