Nimeona taarifa inayosema klabu ya Yanga imetuma barua Azam Media ili kuomba kubadilishwa kwa mtangazaji aliyetumika kumuhoji Gamondi siku ya mechi ya tarehe 29.09.2024 dhidi ya KMC pale Azam complex.
Je taarifa hii ina ukweli wowote..!?
Je taarifa hii ina ukweli wowote..!?
- Tunachokijua
- Young Africans S.C (Yanga) ni timu ya Mpira wa Miguu iliyoanzishwa mnamo mwaka 1935, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mnamo 29, 2024 Septemba Yanga walishuka dimbani kucheza na timu ya KMC ambapo waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0. Mara baada ya ushindi huo, kumeibuka taarifa zinazodai kuwa Yanga wametuma Brua kwenda Azam Tv kuomba kubadilishwa kwa mtangazaji aliyemuhoji Kocha wa Yanga Miguel Gamondi baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga na KMC uliochezwa uwanja wa Azam Complex mnamo 29 Septemb 2024
Je, ukweli ni Upi?
JamiiCheck imetafuta vyanzo mbalimbali vya taarifa vya kuaminika ili kupata taarifa juu ya Yanga kutuma barua Azam kutaka kubadilishwa kwa Mtangazaji ambaye alimuhoji Gamondi na Kubaini kuwa hakuna taarifa hizo, Pia kupitia ufuatiliaji wa kimtandao hakuna taarifa hiyo kwenye page rasmi Za Yanga wala Azam
Aidha, JamiiCheck imezungumza na Mkuu wa Oparesheni Azam Media, Yahya Mohamed ambye amekanusha AzamTv kupokea brua kutoka Yang inayodai kubadilishwa kwa mtangazaji ambaye alimuhoji Gamondi.
"Hatujapata barua yoyote kutoka Yanga inayohusu malalamiko au mtangazaji wetu yeyote, nimewatafuta Yanga labda kama wameandika barua tuwe hatujaipata lakini sijafanikiwa kuwapata kwa harakaharaka, hivyo kwa ufupi nadhani ni masuala ya Mtandaoni tu hakuna ukweli juu ya taarifa hizo".