Yanga wameacha kusema Wana watu, wanasema wamekodi Ndege. Jumapili baada ya mechi watakuja kauli mbiu gani?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
UTANGULIZI
Timu ya Yanga imeamua kukodi Ndege ya Shirika la ndege la Tanzania kwenda Nigeria, lakini tukumbuke mpira siyo uzuri wa lifti kuelekea uwanjani Bali mpira na mbinu na ujuzi. Mchango wa pipa la kukodi wakati walishindwa kutumia uwanja wa nyumbani ni mdogo Sana kwenye ushindi isipokuwa Ni mkubwa kwenye tambo za ndani ya bongo.

YANGA WANA TIMU?
Yanga Bado haijawa na timu bali ina kikundi Cha wachezaji ambacho kinategemea kocha ikiunde kiwe timu.

JE, KIKUNDI HICHO CHA WATU KINAWEZA KUWA TIMU MWA MUDA WA WIKI MOJA?

Hakuna miujiza ya kikundi Cha wachezaji kugeuka kuwa timu ya mpira ndani ya wiki moja. Maandalizi yalipaswa kuanza kabla hata ya Yanga day, uwekezaji ulipaswa kufanywa mwanzo ikiwa ni pamoja na kuandaa timu.

TUTEGEMEE NINI HUKO NIGERIA?
Hakuna namna kikundi Cha watu kinaweza kushinda isipokuwa tutegemee Yanga kurejea na goli 2-0 na hii iwe fundisho kwa matajiri wa bongo. Muda wakuandaa timu wanafanya mbwembwe za jezi! Wanakwenda kuvuna walichopanda.

NINI WAFANYE?

Waamue kwa moyo mmoja kukubaliana kwamba wanawaandaa mashabiki wao kwa matokeo hasi ili wasipate lawama.

LAKINI SIMBA WANA TIMU?

Nao pia safari hii hakuna timu Kuna kikundi Cha watu ila wao Wana bahati kwamba wameona wenzao walivyonyolew na hovyo kuwaondoa wachezaji kwenye presha za Simba day.

Wachezaji wa Simba wanajua jukumu walilonalo la kudhibiti miyoyo ya mashabiki kumomonyoka kwa matokeo mabaya. Wanatakiwa kuwanyima Yqnga wasipate chakusema.

Yanga na Simba chezeni mpira acheni tambo za utajiri na nguvu ya kiuchumi.
 
Yanga SC kwenda na Lundo la Watu nchini Nigeria wamefanya vyema kwani kwa Fujo zitakazoambatana na baadhi ya Viongozi wao Kupigwa hao Watu wengine watakuwa na Jukumu la Kuwachua Majeraha yao na kuwapaka Spirit katika Vidonda vyao.
 
Hivi huwa kunakuwaga na ulazima gani wakuitaja Simba kwenye kila Jambo la yanga? Hii tabia ifike kipindi ikome Mana Simba inajitaidi kutoka kwenye ubabaishaji (na inaena kufanikiwa) kuiweka daraja moja na timu ambayo bado inaamini kwenye ujinga ujinga mwingi ni kuikosea heshima simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom