Wana Yanga tuje tutafakari safari ya nusu fainali hapa

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,373
2,513
Uzi huu ni sehemu ya maoni ya mashabiki mtazamo wao, hauna lengo la kufundisha watu majukumu kwasababu tunaamini tuna benchi la ufundi, wachezaji na uongozi unaojua nini cha kufanya.

Tuje kwenye mada, siku ya Ijumaa timu ya Yanga itamaliza mechi yake ya hatua ya makundi kwa kucheza mechi Cairo dhidi ya Al Ahly.
Je mwananchi ungependa Yanga iongoze kundi au ikibakie hapo hapo kwenye nafasi ya pili?
Kama Yanga itaongoza kundi atapata nafasi ya kuanzia ugenini kwenye mechi yao ya kwanza ya robo fainali na kukutana na timu itakayoshika nafasi ya pili kwenye kundi A, B, au C.

Mpaka sasa ni timu moja pekee ndio iliyokuwa na uhakika wa kuongoza kundi, ambayo ni Asec Mimosa ila timu zilizobakia zote zinasubiri hadi mechi ya mzunguko wa mwisho.

Kundi A
1. TP Mazembe/ Mamelod

Kundi B
1. Asec Mimosa
2. Simba/Wydad/Galaxy

Kundi C
Petro Luanda/ Es Tunis/ Al Hilal

Je mwananchi ungependa mechi ya robo tupewe yupi hapo? Binafsi ningependa timu yeyote kutoka group B na C wale wa group A watuache kwanza hadi huko mbeleni ndio watupe kama tuki qualify.
 
Ninashauri wachezaji, uongozi , benchi la ufundi na wanayanga kwa ujumla wasibweteke na ushindi huu, bali iwe chachu ya kusonga mbele zaidi'.
 
Me ningependa tungepewa timu yeyote ile kasoro isiwe Mamenlod ama Simba.

Nikianza na Simba, huyu jamaa atatuletea kutujua sana, hivyo anaweza kutuharibia ndoto zetu za kuchukua ubingwa na vile vile mechi yetu haitakua na msisimko mkubwa sababu ya hiyo hiyo kujuana.

Kwaupande wa Mamenlod huyu jamaa tukimtoa, fainali tutacheza na nani sasa?
Huyu jamaa inibidi tukutane nae fainali ili iwe yenye mvuto sana.

Binafs ningependa robo tukutane na Atretico de Luanda, nusu tukutane na Al ahal, Fainali tukutane na Mamenlod.

Ila yote kwa yote naiona Yanga ikitwaa ubingwa ACL 2023/ 2024.
 
Back
Top Bottom