kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,318
- 12,622
Hakukuwa na ulazima wa Simba kumfukuza kocha peke yake kwa kosa la kufungwa magoli 5 na Yanga. Kufungwa kwa Simba kulisababishwa na sababu na wadau wengi wakiwemo viongozi na wachezaji wenyewe.
Simba iliingia kwenye mechi ile wadau wote wa simba (kocha, wachezaji, uongozi na mashabiki) wakiwa na hofu kubwa sana ya kupoteza. Hofu yao ilitokana na ukweli ambao walikuwa wanaufahamu kuwa Yanga inacheza vizuri, ina wachezaji wazuri, ina kocha bora na uongozi mzuri kuliko Simba. Na kitendo cha kocha Gamondi kuhudhuria kwenye mechi za Simba kulizidisha hofu yao hii. Hofu hii ya wadau wote wa simba ilifanikiwa kujipenyeza kunye akili na miguu ya wachezaji wa Simba wakashindwa kucheza.
Hofu ya simba kabla na wakati wa mechi inathibitishwa na mambo yafuatayo:
1. Ahmed Ally, msemaji wao kabla ya mechi mbele ya kamera alisema kuwa Yanga ni timu imara na imekamilika kila idara, aliwatia hofu wadau wote wa simba.
2. Manula kudaka: Kitendo cha kumchezesha Manula kwenye mechi ile na kuwaacha makipa wote waliokuwa wakidaka kwa miezi karibu 7 ni dalili nyingine ya hofu kuu ya mechi, hofu hii ilikwenda mpaka kwa wachezaji na wadau wote.
3. Kuumia na kutolewa kwa Kibu Denis kuliongeza hofu kwa wachezaji. Simba amekuwa ikimuimba Kibu mbele ya wachezaji wenzake kuwa ndiye mchezaji bora na muhimu kwenye derby ya Simba na Yanga, hadi wakaampachika cheo cha kijinga cha mgeni rasmi wa mchezo; na baahati nzuri Kibu aliweza kusawazisha goli la Msonda ndaniya dk 6 tu. Kuumia na kuondolewa uwanjani "mgeni rasmi" aliyesawazisha goli kulizidisha hofu kwa simba na kusababisha kocha, wachezaji na wadau wengine kuwa na hofu kubwa.
4. Kutolewa kwa Chama. Chama anaamika kuwa mchezaji anaeweza kubadilisha matokeo yeye kama yeye ingawaje kocha hamtaki Chama kwenye mfumo wake wa uchezaji. Kutolewa nje kwa Chama kulizidisha hofu kwa wachezaji wengine kama Saido na wengine kwenye kikosi.
5. Kuingia kwa Onana: Wachezaji wote na mashabiki wote wa simba wanafahamu kuwa Onana ni unga, kuingia kwa Onana kulizidisha mashaka.
6. Kuundwa kwa kamati ya watu 21 muda mfupi kuelekea siku ya mechi ni ushahidi mwingine kuwa Simba ilikuwa na hofu (phobia) kuu.
Haikuwa sahihi kumuondoa KOcha peke yake, bali walitakiwa kutumia makosa ya mechi ile kujiimarisha zaidi. Vinginevyo, walipaswa kuondoka kocha, baadhi ya wachezaji na baadhi ya viongozi wakuu wa Simba.
Robertihno ana akili sana, aliweza kuwatumia wachezaji wabovu na wazee kupata matokeo, mtamkumbuka tu.