Yanga mnaivimbia TFF kisa kanuni imekiukwa. Mmejipanga kuzifuata kanuni zote au ni mihemko tu?

TFF Ni lini waliifavour Yanga kwenye maamuzi yao. Itoshe kusema Karia na wahuni wenzie siku zao zinahesabika hapo karume mwezi wa name siyo mbali tunaenda kufuatilia mbali upuuzi huu wote.
Mwaka 2016 Yanga walimsajili Mrisho Ngasa na wakati akiwa na mkataba na Azam na Simba hivyo Yanga walivunja kanuni za usajili ilitakiwa kwanza Yanga iwasiliane na Simba maana mchezaji alikuwa kwa mkopo Simba akitoka Azam badala yake TFF haikuipa adhabu Yoyote Yanga ilitakiwa Yanga afungiwe asisajili kwa mujibu ya sheria hapa TFF walibeba Yanga nimeshakupa mfano kuwa TFF wanazibeba sana Simba na Yanga
 
Achwa waumane Jana utopolo wameibuka mshindi sijui sasa uko mbele nani atakuwa bingwa ila sisi simba ngoja tukamtafutie viti maalumu vya club bingwa, uto hanaga shukurani siku zote
 
TFF inaendesha Mambo yake kwa kuzingatia kanuni na sheria. Ni sawa.

Lakini ni mara nyingi sana TFF imekuwa ikifumbia macho makosa mengi ya ukiukwaji wa kanuni na sheria zake yanayofanywa na vilabu vyetu, vikiwemo Yanga na Simba.

Ni muktadha huo wa kubebana na kuchukuliana ndiyo TFF iliutumia kusukuma mbele kwa masaa mawili mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yqnga.

Kitendo cha Yanga kuikaba koo TFF kinamaliza enzi za kuchukuliana na kubebana. Yanga inaiambia TFF kwamba Sasa izifuate kanuni zake kwa 100%. Hapa naona atakayeumia ni Yanga, maana TFF wameshikilia mpini.
Daah Mkuu kwa hili waache waibane Yanga kwenye kanuni zote wanazozijua. Huwezi ahirisha mechi ndani ya masaa 3 tena bila sababu ya msingi, never ever. Mimi binafsi nilifikiri huenda wamepewa tip kuhusu usalama wa uwanja kuwa mdogo, so wanajipanga kumitigate hilo. Ingekuwa kwa nchi zenye kufuata Sheria, Leo Karia angekuwa Mwananchi wa kawaida na si Rais wa TFF.
 
TFF inaendesha Mambo yake kwa kuzingatia kanuni na sheria. Ni sawa.

Lakini ni mara nyingi sana TFF imekuwa ikifumbia macho makosa mengi ya ukiukwaji wa kanuni na sheria zake yanayofanywa na vilabu vyetu, vikiwemo Yanga na Simba.

Ni muktadha huo wa kubebana na kuchukuliana ndiyo TFF iliutumia kusukuma mbele kwa masaa mawili mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yqnga.

Kitendo cha Yanga kuikaba koo TFF kinamaliza enzi za kuchukuliana na kubebana. Yanga inaiambia TFF kwamba Sasa izifuate kanuni zake kwa 100%. Hapa naona atakayeumia ni Yanga, maana TFF wameshikilia mpini.
tff bila hao yanga hawapati ugali ndugu,hizo timu 2 sio ndogo kiasi hicho
 
Mimi najiuliza tu je kwa mfano serikali ikaamua bora ipate hasara tu na kuamua kuwa utatumiwa na timu ya taifa pekee ,iwe Uhuru au mkapa stadium ,pia serikal kuanzia Sasa ikaamua kutotoa ulinzi wowote kwenye micho ya yanga Nan ataumia Zaid hapa?
Muda mwingine ni bora ukawa mjinga tu kama unajua hujiwez kwa vingi ,hapa tz club ambayo angalau inaweza kuvimbiana na serikal ni Azam pekee lakin nao lazima watakaa tu kwenye swala la ulinz siku za match
 
Suala si kuvieleza vilabu kukubali kuwa hii ni dharura na ni ya msingi. Kanuni haijatoa mjadala kati ya TFF na vilabu bali TFF kuiona sababu yenyewe na kuridhia udharura na msingi. Nini kufuate na kulingana na muda uliopo, hayo yote yako mikononi mwao.

Hapa ndo huwa tunaingia kwenye kutengeneza kanuni nyingine ili kulinda upande wa pili usiumie. Lakini, ni baada ya mambo kuwekwa sawa.

Huwa inasemwa kanuni hutengenezwa baada ya kuona mwanya fulani unaoweza kutumika vibaya.

Kumbuka TFF, haiwezi kuelea tu bila kuhusika na serikali. Sisi huwa tunaona tu michezo ikichezeka lakini mfano: FIFA haiwezi kuleta askari wake au TFF ili kuangalia usalama hivyo ukipata udhuru wa upande wa serikali ni mhimu kuzingatia kama unaleta maana.

Ni rahisi kusema mengi lakini suala ni lile TFF wataibuka nalo ikiwa sababu toka upande wa serikali kama wataona haja ya kulisema ndo utasikia SI MNGETUAMBIA KITU CHENYEWE TUSINGEKATAA.

Je kanuni imesema ujulishwe hilo suala?
Ndefu ila haieleweki.....! Yanga wapo sahihi 100%. Mechi itapangiwa tarehe nyingine kuchezwa! Na Tff wameomba radhi kwa upuuzi uliotokea jana!
 
Suala si kuvieleza vilabu kukubali kuwa hii ni dharura na ni ya msingi. Kanuni haijatoa mjadala kati ya TFF na vilabu bali TFF kuiona sababu yenyewe na kuridhia udharura na msingi. Nini kufuate na kulingana na muda uliopo, hayo yote yako mikononi mwao.

Hapa ndo huwa tunaingia kwenye kutengeneza kanuni nyingine ili kulinda upande wa pili usiumie. Lakini, ni baada ya mambo kuwekwa sawa.

Huwa inasemwa kanuni hutengenezwa baada ya kuona mwanya fulani unaoweza kutumika vibaya.

Kumbuka TFF, haiwezi kuelea tu bila kuhusika na serikali. Sisi huwa tunaona tu michezo ikichezeka lakini mfano: FIFA haiwezi kuleta askari wake au TFF ili kuangalia usalama hivyo ukipata udhuru wa upande wa serikali ni mhimu kuzingatia kama unaleta maana.

Ni rahisi kusema mengi lakini suala ni lile TFF wataibuka nalo ikiwa sababu toka upande wa serikali kama wataona haja ya kulisema ndo utasikia SI MNGETUAMBIA KITU CHENYEWE TUSINGEKATAA.

Je kanuni imesema ujulishwe hilo suala?
Leo maelezo ya TFF umeyaona?na wao wanasikitika kama wewe na mimi,
 
Yap, ndo hapo tunasema kanuni kuwekewa mazingira ya kutotumika kumuumiza mwingine kwa nia ovu, badala ya kuziacha zinaelea tu.

Kama hawakuwa na dharura ya msingi wajibebe.
 
Wakati Yanga SC wanang'ang'ana na saa 24 kupewa taarifa. TFF wanaweza kuchomoa kwa hicho kifungu cha tatu. Wakisema walichoelezwa na upande wa Serikali kilikuwa ni cha dharura na msingi.

Wakati huo, si kila kilicho cha dharura na msingi kwa TFF, ni lazima kiwe hivyo kwa Yanga SC.

Kuna upenyo wa ki-mamlaka TFF wanaweza kuutumia na kulingana na kwamba wao si kisiwa, bado wanahitaji kufanya kazi vyema na Serikali.

Ukisoma sheria na kanuni tusipende kuutumia mstari mmoja, baadaye ndo tunabwagwa kirahisi sana.

Huwezi kugomea jambo la Serikali, hasa pale unaendesha mambo yako chini ya mwanvuli wake, uwanja wao na ulinzi ni wao. Ili uendeshe hiyo michezo unahitaji ushiriki wa Serkali kwa njia moja au nyingine.

Wakikwambia tuna dharura ya chochote kwa tukio linaloenda kutokea hapo uwanjani huwezi kuvimba ukaendelea kwani huwezi kujibeba kivyakovyako.

Mengine tunabaki ni ushabiki na ukereketwa tu.

View attachment 1778287
Hiyo sababu TFF waliitaja? Hivi ushajiulizaga kwanini FIFA huwaga wana sisitiza mambo ya mpira serikali haitakiwi kuingilia?

Eddo Kumwembe mchambuzi na mshabiki wa Simba.👇👇

Mmemaliza kuongea na mimi niongee? Haya....walichofanya Yanga jana ni kuwatia adabu wanasiasa tu...kanuni na sheria lazima zizingatiwe kuliko busara na hekima...barua haijaeleza hata sababu ya kusogeza mechi mbele. Unaweza kuwalaumu TFF lakini miaka ya karibuni kuna ujinga umeenea ule wa 'maagizo kutoka juu'...maagizo gani bila ya ufafanuzi? Ndio maana fifa haitaki serikali iingilie mpira. Sehemu ambazo serikali inaingilia mpira ni kupitia watu wa ulinzi na usalama pamoja na watu wa hali ya hewa. Kama United na Liverpool ilivyovunjwa majuzi kwa sababu za kiusalama ambazo kila mtu amezielewa. Wakati mwingine hata snow usogeza mechi mbele na hapo ndipo watu wa hali ya hewa wanatuamulia mechi. Vinginevyo haiwezekani tu eti mtu anamsubiri mpenzi wake yupo saluni atuambie tusogeze mechi mbele. Hasara za mashabiki nani anawalipa? Fifa wanataka sana mpira uchezwe lakini wakipelekewa issue hii ya jana nahisi wataiandikia Yanga barua ya pongezi.
 
Namba tatu inamaanisha tff wao wanaweza kubadili mda wa mchezo husika,hapo hapo kinasema kwa sababu ambazo Tff italizika na sababu hizo,hapa sheria imetaja ikilizika TFF,sasa Tff walitakiwa wawaite viongozi wa timu zote mbili na waongee nao kuna mabadiliko ya mda yametokana na sababu hii na hii.unavyosema tumesogeza mda wa mchezo kwa maelekezo kutoka serikalini maelekezo ambayo wadau hawayajayajua kunaleta sintofahamu,

Fifa inakataza serikali kuingilia maswala ya mpira.sasa kama wao Tff jeuri iwachukulie hatua yanga ya kuipokea pointi,kisha Yanga nao waende Fifa wakaishtaki tff kwa jambo hili la kubadili ratiba kwa sababu wameambiwa na serikali
FIFA kama upuuzi huu ukifika mbele ya meza yao TFF inakula faini na nchi inafungiwa kujihusisha na maswala ya mpira.
 
Mwaka 2016 Yanga walimsajili Mrisho Ngasa na wakati akiwa na mkataba na Azam na Simba hivyo Yanga walivunja kanuni za usajili ilitakiwa kwanza Yanga iwasiliane na Simba maana mchezaji alikuwa kwa mkopo Simba akitoka Azam badala yake TFF haikuipa adhabu Yoyote Yanga ilitakiwa Yanga afungiwe asisajili kwa mujibu ya sheria hapa TFF walibeba Yanga nimeshakupa mfano kuwa TFF wanazibeba sana Simba na Yanga
Unajua Sheria mzee, hebu tuanzie hapo kwanza
 
Hiyo sababu TFF waliitaja? Hivi ushajiulizaga kwanini FIFA huwaga wana sisitiza mambo ya mpira serikali haitakiwi kuingilia?

Eddo Kumwembe mchambuzi na mshabiki wa Simba.👇👇

Mmemaliza kuongea na mimi niongee? Haya....walichofanya Yanga jana ni kuwatia adabu wanasiasa tu...kanuni na sheria lazima zizingatiwe kuliko busara na hekima...barua haijaeleza hata sababu ya kusogeza mechi mbele. Unaweza kuwalaumu TFF lakini miaka ya karibuni kuna ujinga umeenea ule wa 'maagizo kutoka juu'...maagizo gani bila ya ufafanuzi? Ndio maana fifa haitaki serikali iingilie mpira. Sehemu ambazo serikali inaingilia mpira ni kupitia watu wa ulinzi na usalama pamoja na watu wa hali ya hewa. Kama United na Liverpool ilivyovunjwa majuzi kwa sababu za kiusalama ambazo kila mtu amezielewa. Wakati mwingine hata snow usogeza mechi mbele na hapo ndipo watu wa hali ya hewa wanatuamulia mechi. Vinginevyo haiwezekani tu eti mtu anamsubiri mpenzi wake yupo saluni atuambie tusogeze mechi mbele. Hasara za mashabiki nani anawalipa? Fifa wanataka sana mpira uchezwe lakini wakipelekewa issue hii ya jana nahisi wataiandikia Yanga barua ya pongezi.

Suala ni uelewa si ushabiki.
TFF haiwezi ku-survive peke yake kamwe mambo inayofanya bado yanaihitaji serikali, ni mtambuka.

Usione mpira unachezwa kirahisi, kuna mambo ya ulinzi na usalama. Kwa mfano siku umepanga mechi ukaambiwa tuna tukio jingine linalohitaji wana usalama, utavimba tuu na kusema hatuingiliwi na serikali? Siku unataka kuutumia uwanja ukaambiwa kuna shughuli ya serikali au chama kwa viwanja vya vyama utavimba tuu na kusema FIFA inasema .....

Serikali imewapa TFF sababu zao, wao walitakiwa kujitathmini na kutoa maamzi kama sababu zinakidhi. Hakuna aliyekamatwa huko TFF na kushinikizwa akubali hoja ya serikali.

Suala la msingi ni je hili la jana kulikuwa na udharura na mhimu?

Kuna mambo si ya kwako moja kwa moja kama yakitokea mfano: tishio la kiusalama, utasubiri uambiwe kuna taarifa ya kuwepo kwa mabomu ndo ukubali kuahirisha mpira?

Tujitathimini?
 
Walitoa sababu ipi,mbona kipindi fulani walizuia sherehe kama sikosei kwa maene ya Masaki na Msasani wakasema sababu za kiusalama,Jana walitoa sababu gani TFF?

Hamna ushabiki siku zote sheria ya FIFA serikali haitakiwi kuingilia mambo na maamuzi ya mpira wa miguu,hili jambo kwa jicho lako unaliona dogo ila likifika FIFA TFF na nchi kiujumla inafungiwa tutaishia kuwa wa humu humu ndani.
 
🐒🐒🐒
098776111.jpg
 
Walitoa sababu ipi,mbona kipindi fulani walizuia sherehe kama sikosei kwa maene ya Masaki na Msasani wakasema sababu za kiusalama,Jana walitoa sababu gani TFF?
Ndiyo maana nimekueleza kuwa kuna sababu ambazo unaweza kuzieleza moja kwa moja kwenye jamii na kuna ambazo huwezi kuzieleza kulingana na msingi wa tatizo husika.

Mimi na wewe hatujui kama kulikuwa na sababu na ni ipi. Ila nakupa mazingira tofauti yanayoweza kujitokeza.
Viongozi wa timu walipopigiwa simu mara ya kwanza walielezwa au la?

Tujikite kwenye hili la jana, je Serikali ilikuwa na sababu za msingi ambazo ni dharura na TFF kujiridhisha juu ya hilo?
Kama sababu hazina mashiko then wanaubeba mzigo.

Lakini pia una haki ya kujua kuwa kuna siku pia hutapewa sababu moja kwa moja, utaambiwa tu milango inayopitika ni ile kule na elekea upande ule. Si kazi yako kuhoji wakati ule, baadaye utapewa taarifa rasmi.

Jaribu kupitia kwenye issue za majanga na uokozi. Hivyo, tusishupaze shingo.

Sasa hivi tuna haki kamili ya kujua tatizo la msingi lakini kama una haki nayo, mengine ni ya wakubwa. TFF vs wizara watasema hii inahusika na watu fulani hivyo hatuna haki kulisemea.
 
Yanga hawajaigomea tff wameigomea serikali bahati mbaya yao wamefanya uamuzi kwa kukurupuka wakidhani wanawakomoa TFF. tnaenda kuona gsm wakiyumbishwa mpaka waombe poo.
 
Tatizo TFF wenyewe hawajaweka wazi Sababu ni zipi za kuhairisha game. Maana watu makini tunaweza kuona umuhimu wa sababu. Ila kutokusema hizo sababu ndio shida
 
Back
Top Bottom